Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wamepona mi jirani yangu amepona kabisa ehhe ushahidi gani mnautaka
Mdondoaji na watu wengine mnaodadisi hii 'tiba' ya babu!
Hii sio mara ya kwanza na wala haitakuwa mara ya mwisho kwa watu wa aina hii ya babu wa Loliondo kujitokeza. Mnamo miaka ya 2003 (sina uhakika na kumbukumbu zangu) sehemu za Moshi vijijini alijitokeza mtoto aliyekuwa anatibu kama huyu babu.... kwa kutumia imani na unapewa maji aliyokuwa anayaita ya 'baraka' unakunywa. Alifanikiwa kuvuta umati mkubwa wa watu (japo si kwa kiwango cha babu) lakini japo mwanzoni kulikuwepo na shuhuda za kupona lakini kwa sasa sijui alikoishia. Mambo nililoligundua kuhusu 'watabibu' wa aina hii:
1. Hudai wametokewa na Mungu
2. Huanza kuvuta watu polepole, baada ya muda watu huongezeka sana na mwisho huanza kupungua na 'wanapoishia' hakuna anayekumbuka kuwafuatilia wao wala wagonjwa wao, jambo linatoa mwanya kwa 'waganga' wapya wanapoibuka watu wasifanye rejea ya nyuma.
3. Mara nyingi hutaka kutoa dawa wenyewe kwa mikono yao na wanywaji hunywea papo hapo.
4. Gharama zao zinakuwa ndogo sana au bure.
Mwisho nataka kusema tu hizi ni dalili za watu tuliokata tamaa na tunajaribu kutumia upenyo wowote kutatua matatizo yetu.
padre ana hoja ya msingi. wakristo hawpaswi kushabikia jambo na kilikimbilia kama majuha. padre amewapa vipendele vya kuzingatia kama checklist kabla hawajakurupuka kukimbilia loliondo. najua watampuuza na wameishampuuza sana huyo padre lakini yeye katimiza wajibu wake. Mungu ambariki sana
tatizo watu wameishalewa na mrigariga hawataki tena kusikia maneno ya Mungu yanasemaje!
ooh Lord have mercy on your people. amen
Glory to God
ndugu yangu huyu mtu anahitaji evidence ili awa na uhakika! Jibu ulilotoa ni sahihi kweli? Acha hasira mtu anapouliza swali. Kama huna jibu ungenyamaza tu. Sasa amekosea wapi kuuliza hilo swali? Kwani wewe umeenda? Wapo watu waliokwenda ndio wana jibu. I've seen no mistake in this question.
kama ni kwa jina la Yesu angewahubiria watu waokoke sio tu kupewa kikombe cha dawa na kuondoka bila wokovu.pole uliyedanganyika. Yesu wetu anataka watu wote waokoke na waijue kweli bwana.
Mbona hatujasikia mahubiri yoyote pale! PALE YESU HAYUKO .IKO MIZIMU YA KWAO NDIYO INAYOTIBU!
Tanzania mambo ya mmpito ni mengi mmno,
miaka ya 80-90's kulikuwa na imani ya kakakuona ,kuwa anatabiri mambo makuu na muhimu,viongozi wa serikali walishiriki ktk hilo zoezi,wanaanchi tukaaminishwa juu ya umuhimu wa kaka kuona na utabiri wa Mvua,Njaa etc
Then ilikuja product moja inaitwa OKO ,inaziba pancha ya gari likiwa in motion,kwamba ukiweka oko ktk gari lako hupati pancha tena,nayo hii ikapita,so kwa babu ni moja ya mozonge ya Tanzania na upeo wetu mmdogo kitaifa wa kupambanua mambo.
Hilo ndio jibu nililoona linamfaa kwa mtizamo wangu.
Kwani watu wengi wamekuwa wa siri na magonjwa yao. Yeye kwa kuwa anataka kupata scientific result aende yeye aje atuwekee matokeo
Dah!!! Mungu wabariki watumishi wako!!! Ushukuriwe Mungu kwa kuwa shauri lako tu ndilo linalosimama. Na mambo yote tunayakabidhi mikononi mwako, ukweli wa mambo haya unaujua wewe Mungu. Utupe neema yako ili tusije tungaamia kwa kukosa maarifa. Ni wewe Mungu uliyetuumba kwa sura na mfano wako, na ni wewe pia unayetulinda na kutuponya nafsi zetu na magonjwa na hila mbaya za shetani.
Ninachokiamini kwako wewe ni wa huruma na Neema huwezi kutuacha tungaamia kwa kutojua ee Mungu. Tulinde sisi na wagonjwa tulio nao uwape afya na nguvu. Utakapofika wakati ulio uamuru wewe mwenyewe uhukumu hukumu ya haki juu ya haya mambo, utupe kuujua ukweli ili huo ukweli utuweke huru.
Amen!!!!
Miss, hata wakati wa Yesu watu walikimbilia miujiza na wakati mwingine mikate na vipande vya samaki. cha msingi ni wewe mwenyewe kulijua, kuliishi na kulitenda Neno.
mkuu, kumbuka kuwa wakati wa Yesu kulikuwa hakuna wakristo. ukristo umezaliwa wakati wa mitume (apostolic era). zingatia sana hili please.
glory to God