MJADALA: Kwa Nini Fally Ipupa Anashindana Na Yeye Mwenyewe Na Si Wasanii Wengine?

MJADALA: Kwa Nini Fally Ipupa Anashindana Na Yeye Mwenyewe Na Si Wasanii Wengine?

kaisar19

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2021
Posts
274
Reaction score
488
SmartSelect_20261003-154957_Chrome.jpg

Poleni na majukumu ya kujenga taifa.
Kwa muda sasa nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mwenendo wa kimuziki wa Fally Ipupa "El Maravilloso". Tangu alipotoa "Maria PM"—wimbo uliokuwa hit kubwa sana barani Afrika na duniani kote—na baadaye kuja na mradi mwingine mkubwa wa "Mayday", kumekuwa na mabadiliko ya wazi kwenye mapokezi ya kazi zake mpya.

Fally anatoa nyimbo nyingi nzuri tu, lakini ukizitazama kwa jicho la kiuchambuzi, utagundua anashindana na kivuli chake mwenyewe.
Hapa kuna mambo matatu yanayoeleza hali hii:

1. Kujirudia na Kutoingiza Ladha Mpya
Suala kubwa linaloonekana kwa Fally hivi sasa ni kutobadilisha ladha ya muziki wake.

Baada ya kupata fomula iliyofanya vizuri (mchanganyiko wa Rumba/Sebene la Kongo na vionjo vya Afro-pop), amebaki kwenye eneo hilo hilo la ComfortZone. Pasipo kufanya majaribio ya hatari na producers wapya wenye sound za kileo, nyimbo zake mpya zinaleta mwangwi wa nyimbo zake za zamani.

2. Expectations ya Kazi za Nyuma
Mashabiki na soko hawamlinganishi tena Fally na wasanii wengine wa Afrobeat au Rumba; wanamlinganisha Fally wa sasa na Fally wa "Maria PM", "Eloko Oyo", au "Un Coup".
Kiwango alichoweka huko nyuma kimekuwa kikubwa mno kiasi kwamba wimbo mpya hata ukiwa mzuri kiwango cha kawaida, unaonekana "haujafanya vizuri" kwa sababu haujafikia ule mlipuko wa zamani.

3. Mabadiliko ya Kasi ya Soko la Afrika
Muziki wa Afrika hivi sasa unasukumwa kwa kasi na miondoko mifupi (shorts/TikTok) na ladha zinazobadilika haraka kama Amapiano na Afro-fusion mpya. Rumba na Afro-Congo vinahitaji mbinu mpya kabisa ya utayarishaji ili kuingia kwenye masikio ya kizazi kipya bila kupoteza asili yake.

Maswali kwa Wana-Jukwaa:
Unadhani Fally Ipupa anapaswa kubadilisha nini sasa hivi—mtindo wa uandishi, watayarishaji wa muziki, au kushirikiana na wasanii wa aina gani ili kurudisha ule vuguvugu la mwanzo?

Au unaona ni jambo la kawaida kwa msanii aliyefikia ngazi ya "Legend" kubaki kwenye misingi yake bila kulazimisha kwenda na trends mpya?
Nawasilisha, tupeane mitazamo!
 
Msingi wa muziki wa Congo ni Rhumba, Ndombolo na Soukous. Msanii aongeze ujuzi wake wote, teknolojia yake yote lakini asitoke kwenye msingi huo.
Sasa siku hizi Congo, sijui ndio mabadiriko ya kizazi, unapigwa wimbo ni kama "personally" wa P-SQUARE ila unaaambiwa ni wa flani toka Congo. 😊

Unapigwa muziki mtu unashindwa kujua ni aina gani kati ya Ndombolo, Rhumba au Soukous. Congolese wabaki na mziki wao, kinyume na hapo wasanii wengi watapotea kwenye biashara.

Kuhusu mada; Fally arudie misingi yake ya album iliyomtambulosha kama Solo artist "Droit chemin" au Originale asitoke mle. Associe, Bakandja, Ecole ndio nyimbo ambazo anatakiwa kuziimba.
 
kweli mkuu hilo nalo ni jambo la msingi.
 
Rhumba ina misingi yake akibadilisha kidogo anakua yupo nje ya rhumba,hata nilimsikia christian bella akihojiwa na bbc Swahili,alieleza hilo vizuri,ukisikiliza album yake mpya ya juzi hapa XXX Derilium utaona nyimbo nyingi kama Parable,RDV, crime passionell,mo_perso,choix eternel,homage,zina radha zinazofanana na Associe,Attente,Liputa, science fiction,humanisne nk,Kuna nyimbo alifanya na Mr flavour na diamond akiwemo ile radha ya rumba ilikua huioni kabisa.
 
Fally Ipupa ni wakipee kabisa, hakuna wa kulingana naye kwa sasa,
Wengi wangejua kama Michael Jackson ni mwanamziki mkali kupata kutokea, lakini uwepo wa Fally Ipupa unafanya mtu unajiuliza Mara mbili mbili,
Je , Michael Jackson ni bora kuzidi wote?

Fally anapiga show London, Portugal, France, Ivory Coast, Kenya n.k
Kwangu Mimi huyu ni mwanamziki aliyekamilika zaidi,
Kuhusu kubadilika hawezi kubaki vile vile, maana hata wasikilizaji wa muziki wake wamebadilika
 
Back
Top Bottom