Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania Kadinali Pengo

Kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana alielezea msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu tiba ya Loliondo inayotolewa na Mchungaji Ambikile Mwaisapile kuwa kabla mtu yeyote hajapata tiba hiyo lazima ajiulize maswali manne kwanza kabla ya kuamua kuitumia.

Akihutubia katika Ibada ya Jumapili katika Kigango cha Mt. Yohane wa Msalaba Parokoa ya Mbezi Luis, Paroko wa parikoa hiyo Padre Vivian alisema, "Sina chuki wala tatizo lolote na tiba ya Loliondo, lakini kama unataka kwenda lazima ujiulize maswali manne yafuatayo.

"Kwanza, tiba inayotokana na miujiza ya Mungu lazima iwe endelevu isiwepo kwa kipindi kifupi tu," alisema.

Swali la pili alilotaka watu wajiulize ni kuwa tiba inayokuja kama muujiza kutoka kwa Mungu huwa na masharti? Swali la tatu alilolitaja Paroko huyo ambaye ni Padre wa Shirika la Wakalmeli ni kuwa, Kama tiba hiyo inafanya kazi ndani ya Loliondo, kwanini isifanyekazi Dar es Salaam na kwingineko?

Na swali lake la mwisho alilotaka watu wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo UKIMWI ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?

"Ukiisha jiuliza maswali hayo na kujiridhisha kwa majibu utakayopata unawea kufanya maamuzi ya kwenda Loliondo. Hivyo ukiliona basi limeegeshwa katika stendi ya Mbezi au mahali pengine na ukasikia wapigadebe wanaita Loliondo Loliondo Loliondo, basi panda ukapate kikombe cha Babu," aliongeza kusema.

Katika siku za hivi karibuni Mchungaji Mwaisapile ameutikisa Ulimwengu baada ya kutangaza kuwa anatibu magonjwa sugu kwa kutoa dozi ya kikombe kimoja cha dawa ya kienyeji kwa gharama ya shilingi 500/ kwa Watanzania na Tsh 1,000/= kwa wageni.

Viongozi mbalimbali wa siasa na dini wakiwemo maaskofu wa madhehebu ya Kikristo wamekuwa wakitoa ushuhuda wa ukweli wa tiba hiyo na kuwashauri wananchi wenye magonjwa sugu kwenda kijijini Samonge mkoani Arusha kupata tiba.

Hata hivyo kwa upande mwingine, baadhi ya viongozi wa makanisa hayo akiwemo Askofu Zakaria Kakobe wa kanisa la FGBF na Mchungaji Christopher Mtikila wamekuwa wakiipinga vikali tiba hiyo.

Source: mbs

Kanisa Katoliki lina msimamo ufuatao kuhusu mafundisho yake:

1. Mambo yote yanahusu imani kwa Mungu na namna ya kuiishi hiyo imani - inagusa mafundisho makuu, ambayo inabidi tuyafuate (mfano, kumpenda Mungu kwa moyo wetu wote, kwa nguvu zetu zote, kwa akili yetu yote na kuwapenda jirani kama tunavyojipenda wenyewe/kama tunavyotaka tutendewe nao).

2. Mafundisho yote yanayofuata imani binafsi (mfano, kipaji cha uponyaji au karama nyingineyo) inabaki ni uhuru wa mwumini mwenyewe kulingana na jinsi anavyoona itamfaa kumwongezea imani au kumfanya awe karibu na Mungu.

3. Hivyo, ningesema: kwa tiba ya Loliondo, Kanisa Katoliki linaacha waumini wake watumie utashi wao kulingana na jinsi wanavyoona inawaongezea ibada kwa Mungu au la! Kama inawaongezea wanaweza kuiamini na kama haiwaongezei wanaweza (kulingana na dhamiri yao njema inavyowatuma) kuiacha.
 
....lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. .

Pole sana ndugu;
hapo umeeleza vizuri kabisa - hakuna dawa ya kifo;
Na babu hajasema dawa anayotoa inatibu kifo; muda unafika Mungu akakupenda zaidi, basi anakuchukua!
 
Pole sana siku yake ilifika tu, mimi bosi wangu ameenda na sasa yuko fiti sana ameanza hadi kula vyakula alivyokataliwa na doc
 
Pole sana ndugu;
hapo umeeleza vizuri kabisa - hakuna dawa ya kifo;
Na babu hajasema dawa anayotoa inatibu kifo; muda unafika Mungu akakupenda zaidi, basi anakuchukua!

That is true, muda ukifika utaondoka tu.
Babu hatoi dawa ya kuishi milele.
Pole sana wafiwa sote tusafari moja but muda na wakati aujua muumba wetu.
Wengi wamekunywa dawa kwa babu na wanaendelea vyema tumshukuru mungu kwa kila jambo.
Mungu ampumzishe mahari marehemu pema peponi
 
ww utakuwa wa2 kutoka mwsho cz mm nlshasema hta atokee m2 ankate kchwa, babu cwez kumwamin hta kdgo! Pole ulyefwa na shemejio. Mung ailaze rho yke pema pepon! Asbh wkt nafka ofcn, akaja mama mwnye ofc na majonz tele, shemejie amerd jana kpata kkombe, hakuwa na hal mbya ila alpofka 2 nymbn hal ikaw tofaut, amefark uck wa kuamkia leo. So huyu ni m2 wa2 kufa baada ya kunyw dawa kw babu. Alkuw na sukar na alkatza doz! RIP WOTE!
Asante kwa ushuhuda pole sana mkuu, mimi nitakuwa wa mkristu wa Mwisho TZ kumwamini huyu babu.
 
Pole mkuu, bahati mbaya watu wako desperate hawawezi kufikiria kabisa na hawaambiiki kitu.
 
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.
Sijakuelewa mantiki ya kuleta hii thread humu,hadi sasa unaleta hii habari bado hauna imani na ndio maana unasaka watu walete ushahidi ili wajiridhishe.Babu kule yuko wazi ukichakachua unakunywa maji.Mwenyewe umelonga kuwa hakuna dawa ya kuponya kifo kwa hiyo unacholaumu ni nini!!!Unaogopa kusema ukweli kuwa huwa imani na tiba ya babu ila unatumia lugha rafiki ili usishambuliwe humu.Hakuna mtu ambae hataonja mauti hivyo kubali matokeo tu kwani hata wale waliofufuliwa na yesu(kwa imani yangu) mwishoe walikufa.na hata ambao watajitokeza kutoa ushuhuda wa babu mwisho wa siku watakufa tu.suala ni timeframe huyu kakaa siku ngapi huyu miaka mingapi.huo ndio ukweli
 
Pole sana kaka na r.i.p dada yetu. Jamani babu hajasema ukinywa dawa yake hufi,unywe usinywe kifo kiko palepale. Huko tunaenda kurefusha cku tu.
 
Jamani babu hatoi uzima bali ni tiba ambayo ipo kiimani zaidi.
Hivyo watu kufa itatokea na itaendelea kutokea, hata hosp watu wanakufa kila saa japo kuna tiba za kila aina.
So kama huamini usimkwaze anayeamini, babu hajawahi kufanya pr campaign kuwavuta watu bali ni ushuhuda sa watu ndio unaovuta watu.
 
Pole sana
1. tunatakiwa kuelewa kwamba babu hatoi dawa ya kuzuia kufa
2. mtu yeyote siku yake ikifika imefika awe amekunywa dawa ya babu au la
3. kwa tatizo la huyo mgonjwa tayari alikuwa katika hali ya mwisho kufikia mauti

kuna wagonjwa ambao wamepona hawana muda wa kukuletea wewe uthibitisho
wanachojua kwa sasa kwamba walikuwa wagonjwa sasa wamepona
kumbuka hili ni swala la kiimani
 
pole sana kwa msiba ila naomba ujue kwamba kuna dawa ya babu na mapenzi ya Mungu.hata ukinywa dawa ya babu kama muda wa kuitwa kurudi kwa BABA umefika ni lazima utatuacha tu.
jina la Bwana lihimidiwe
 
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi kwa Babu wiki mbili zilizopita ili kupata dawa kutokana na maradhi ya Breast cancer ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu. Kama sote tunavyojua hakuna dawa ya kutibu kansa, lakini baada ya kusikia habari za Babu tulijenga imani kuwa huenda akapona. Tulimpeleka huko, na baada ya kukaa siku mbili kwenye foleni alibahatika kupata dawa na kuinywa. Lakini toka anywe hiyo dawa hali yake imekuwa sio nzuri na kudhoofu siku hadi siku hadi hii leo saa nne asubuhi amefariki dunia. Ninatoa ushuhuda huu si kwa kuwakatisha tamaa watu la hasha bali ni kutaka kuweka vitu hadharani ili watu wajue kuwa pamoja na kuwa huenda dawa hiyo ikawatibu baadhi ya watu lakini watu tujue pia hakuna dawa ya kuponya kifo. Huenda kweli babu anatibu kwa imani, lakini sidhani kama wale wote wanaoenda huko hawana imani. Namalizia kwa kuzidi kuwaomba waliotibiwa na kupona kweli wajitokeze watuthibitishie kwa ushahidi wa kitabibu.

umeandika vizuri sana. natamani watu wasome na waelewe. kupona ugonjwa siyo kupona kifo. kama kifo chako kimepangwa kutimia kwa ugonjwa,basi hata kama dawa ya ugonjwa huo ipo na umetumia kifo kitakuja tuuu.

ni vema tukaelewa kuwa kutumia dawa ya Babu siyo kuepuka kifo, bali ni kupona ugonjwa , hata wale wote walioponywa na Kristo Yesu baadae walikufa. Tukeshe tukiomba kwakuwa hatujui saa ya hukumu yetu
 
Na kweli haumwi laiti angejua!!!! Mbona mimi Shangazi yangu amepona kabisa alikuwa na ugonjwa wa moyo. Maisha yake yote ni vidonge anavyovichukua hapo THI na toka amekunywa kikombe kwa babu hii week ya tatu na yuko fit.
 
Kumbukeni Marais hawa Bomedien wa Algeria na mfalme wa Syria na wengine wengi vifo vyao,pamoja na kuzungukwa na maproffessional doctors lkn siku au saa ilipogonga walirudisha no. kwa hiyo kama jamaa walivyosema hapo juu kkombe isn't a guarantee that u cant ded
 
umeandika vizuri sana. natamani watu wasome na waelewe. kupona ugonjwa siyo kupona kifo. kama kifo chako kimepangwa kutimia kwa ugonjwa,basi hata kama dawa ya ugonjwa huo ipo na umetumia kifo kitakuja tuuu.

ni vema tukaelewa kuwa kutumia dawa ya Babu siyo kuepuka kifo, bali ni kupona ugonjwa , hata wale wote walioponywa na Kristo Yesu baadae walikufa. Tukeshe tukiomba kwakuwa hatujui saa ya hukumu yetu

anachosema ni kuwa dawa ya babu ime speed up kifo cha shemejie. Kufa kila mtu atakufa hakuna mjadala hapo. si vibaya tukahabarishana na yatokanayo na dawa ya loliondo. kuna mazuri na machungu. Kwa hiyo wale ambao hawajaenda waweza kutafakari zaidi.
 
Pole..RIP marehemu...lakini dawa yoyote ina maelezo, siko sure sana kama dawa ya babu inatibu Breast Cancer!!, sijawahi ona kwenye maelezo yake.
 
Kwa wanajamii wote, naomba kutoa ushuhuda kuwa nilimpeleka mgonjwa wangu mke wa rafiki yangu mpenzi

Hapo mkuu,au wanajamii hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom