Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

Mjadala kuhusu Babu wa Loliondo na dawa yake.

ndodi msanii sana, kanipa dawa ya kuondoa kitambi kumbe kaponda ponda vitunguu swaumu na adala sini, sasa tumbo hiloo utazani nanyea humuhumu. Ulia bei sasa laki 3

Mkuu Ngalangala kumbe nyie ndio mnampa Ndodi kufanya matanuzi.

Nimebahatika kusafiri mara kadhaa na huyu bwana, jamaa yeye na vile vibinti ni mwendo wa Business Class.
Hotel za ukweli tu, kama mnampa 300k kuondoa kitambi kinachosababishwa na lager muda si mrefu ataanza kukodi Jet ya Kikwete.

Big up Babu wa Loliondo!
 
babu udumu daima milele,,,,,uisaidie serikali yetu mizigo ya kulaza wagonjwa miaka,,,,ubarikiwe sana kwa kupunguza wagonjwa majumbani kwetu,,,,,huyu ndondi amejitahidi kuijaza account yake adhani account yake inasoma kama ya lowasa,,mitishamba ya bure haiwezi kuuzwa beikubwa kama yake,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
 
Babu amezingatia zaidi kuhakikisha binadamu wanapona tu na hatoi kinga yeye anatoa tiba kwa hiyo kumfananisha na ndondi ni sawa na kumfananinisha mwewe na kumbikumbi
 
Yani ujio wa huyo babu umetufungua macho kwa hao wanaojifanya watu wa Mungu kakobe na huyo anaejiita dr badala ya kufurahia maajabu ya Mungu wao wanamponda km kweli wao ni wa2 wa Mungu mbona kazi zao zinalenga kujinufaisha wao. 2megundua kuwa kwa sasa wa2 wa dini wanaitumia dini vibaya ku2lia pesa 2nazohadaiwa kuwa 2namtolea Mungu kwa kisingizio cha sadaka
 
Babu uzuri wa bei yake ndio unaonesha wazi kwamba ametumwa na mungu, sio huyu msanii ndodi eti dozi ya minyoo sh laki nne, mbwa kabisa huyu.


Mie price ya Dr Ndodi ndo huwa inaniacha mdomo wazi
 
ndodi msanii sana, kanipa dawa ya kuondoa kitambi kumbe kaponda ponda vitunguu swaumu na adala sini, sasa tumbo hiloo utazani nanyea humuhumu. Ulia bei sasa laki 3

hahahahahah hii kali laki tatu kupunguza kitumbo mswede,kumbe umepewa vitunguu swaum hahahahaah:wink2:
 
Babu kaja kuwaambieni akina Ndodi ni watu wa aina gani, mjihadhari nao. Kama wao ni watu wa Mungu kwa nini wajinufaishe iwapo ujuzi huo wamepewa na Mungu kweli? Bila shaka wamejifunza kwa Shetani!!!!
 
Kabla hatujamsifia babu tujiridhishe kama kweli dawa yake inafanya kazi. Yaani ithibitishwe kwa vipimo vya kitaalamu kabla na baada ya kutumia. Hata kakobe aliwahi kusema anaombea na watu wanapona ukimwi, lakini kuna mtu ambaye baada ya maombezi kwa kakobe hakusumbuliwa na maradhi kwa muda wa miezi 6, then alipougua tena ikawa moja kwa moja(akafa). Ninamaanisha, kile kinachoitwa nafuu/kupona kunatokea kwa muda tu kwa sababu mtu anakuwa amepata tumaini kwamba dawa inaponyesha wakat ukweli haiponyi. Tukumbuke kuwa kuishi kwa matumaini kunapunguza makali ya ugonjwa wa ukimwi, tumaini ni kitu kikubwa sana katka maisha.

Vile vile tuwe macho na watoa tiba kwa njia mbadala-jadi (ambao kwa sasa wameibuka kwa wingi), wengi wao wanatumia magonjwa yetu na kukosa tumaini la matibabu bora kujinufaisha.
 
we nawe tutolee mazingaombwe hapa.

Hujanielewa ndugu yangu, namaanisha kwamba kweli hii ni dawa kutoka kwa Mungu, dawa ambayo ni kama inatolewa bure ili watu wote wapone. Nimelinganisha na sukari kuonyesha kwamba kama Babu angekuwa amekaa kibiashara zaidi angeuza kwa mamilioni. Pole sana kama nimekukwaza ila naamini tuko pamoja.
 
ndodi msanii sana, kanipa dawa ya kuondoa kitambi kumbe kaponda ponda vitunguu swaumu na adala sini, sasa tumbo hiloo utazani nanyea humuhumu. Ulia bei sasa laki 3

Mungu wangu, kuna watu mmeshaingizwa mkenge na huyu tapeli?
 
Kwa nini watu washindane kwa karama walizopewa na Mungu? Huyo ndodi ni wa ajabu sana.
 
nani kathibitisha kuwa iyo dawa inaponya?huo ukimwi?
 
Tiba ya Loliondo yamtisha Kakobe

Mussa Juma, Loliondo na Nora Damian
WAKATI idadi kubwa ya wagonjwa wakionekana kumzidi nguvu mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapile, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe ameingia hofu ya kupoteza waamini kufuatia taarifa kwamba mchungaji huyo anatibu Ukimwi.

Jana akihubiri katika kanisa lake lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Askofu Kakobe alisema uwepo wa mchungaji Mwasapile unatishia vituo vya maombezi vinavyofurika mijini kubaki vitupu kutokana na watu kukimbilia Loliondo.
Habari kutoka Loliondo zinasema wakati watu wakiendelea kufurika nyumbani kwa mchungaji huyo ili kupata matibabu, mamia ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa mchungaji Mwasapile.
Mwasapile(76) ni mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) na Inadaiwa kuwa anatibu magonjwa sugu ukiwemo Ukimwi.
Mwananchi lilishuhudia mamia ya watu katika maeneo kadhaa ya jiji la Arusha na mji wa Mto wa Mbu kwenye barabara inayoelekea Samunge kupitia Engaruka na Ngaresero umbali wa takriban kilometa 400 toka Arusha mjini.
Taarifa zinasema kuzidi kuongezeka kwa idadi hiyo kumechangiwa na baadhi ya ndugu za wagonjwa wa HIV, Saratani, Kisukari na pumu waliokuwa wamelazwa katika hospitali mbali mbali nchini, kuwaondoa wagonjwa hao na kuwapeleka kwa mchungaji huyo.
Hali za baadhi ya wagonjwa zimeelezwa kuwa ni mbaya na wengine bado wamekwama njiani ambapo hadi jana vilikuwa vimeripotiwa vifo vya watu wawiliambao walifikishwa Loliondo kwa lengo la kupatiwa tiba.
Mwandishi wa Mwananchi alishuhudia idadi kubwa ya magari yakifika kwa mchungaji huyo, huku wagonjwa wakiwa kwenye magodoro na wengine wakiwa hawajitambui kutokana na maradhi.
Hali hiyo pia inachangiwa na masharti ya dawa hiyo, ambapo mchungaji Mwasapile anasema, hairuhusiwi kusafirishwa na ni yeye pekee kwa mkono wake akikupa ndipo utapona.

Uhaba wa Magari
Mbali na uhaba wa magari, pia gharama za magari ya kukodi na mabasi zimepanda.
Magari ya kukodi kwenda na kurudi kijiji cha Samunge wilayani Ngorongoro, alipo mchungaji huyo imefikia kati ya Sh100,000 na Sh150,000 kwa mtu mmoja huku nauli za mabasi zikiwa ni kati ya Sh50,000 na Sh80,000.

Bei ya magari ya kukodi siku tatu ziliyopita ilikuwa ni kati ya Sh50,000 hadi 80,000 ambapo mabasi ya kawaida nauli ilikuwa ni kati ya Sh14,000 hadi 20,000.

Watu kuongezeka
Mchungaji Mwasapile alisema juzi kuwa idadi ya watu watakaofika kupata tiba inatarjiwa kuongezeka na kwamba ameoteshwa kuwa watu watatoka mabara mbalimbali na kwamba itamchukuwa mwezi mmoja mtu mmoja kupata tiba.

Dalili za hali hiyo, zimeanza kujidhihirisha kwani tofauti na awali ambapo kwenda kupata dawa na kurudi ilikuwa ni safari ya siku moja, hivi sasa maelfu ya watu kutoka mikoa mbali mbali nchini, wapo kwa mchungaji huyo kwa zaidi ya siku tano na hawajafanikiwa kupata tiba.
Mchungaji Mwasapile anadai kuwa alioteshwa na Mungu kuhusu dawa hiyo inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga, tangu mwaka 1991 lakini alisubiri hadi mwaka jana alipoanza rasmi kutoa tiba.
Alitahadharisha watu wenye virusi HIV ambao watakaokunywa dawa hiyo na kupona kujikinga na maambukizi mapya, kwa kuwa mgonjwa haruhusiwi kunywa dawa hiyo mara mbili.
"Wanaopona HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambuki kwani hawatapona tena...; Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.
Msaidizi wa mchungaji huyo, Marko Nedula alisema kuwa watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya wilaya ya Ngorongoro hasa kutokana na wenyeji kudharau awali.
"Hawa wanaoleta vurugu leo hapa, mchungaji aliwambia siku nyingi njooni mpate tiba lakini walidharau,"alisema Nedula.

FFU waongezwa
Kutokana na maelfu ya watu kufika katika kijiji hicho kupata tiba jeshi la polisi mkoani Arusha, limelazimika kuongeza askari wa kutuliza ghasia(FFU) katika eneo la mchungaji huyo.

Askari hao, wamekuwa wakisimamia na kupanga watu ili kupata tiba na kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho, ambacho hakina huduma za kulala, vyoo, hoteli wala umeme.
Akizungumzia hali ya sasa Loliondo, Mkurugenzi wa kampuni ya kukodi magari ya Sanufa , Said Kakiva aliomba serikali kuingia kati suala hilo kwa kupeleka mahema eneo la tiba na kukarabati barabara.
"Mimi magari yangu yote yamekodishwa kupeleka wagonjwa, kwa huyo babu, lakini, barabara ni mbaya sana na kule hakuna huduma zozote muhimu kama mahala pa kulala na chakula,"alisema Kakiva.
Alisema suala la matibabu ya magonjwa sugu Lilondo serikali inaweza kulifanya ni sehemu ya kutangaza utalii kwani, watu wa mataifa mengi wanafika kupata tiba ambayo inatokana na miti ya asili ya Tanzania.
"Serikali itengeneze sasa barabara, kwani barabara hii ndiyo iliahidiwa lami na rais na inakwenda hadi mkoani Mara,"alisema Kakiva.

Hofu ya Askofu Kakobe
Askofu Kakobe alisema Watanzania wengi wanapenda uwongo kuliko ukweli na kutahadharisha kuwa kutokana na kuwepo mtu huyo watu hawatasubiri tena maombezi bali watapukutika kwenda Loliondo."Hofu yangu iko katika vituo vya maombezi vilivyofurika mjini, wakati huu vitabaki tupu, watu wataenda Loliondo na hawatasubiri tena maombezi,"alisema Kakobe na kuongeza :

"Tukisema tusubiri serikali ama TFDA ituthibitishie itakuwa ngumu maana kila mmoja anatia bidii kama polisi na wengine".Alisema kanisa lake litaendelea kuwepo na kamwe haliwezi kutikiswa na Loliondo na kujigamba kuwa wanaweza kumsambaratisha mchungaji huyo.
Kakobe alieleza kuwa kwake yuko muhubiri wa Injili iliyo hai na ambayo iko ndani ya Biblia huku akikumbusha mtu aliyemwita 'Babu wa Tegeta' ambaye alijitokeza miaka ya nyuma na kudai kuwa anatibu Ukimwi ambaye alisema walimsambaratisha.Kakobe ambaye alitumia muda mwingi kunukuu vifungu mbalimbali vya Biblia, alisema mfumo wa uponyaji wa Mungu umeshafunuliwa na kwamba kwa sasa hawahitaji Mungu yeyote atoe ndoto.
"Hizi ni nyakati za mwisho, unatakiwa kuchagua kanisa ambalo utaongozwa katika haki na si kupeperushwa kama karatasi,"alisema Kakobe huku akishangiliwa na waumini wake.Aliwatahadharisha waumini wake akiwataka kuwa makini na mchungaji huyo huku akimtuhumu kwa kudai kuwa anatumia nguvu za giza.
"Kama umesikia mtu fulani anafanya maombezi la kwanza la kujiuliza je ameokoka kwa sababu Mungu hatendi kazi na watu ambao hawajaokoka, lazima awe anahubiri Injili,"alisema.Askofu huyo alitumia ibada hiyo kuwahamasisha waumini wake kumpinga mchungaji huyo kwa maombi huku akitamka:
"Kanyaga Babu wa Loliondo, sambaratisha babu wa Loliondo, kazi za babu saga."Kakobe alikwenda mbali zaidi na kumfananisha mchungaji huyo na mganga wa kienyeji huku akijigamba kuwa hata kanisani kwake watu waliokuwa na Ukimwi walipona."Tusibabaishwe na Ukimwi, hapa tumeombea watu wamepona Ukimwi na vithibitisho vya vyeti vipo,"alisema Kakobe na kushangiliwa na waumini wake ambao baadhi yao walisikika wakisema, "tupo."
Kakobe alisema hata kama mtu huyo angekuwa anatibu kwa Sh1 kwenye Neno la Mungu haikubaliki na kueleza kuwa maandiko yanasema, 'mmepewa bure toeni bure.'Katika hatua nyingine, askofu Kakobe alisema matatizo ya umeme nchini hayataisha hadi waziri wa Nishati na Madini aende akatubu kanisani kwake.Alisema mambo yanayojitokeza sasa ni matokeo ya yale waliyoyafanya Tanesco kanisani kwake na kutaka Ngeleja akatubu ili matatizo yaishe.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Mtazamo wangu
Nilitarajia Kakobe angemsifu Mchungaji mwenzake kwa kupunguza wagonjwa mitaani, yeye kakalia kumponda. Sijafurahishwa na maoni yake hata kidogo.
 
ndodi msanii sana, wewe ukitaka kulifahamu hilo msikilize kipindi chake ataishia kutaja taja magonjwa tu halafu tiba umwone yeye
 
Back
Top Bottom