Mjadala kuhusu Elimu ya Tanzania: Je, Tanzania ina Uhaba wa Ajira au Uhaba wa Wataalamu?

Mjadala kuhusu Elimu ya Tanzania: Je, Tanzania ina Uhaba wa Ajira au Uhaba wa Wataalamu?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Habari za wakati huu;

Kwanza nieleze kwa uwazi kabisa kwamba huu mjadala ni wa wazi hauna lengo la kubomoa bali unalengo la kujenga.
Kati ya mwaka 2016-2019 nilishirika katika utafiti mkubwa ambao ulikuwa na husu swali zima la Nguvu kazi(Labour Force).Katika utafit nilijifunza mengi sana ikiwapo historia, maendeleo na dhana ya Nguvu Kazi.Tulitazama Nguvu kazi ya dunia, Maeneo ya kiuchumi, kanda, mabara, mataifa na nchi moja moja. Tulitazama pia sekta mbalimbali za kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya ulimmwengu ikiwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea ikiwamo China, Uingereza na Tanzania.

Nilibahatika kujifunza mengi kwani pamoja na kwamba sikuwa mtaalam katika utafiti huu lakini nilipewa nafasi ya kipekee ambayo iliniwezesha kusoma maandiko mengi,kushiriki katika mijadala mingi na hata kupitia takwimu na taarifa nyingi. Utafiti ulikuwa unalenga sana kuelewa Changamoto za ulimwengu katika swala la Nguvu Kazi. Baadhi ya mambo tuliyotafiti yamejadiliwa katika tafiti na ripoti mbalimbali ikiwamo World Development Report 2020.

Moja kati ya swali ambalo tulijiuliza ni juu ya Mchango wa elimu kama ilivo katika mfumo wa sasa katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na Nguvu kazi yenye TIJA.Hoja ilikuwa ni iwapo elimu ya sasa inamuaandaa msomi kwa ajili ya kufanya kazi za huko mbeleni kwani kwa mkasi ya maendeleo ya dunia tunaona kabisa kutaibuka aina nyingi mpya za kazi na pia aina nyingi sana za kazi kama tunavozifahamu sasa zitatoweka teknolojia kama AI,ML,IT,Space Technology,Robotics,etc zitabadilisha sana fani nyingi ulimwenguni swali ni Je tunawaandaaje watoto wetu kufanya kazi katika mazingira haya?

Miaka ya nyuma mafaili na nyaraka zote zilihifadhiwa ofisini,zilichapwa ofisini na hakuna namna mtu angeweza kufanya kazi bila kwenda ofisini lakini hali imebdailika kwa sasa.Ninapoandika andiko hili niko nyumbani kwangu,kwenye ofisi yangu ambayo iko nyumbani ambapo katika ofisi hii yangu ndgu ninahudumia wateja zaidi ya 50 ambao ni individuals,na kampuni 14 na kwa siku na pokea simu za kazi zisizopungua 20 na kuandika email zisizopungua 20 na kupokea email zisizopungua 20.

Kazi hii naifanya na wasidizi wawili tu ambao kila mmoja yuko nyumbani kwake na tunaunganishwa na mfumo wa kompyuta tu kufanya kazi zetu. Haya ni mabadiliko makubwa sana katika teknolojia. Ukiitazama workload yangu na project ambazo tunafanya utaona kwamba zinahitaji watu wengi zaidi na eneo kubwa zaidi lakini mimi natumia less space, less time, less resources huku nikitengeneza value kubwa kwa ajili yangu na wateja wangu.

Swali la kujiuliza ni Je kama katika udogo wa mtaji wangu na uwezo,uchache wa fursa,changamoto za kibiashara na kiuchumi nimeweza kufanya shughuli zangu nyumbani kwa kipindi chote hiki Je, huko mbele tunakoenda hali itakuwaje? Je, kama kila kampuni ikichagua kutumia mfumo wa teknolojia katika kufanya shughuki zake ni watu wangapi watakosa fursa kwa sababu ya kuwa wazito kujifunza teknolojia mpya? Je, tunawaandaaje watoto hawa na wafanyakazi hawa kwa ajili ya fursa zijazo?Tunawapa elimu itakayowafaa?Tunawapa skills zitakazowafaa?Tunawapa ujuzi utakaowafaa?

Mwaka Jana nilianza kufanya maandalizi ya Program mpya ya MVP (Managed venture Program) Ilikuwa ni Program nzuri sana na ya kipekee na ambayo na amini ingekuwa moja kati ya Program za mwanzo kabisa kama hizo hapa nchini.Itakapokamilika Program hii itaongeza Productivity ya wasomi wetu kwa asilimia 200 yaani kama mtu anafanya kazi yenye thamani ya TZS 1,000,000 basi atakuwa anafanya kazi ya 2,000,000 katika program hii.

Katika hatua za mwanzo nilipata watu wengi sana ambao walitaka kushiriki mpaka nikapata wasiwasi wa kwamba naweza nikashindwa ku scale up. Niliwaambia wale ambao walisign up mapema kwamba tutaenda taratibu kwa sababu ni program mpya na lazima nitafute enough skills kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wateja wanapata huduma bora yenye thamani ya pesa zao.Kwa ajili ya Program Hii nilibahatika kukagua CV(Wasifu zaidi ya 1000) nilifanya Interview kwa njia ya simu zaidi ya 200 na za ana kwa ana zaidi 200.

Nilichojifunza ni kwamba kulikuwa na skills GAP kubwa sana katika wote niliozungumza nao hasa katika maswala ya teknolojia.Wengi bado wanaitazama teknolojia kama mazingaombwe na mchezo wa burudani.NIlikutana na wahitimua wa IT ambao walikuwa BUSY kutaka kutengeneza OS zao huku wakiiga fetaures kutoka kwa MS na nikawauliza kitu kitawafanya watu waache Windows OS watumie ya kwako? Nilikutana na watu wanatengeneza Program mbalimba nzuri na za kipekee ila wanakwama kwenye kuzifanya ziiingize Pesa.

Kuna watu wana Passion sana ila hawana mitaji au skills za kutosha na kuna watu wana mitaji na skills ila hawana Passion.Pia kuna ambao wanakuwa na Pasion na skills ili wakipata mitaji huu upande mwingine unapoa.Yaani ni kama vile wamelogwa.Nikakumbuka kauli ya Prof Shivji katika maandiko yake aliposema kwamba Taasisi za elimu zisiwe assembly line za wahitimu bali ziwe kisima cha maarifa, kitovu cha mijadala na kuzalisha maarifa mapya"Prof Shivji alikuwa sahihi kwani vyuo vilikuwa vianshindana kwa vigezo vya udahili na wahitimu huku kukiwa hakuna Publication za aina yoyote ile na hata zile chache zilizopo zikiwa hazina viwango. Ukitembelea vyuo vingi vikuu Tanzania utakuta hawana mfumo mzuri wa kuchapisha maandiko. Wasomi wachache ambao wanakiu ya kuchapa inabidi wahangaike kupeleka machapisho yao sehemu tofauti.Wachache ambao wanachapa kwa bidii ni wale ambao wanakimbiza kutafuta namna ya kula fedha za ufadhili(Grants) huku wakitoa maandiko ambayo hata ukitaka kuwa recite unashtuka kidogo.

Ukija huku mtaani utakuta idadi kubwa ya vijana wakitembeza CV huku wale ambao wako katika maofisi wakiwa wanapiga umbea kwa sababu ama ya uvivu,uzembe. Unakuta Mtumisihi wa serikali au sekta binafsi analala na kazi kwa muda mrefu huku akitumia muda mwingi kuzurura mitaani na mitandaoni na kupiga umbea na kusubiri mshahara utoke. Kwa ufupi unakuta katika masaa 8 ya kazi kwa siku tunatumia masaa 6 katika umbea soga na saga. Tunajikuta kama taifa tuna high unemployment and underemployment.

Jacob Mincer ambaye ni mmoja wa wasomi mahiri kuhusu masuala ya Labour Economics ametafit sana kuhusu changamoto za kufahamu nafasi ya Nguvu kazi katika uchumi. Ni mtu ambaye ukimsoma katika maandiko yako utapata uelewa zaidi juu ya changamoto ya miaka ijayo. Wapo wasome wengine katika eneo hilo ambao wamewahi kutoa michango ya kipekee kama Alvin Toffler aliyesema kwamba "Washamba/Wajinga wa miaka ijayo sio wale wasiojua kusoma na kuandika bali ni wale ambao watashindwa kujifunza,kubadilika na kujifunza upya"Hii sio tafsiri rasmi ila kiingereza chake ni hiki

The illiterate of the 21st century will not be those who cannot read and write, but those who cannot learn, unlearn, and relearn. ”​


Nimeleta mjadala huu hapa baada ya kumsikia Mbunge Kishimba ambaya naamni kabisa anastahili kuwa Education Theorist wa Zama Zetu hapa Tanzania kwa sababu ya namna mtazamo wake kuhusu elimu unavohoji maswala ya msingi katika mfumo wetu wa elimu.Nimeleta mjada huu ili nichokoze mjadala wa kitaifa kuhusu mfumo wetu wa elimu na changamoto zake kwani naamini kabisa ni suala ambalo linahitaji mtazamo wa kila mmoja wetu kwa kadiri ya uelewa wake kwa kuzingatia uelekeo wa elimu yetu.

Ninataka kuchokoza mjadala kuhusu thamani ya elimu yetu(Cost vs Output) Je elimu yetu inatupa Return On Investment tunayostahili au kutarajia?je kuna haja ya kila mtu kuwa na Degree, Masters au PHD?Je kuna haja hata ya kila mtu kuwa na Cheti cha ngazi ya elimu fulani. Je, kati ya Cheti na maarifa yanayomjenga mtu kipi ni Cha muhimu?Je tuendelee kuwa taifa la vyeti, passmark na elimination?Je mfumo wetu wa elimu una mantiki yoyote katika muundo wake wa sasa iwpo shule zetu hazina maktaba, hazitumii teknolojia ya kisasa katika kutoa elimu,hazizingatii uwezo na kipaji cha mwananfunzi, na wala hakizingatii mahitaji ya kijamii na mazingira ya mwanafunzi?

Kuna maswali mengi ya kujiuliza mintarafu elimu yetu na mustakabali wa nchi yetu.Ni maswali ambayo hayahitaji siasa, uchama, udini, ukabila aua hata tofauti za kielimu ziletwazo na vyeti. Ni majadala ambao unahitaji kutazama changamoto zetu katika uhalisia wake na kuzitafutia suluhu kwa pamoja kama askari walioko vitani ambao wajibu wao ni mmoja tu kushinda vita.

Mwandishi wa makala hii anaweza kufikiwa kwa email:masokotz@yahoo.com ili kuendeleza mjada huu nje ya jukwaa hili.

Hata hivyo maoni yote yatakayowekwa hapa yatakusanywa na mwandishi kwa kuzingati uzito wake na kuwasililishwa wizara ya elimu kwa ajili ya mjadala zaidi. Tujitahidi kujadili kwa staha, maarifa, hekima, heshima, utulivu na kama mods itawapendeza basi niwe nimechokoza mjadala wa elimu yetu kwa kuufanya uzi huu uwe sticky thready.

Kuhusu kichwa cha mada hii ningeonmba kibaki kama kilivyo kwani tunatafuta Jibu la hilo swali
 
Mkuu elimu yetu inatakiwa ijikite kwenye practical zaidi na siyo theory kama sasa, una kuta Eng mzima hawezi hata kupiga rangi banda lake mwenye, pia elimu ya kati ithaminiwe kuliko hizi degree ambazo hazina manufaa yoyote.
 
Uhaba ni ajira na sio wataalamu. mara nyingi watu upata utaalamu pale anapokuwa na ajira sababu, kipindi yupo kwenye ajira uwa anafanya kwa vitendo kazi zake. tufikirie tu wale waliotolewa kazini kwa dhana ya vyeti feki unadhani wamekuwa wataalamu kwa kiwango gani?

Mfano,mataifa ya nje yaliowekeza nchini uwaleta maexpert hapa kufanya kazi, ambapo wengi wao hawana sifa za vyeti(taaluma) lakini ni wataalamu katika kazi io, watu waliofanya kazi za kiufundi kwa muda mwingi wamekuwaa wataalamu wa kiwango cha juu sana pasina kutambuliwa kupitia baadhi ya bodi kama ni wanataaluma. Ndo mana kwenye sekta binafsi kigezo cha kwanza ni uzoefu kazini halafu mengine yanafuata.

kwaio kama ajira zinapatikna za kutosha ni rahisi sana kuwaibua wataalamu kupitia ajira hizo.
 
Uhaba ni ajira na sio wataalamu. mara nyingi watu upata utaalamu pale anapokuwa na ajira sababu, kipindi yupo kwenye ajira uwa anafanya kwa vitendo kazi zake. tufikirie tu wale waliotolewa kazini kwa dhana ya vyeti feki unadhani wamekuwa wataalamu kwa kiwango gani?...
So tunaunganishaje haya mambo mawili.Kuzalisha wataalam na kuzalisha ajira maana kwa inavoonekana sasa na kwa maelezo yako ni kama vile tuna uhaba wa wataalam ambao unasababishwa na uhaba wa ajira na uhaba wa ajira unaosababishwa na uhaba wa wataalum.Swali je ni farasi yupi tukiompanda atakuwa na tija?
 
Kimsingi vinategemeana, lakini jicho la ajira limekuwa kubwa sana.lazima ajira ipewe kipaumbele ili wale wabobezi kwenye ajira (wameshakuwa wataalamu) wawe wengi lakin pia wawaongezee wale wanaoitafuta taaluma.
So tunaunganishaje haya mambo mawili.Kuzalisha wataalam na kuzalisha ajira maana kwa inavoonekana sasa na kwa maelezo yako ni kama vile tuna uhaba wa wataalam ambao unasababishwa na uhaba wa ajira na uhaba wa ajira unaosababishwa na uhaba wa wataalum.Swali je ni farasi yupi tukiompanda atakuwa na tija?
 
Kimsingi vinategemeana, lakini jicho la ajira limekuwa kubwa sana.lazima ajira ipewe kipaumbele ili wale wabobezi kwenye ajira (wameshakuwa wataalamu) wawe wengi lakin pia wawaongezee wale wanaoitafuta taaluma.
Katika mada yangu nimedokea swala la under employment yaani unakuta ofisi imejaa wafanya kazi ambao hawana tija.Kazi ya kufanywa mtu mmoja inafanywa na watu zaidi ya mmoja.je kuna uwezekano kweli wa kuweza kuajiri watu ili wajifunza katika mazingira kama hayo?
 
Katika mada yangu nimedokea swala la under employment yaani unakuta ofisi imejaa wafanya kazi ambao hawana tija.Kazi ya kufanywa mtu mmoja inafanywa na watu zaidi ya mmoja.je kuna uwezekano kweli wa kuweza kuajiri watu ili wajifunza katika mazingira kama hayo?
Hapana, unajua lazima misingi ya kuwapatia watu ajira iweke wazi na mara nyingi watu wanaajiriwa kutokana na uhitaji wa taasisi au kitu husika. ambacho najaribu kukiona ni kwamba endapo mtu amegraduate leo,huyo tunamuita mtaalamu kwa kile alichokisomea lakini anapokuja kwenye vitendo zaidi hapa tunamvua sifa za utaalamu, kwasababu kazi na kile tunachokisomea kuna baadhi ya maeneo vimekuwa vinapishana na uwenda kutokumbua nini kinahitajika.

Leo hii mfanyakazi ambaye amerudi shule(chuo) kujiendeleza anakuwa na utofauti mkubwa sana na mwanafunzi ambaye hakuwai kufanya kazi, kwa maana ya uwelewa wa kile wanachojifunza.

kwa upande wangu kama kungekuwa na kitu cha kwanza kuwezesha katika hayo bsi swala la ajira lingekuwa la kwanza.
 
Hapana, unajua lazima misingi ya kuwapatia watu ajira iweke wazi na mara nyingi watu wanaajiriwa kutokana na uhitaji wa taasisi au kitu husika. ambacho najaribu kukiona ni kwamba endapo mtu amegraduate leo...
Good point,Tukija kwenye swala ajira Je uzalishaji wa hizi ajira utumie mfumo gani?Serikali?Private Sector au namna gani?Maana swala kuanzisha Ajira as it is lina changamoto zake.
 
Tz haina uhaba wa ajira , ila elimu haituandai kujiajiri kwa maana ya kutumia mamia ya fursa ambazo ziko hapa kwetu Tz .. Hata ukitaka kujua tuu angalia jinsi upashanaji hbr chanya unavyodharauliwa au hautumiki ipasavyo na kama taifa hatujawekeza hapa.. Uwekezaji ktk kupashana hbr chanya ndo kitu pekee kitatuvusha kama taifa na kututoa kwenye ombwe la kudhaniwa kuwa tuna uhaba wa ajira kwa vijana . Tukifaulu UPASHANAJI HBR Wenye tija tutatoboza na kungara
 
Mimi ninachojua ni kitu kimoja tu. Tanzania hatuna kitu kinaitwa UHABA WA AJIRA bali tuna UHABA WA UJIRA. Hatuna PESA za kulipa watu MISHAHARA.

Tanzania hii ina watu takribani milioni 60 wafanyakazi wa nchi hii wamezidiwa na watu wakuwahudumia ndio maana hata hakuna ufanisi.

Fikiria tu shule zetu waalimu ni pungufu sana!, na pengine kama 60% ya wahitimu wote wa ualimu wakiajiriwa hata leo hawataweza kuziba pengo ili tufikie standards za uwiano wa mwalimu na idadi ya wanafunzi

Hapo bado hatujachungulia sehemu kama polisi nao ni wachache hatari, hujaingia kwenye afya manesi na wakunga idadi yao ni maajabu ya dunia ndio maana vifo vya wajawazito havitaisha Tz, bado madaktari n.k

Tunao uhitaji mkubwa sana wa wafanyakazi ila tatizo shekeli za kuwalipa hakunaa.
 
Mimi ninachojua ni kitu kimoja tu. Tanzania hatuna kitu kinaitwa UHABA WA AJIRA bali tuna UHABA WA UJIRA. Hatuna PESA za kulipa watu MISHAHARA.

Tanzania hii ina watu takribani milioni 60 wafanyakazi wa nchi hii wamezidiwa na watu wakuwahudumia ndio maana hata hakuna ufanisi.

Fikiria tu shule zetu waalimu ni pungufu sana!, na pengine kama 60% ya wahitimu wote wa ualimu wakiajiriwa hata leo hawataweza kuziba pengo ili tufikie standards za uwiano wa mwalimu na idadi ya wanafunzi

Hapo bado hatujachungulia sehemu kama polisi nao ni wachache hatari, hujaingia kwenye afya manesi na wakunga idadi yao ni maajabu ya dunia ndio maana vifo vya wajawazito havitaisha Tz, bado madaktari n.k

Tunao uhitaji mkubwa sana wa wafanyakazi ila tatizo shekeli za kuwalipa hakunaa.
Mkuu asante kwa nyundo nzuri hii.Nafikiri sasa washiriki wengine wataanza kujua kamba ni ipi na ng;ombe ni ipi ili tumfunge Ng'ombe kamba.Umegusia swala sahihi kabisa. Mkwekwe_mchanja
 
Good point,Tukija kwenye swala ajira Je uzalishaji wa hizi ajira utumie mfumo gani?Serikali?Private Sector au namna gani?Maana swala kuanzisha Ajira as it is lina changamoto zake.
Bado mifumo ya kupata ajira Tz ni changamoto sana, nadhani kutokana na uwekezaji uliopo nchini. kikubwa ambacho nadhani kitakuwa na tija serikali kujenga mifumo kwa wawekezaji kuwa kipaumbele wawe wazawa endapo watakuwa wanaitaji wenye uzoefu.
 
• Mjadala wa elimu usitekwe na wanasiasa, elimu iwe huru na iachwe kwa watu wake, wataalamu. Elimu inayovuma kwa kwa utashi wa siasa, tena za hovyo hauna tija kwa watu wake.

• Tujitafute upya kama Taifa tunahitaji mTanzania wa namna gani katika karne ya 21, falsafa. Tutafasiri changamoto na matatizo tuliyonayo na tuyatufutie jukwaaa lake, elimu inayojibu changamoto na matatizo ya kila simu yanayomkabili mTanzania.

• Dunia inakwenda kwa kasi ya mwanga— sayansi na teknolojia inakuwa na hats mazingira yana badilika na mitindo ya maisha inabadilika; elimu yetu haijabadilika. Tuna watu ambao ni wahafidhina wamekalia jukwaa, wanakaa sehemu ‘wakitunga’ kile ambacho mtanzania anatakiwa asome.

Elimu yetu bado inamabaki ya elimu ukoloni; wakoloni walikuwa wanajua wanataka nini katika elimu yao lakini sisi hatujui tunataka nini. Tunafundisha K.K.K elimu ya awali na mkakati mkubwa ni kuzalisha WAAJIRIWA. Elimu ya sasa ni ya uongo ila waliopewa dhamana hawalioni hilo.

• Tuanze kufundisha elimu inayotamka bayana kwamba: kuna kuajiriwa, kujiajiari na kuajiri. Kwamba mtoto na kijana anaweza kuamua; na sio kuaanza kumpanga na kumprogramisha na ujinga “soma uje upate kazi nzuri” hiyo kauli ni zilipendwa! Elimu ikae mkao huo.

• Elimu inaathiriwa na mambo mengi ikiwemo sheria na kanuni ambazo zinaihujumu elimu yenyewe. Tunafundisha elimu ambayo inato majibu ya zamani katika jamii ya sasa ambayo inachangamoto mpya. Tunajamii ambayo inashindwa kunyumbulika katika mwitikio chanya kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Badala ya jamii kuelimishwa jamii inatungiwa sheria za kudhibitiwa. Ujinga wa karne ya 21 ni zaidi kutojua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu(K.K.K); hayo yalikuwa matatizo ya wazazi wetu na mababu zetu baada ya Uhuru; sisi tunahitaji zaidi -changamoto zimeongezeka.
Kuwa mjinga zama hizi imekuwa kitu rahisi kuliko enzi za wazazi wetu; mambo yamebadilika. Kanuni kwamba shilingi ina pande mbili: ‘kichwa’ na ‘mwenge’ imepitwa na wakati. Tunahitaji elimu inayotambua uwepo wa PANDE TATU ZA SHILINGI: ‘kichwa, ‘mwenge’ na ‘kingo’, kuna mambo zamani hayakupewa uzito ila zama hizi ndo yanayoibeba dunia. Kwa mfano: mdahalishi, simu , hivyo vitu sio anasa tena ni vitu vya msingi, husasani katika elimu. Kwani sheria zetu zenyewe zinasemaje kuhusu hilo?
0759 170 823
• ...
 
So tunaunganishaje haya mambo mawili.Kuzalisha wataalam na kuzalisha ajira maana kwa inavoonekana sasa na kwa maelezo yako ni kama vile tuna uhaba wa wataalam ambao unasababishwa na uhaba wa ajira na uhaba wa ajira unaosababishwa na uhaba wa wataalum.Swali je ni farasi yupi tukiompanda atakuwa na tija?
Je, kuna nafasi gani zinazotafuta wataalamu lakini hawapatikani?

Kwa kawaida tuko kwenye ulimwengu wa fursa. Ikitokea kuna ujuzi unahitajika kwa wingi basi hata watu watapenda kuusoma ujuzi huo ili kujipatia ajira.

Binafsi kwa mtazamo wangu, naona tatizo la Ajira limekuwa kubwa kutokana sababu kuu zifuatazo:

1- Uwezo mdogo wa kiuchumi wa nchi pamoja na vipaumbele.

Mfano: Kuna siku Magu alikuwa anafungua hospitali ya rufaa Mloganzila akasema, mpaka mwaka huo 2017 kulikuwa na upungufu wa watumishi wa Afya Elfu 90 lakini kwa mwaka huo huo serikali ilitoa vibali vya kuajiri watumishi wa Afya 2,000! tu.

Sasa hapa utaona tatizo siyo taaluma waka nafasi za Ajira, tatizo ni uwezo wa nchi kuajiri.

Hali hii ipo pia kwenye sekta ya elimu, polisi n.k

2- Pili, Uanzishwaji wa kozi vyuoni zisizoendana na mahitaji ya nchi.

Kuna mrundikano wa kozi vyuoni ambazo yaani hata wasomaji wenyewe hawajui wakimaliza wanakuwa kina nani?

Tena wakati mwingine mwanafunzi anachaguliwa tu kozi ambayo hata haikuwa chaguo lake.

3- Ni uwezo wa sekta binafsi.
Hapa inategemeana na serikali yenyewe.

Ikitokea serikali inalazimisha kufanya biashara yenyewe then usitegemee kama itatanua wigo wa kodi na ajira kwasababu itahusisha kodi dogo la watu wale wale.
 
Mkuu elimu yetu inatakiwa ijikite kwenye practical zaidi na siyo theory kama sasa, una kuta Eng mzima hawezi hata kupiga rangi banda lake mwenye, pia elimu ya kati ithaminiwe kuliko hizi degree ambazo hazina manufaa yoyote.
Chuoni tunasoma vitu vikubwa mno, ambavyo hapa Tz hatuna uwezo wa kupractice, chuoni tunasoma masuala ya ubunifu wa hali ya juu, practically hapa TZ hatuna viwanda vinarelate na mambo tunayosoma huko vyuoni, mfano wanao soma Electronic, electrical machines na mengine , we are so deep,
Shida kubwa ni kwamba sisi ni 3rd world country

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chuoni tunasoma vitu vikubwa mno, ambavyo hapa Tz hatuna uwezo wa kupractice, chuoni tunasoma masuala ya ubunifu wa hali ya juu, practically hapa TZ hatuna viwanda vinarelate na mambo tunayosoma huko vyuoni, mfano wanao soma Electronic, electrical machines na mengine , we are so deep,
Shida kubwa ni kwamba sisi ni 3rd world country

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unakuwaje Engineer wa majengo huwezi hata kupiga plasta wala kupaka rangi hata jiko lako? mbona madaktari wanasoma vitu vikubwa kuliko nyie na kweli wanatibu? nyie mmebaki kuwa ma-engineer wa BOQ pekee.
 
Mkuu unakuwaje Engineer wa majengo huwezi hata kupiga plasta wala kupaka rangi hata jiko lako? mbona madaktari wanasoma vitu vikubwa kuliko nyie na kweli wanatibu? nyie mmebaki kuwa ma-engineer wa BOQ pekee.
Division of labor lazima iangaliwe ili kila mtu afaidi, Hafu madaktari awasomi vitu vikubwa kuliko engineers ,wao wanakalili tu , ukiona dalili fulani basi anajua kuwa ni Malaria hakuna akili kubwa inayotumika hapo,
Sasa ukija kwa engineers , angalia kuhusu engine, umeme, building, brigdes, even biomedical equipment, electrons , complex structural design, communication ni ubunifu wa wahandisi.
Kwa sisi watanzania tunasoma mambo ambayo yapo deep sana lakini sehemu ya kuenda kuyafanyia kazi hakuna, unafanya calculation ngumu sana kuhusu design , hafu mwisho wa siku mtu anasema huyu ajui ni Bora wa veta, elimu yetu inawaandaa
wahandisi kuwa watatuzi wa matatizo na kurahisisha kazi, unamuajiri engineer ili akapige plaster afu unasema mvivu, mpeleke sehemu sahihi ambayo anaweza kuutilize full potential , hapo ndo useme elimu yetu hamna kitu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom