INTRODUCTION
Halooo salama ndugu Wajumbe...
Za weekend.
Hivi unajua ukichunguza kwa makini utagundua Ndoa ni kama Q-NET tuuu..!!!
Yaani ndoa zimezalisha wagonjwa na maskini wengi sanaa.
Wapo waliokuwa wazima ila wameingia kwenye ndoa na kupata visukari na mapresha bila kusahau UKIMWI.
Wapo waliongia kwenye ndoa matajiri ila kwasasa wanapumulia mashine za UMASIKINI....!!
Ndugu zangu ndoa ni Kalynda kabisaa..
SCENARIO.
1. PS wetu wa DED (District Executive Director)
Huyu dada ana mahusiano na muhasibu wetu.
Ila cha ajabu Mwaka huu alitangaza ndoa na mwanaume mwengine..!!!
May/2022 alinipa Kadi ya mchango wa harusi, kundi la WhatsApp likaundwa.
Tukachangia na October harusi ikafungwa.
Wafanyakazi wenzake (pamoja na huyo muhasibu) tukaenda kula ubwabwa washerehe...!!
Mi nakadhani kwa kuwa kashaolewa basi mahusiano na muhasibu yatakufa, ila huwezi amini, alivyomaliza honeymoon akarudi job kaendelea kugongwa na muhasibu.!!!
Ndoa zimejaaa uzinzi mtupu..!!!
2. Dada angu.
Dada angu aliolewa 2017, tokea aolewe sijawahi sikia habari njema kwenye ndoa yake.
Mara Leo kapigwa, Leo ananiomba nimpush kwenye kodi kisa mumewe kasusa, Leo ananipigia analia kisa kamfuma mumewe bar na mwanamke.
Yaani ni full majanga.
Ila in other side dada angu nampenda sanaa, kwanza ni mlokole (huwa akianza kuomba huwa mpaka panya Wana abudu..!!)
Anapiga maombi balaa na hakosi church.
Nikiwa naongea nae utamsikia "ipo siku Mungu atatenda maajabu"
2021 nilivyoona to much sasa, ikabidi nimwambie "Imefika muda sasa unatakiwa kuvunja hiyo ndoa maana Kama kuvumilia vipigo na manyanyaso INATOSHA"
Ila aligoma kumuacha mumewe kisa watoto wake wa4.
Mwaka huu (2022) huwa nikiongea nae anasema "Shemeji yako amebadilika sanaa, anasali siku hizi, kaacha pombe na kawa baba wa familia"
Nikakaa na kujiuliza "Kwahiyo dada kavumilia miaka mi4 ili mtu abadilike..!!""
Yaani kavumilia vipigo, matusi, manyanyaso na Majanga yotee kwa miaka mi4 ili tu mtu abadilike..!!!
Ndoa ni kuuana tu..!!!
3. Kuna pisi najipigia.
Hii pisi inalilia sanaa ndoa.
Juzi bana tumelala simu yake ikawa inaita sanaaa.
Mi usingizi ukapaa, ile simu nikaona kero ikabidi niichukue na kuiweka silent.
Dah pepo la FBI likapanda, si nikaichokonoa bana..!!
Nakuta anachat na mwamba na alimuahidi angeenda kwake siku ile aliyokuja kwangu na mwamba ame-mind anataka kitumbua na demu hajatokea maghetoni kwake..!!
Mi nilisoma chatting zao nikaona hazinihusu Nika screen shot na kujitumia na kuvunga.
Asubuhi akasepa mi nikaenda job kama sijaonaloloteee.
Hapa namsubiri siku tu akomalie ndoa nimlipue kwa kumtumia hizi screen shot "SITAKI ndoa, na hata kama nikioa SIWEZI OA MALAYER"
CONCLUSION.
Hivi ni visa vichache kwenye vingii vinavyoviona huku mtaani.
Wanandoa ni mabatili sanaa mpaka unajiuliza "Kwenye ndoa walifata nini?"
Nikisema niandike visa vyotee nitajaza server za JF buree..
Mabaharia acheni kuoa.
Mabaharia kijiteni kutafuta hela.
Ukiwa na hela utatoa sadaka, zaka, saidia masikini na wenye uhitaji, yaani utaishi maisha ambayo KWENDA MBINGUNI LAZIMA..!!!
Ungekuwa na hela sasa hivi ungekuwa Qatar unapiga selfie na Messi na CR7..!!!
Ukiwa na hela ni full traveling to the adventure..!!!
Ukiwa na hela utakula chochote ukitakacho..!
Yaani kifupi ukiwa na hela YOU WILL BE SOMEONE.
Achana na ndoa tafuta hela.
Yaani unagharamia sherehe na mahari halafu unakuja kugongewa na bwege tu mtaani..
Hizo hela za mahari na sherehe si Bora ungenunua Bond za BOT uone kama zingekusaliti..!!!
Anyway YANGA BINGWA..!!!
#YNWA