MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Umevurugwa

Umevurugwa kama hujui jambo ni vyema ukanyamaza kimya.
 
Ukienda kwenye lugha ya Kiingereza inaeleza kwa uwazi zaidi:

54. And when he was come into his own Country,he taught them in their synagogue.....
55. Is not this the Carpenter's son?is not his mother called Mary?and his brethren James, and Josef, and Simon, and Judas?
56. And his sisters, are they not all with us?....

Walishangaa kwa sababu kwa macho ya kibinadamu hakukuwa na tofauti kati ya familia zao na familia ya Yusufu waliyemtambua kama ndiye Baba yake Yesu.

Kama walivyokuwa wao na watoto wengi wenye tabia tofauti ndivyo familia ya Yusufu ilivyokuwa.Ila walimshangaa mtoto Yesu kapata wapi ufahamu mkubwa hivyo?

Yohana 7:2-5 inatuambia pia juu ya kaka zake Yesu na inaenda mbali zaidi kwa kutuambia pia kuwa sio watu wa Galilaya peke yao bali ata kaka zake Yesu pia hawakumuamini Yesu kuwa ni Kristo.
 
Ahahahahaha hiyo source unayoitumia umelishwa matango pori
 
Mathayo 1:25 inamalizia kwa kusema kuwa Yusufu alilala na Maria baada ya Yesu kuzaliwa.

 
Kwenye kitabu cha ufunuo unayajua yale makanisa saba? Kama Yesu alianzisha kanisa katoliki, Mbona kanisa katoliki halikutajwa kwenye yale makanisa saba? Jibu Hilo swali kwanza?
Wewe hayo makanisa saba umeshawahi kuyaona...??
 
Ahahahahaha hiyo source unayoitumia umelishwa matango pori
Source gani....?

Unachokataa nini hasa..??

Kuwa kitabu cha Mombolezo sio Maombolezo ya Yeremia...??

Soma theology angalau unaweza jibizana na mimi..
 
Yusufu hakufanya ngono na Maria hadi yesu alipozaliwa. baaday ya hapo wakafanya ngono na kuzaa hao ndugu wa yesu niliokutajia.
Jinga kabisa...??

Sasa fuatana na mimi
Maneno kaka na dada ktk utamaduni wa Wayahudi yalimaanisha ndugu yoyote wa karibu..(Rejea Mwa 13:8; 29:11-15), Mtu wa kabila moja (Hes 16:10) Hata Myahudi mwenzie (Kumb 15:12)

Hivyo Kaka na dada wa Yesu wanaotajwa ktk Injili ni wale ambao sisi tungewaita watoto wa Baba mdogo, mkubwa nk nk...

Na pia, kama Maria alikuwa na watoto wengine, kwanini Yesu hakumkabidhi Maria kwa hao na badala yake alimkabidhi kwa mwanafunzi wake(Yn 19:25-27)
 
Source gani....?

Unachokataa nini hasa..??

Kuwa kitabu cha Mombolezo sio Maombolezo ya Yeremia...??

Soma theology angalau unaweza jibizana na mimi..
siyo theology tu nimepiga na escatology
 
Source gani....?

Unachokataa nini hasa..??

Kuwa kitabu cha Mombolezo sio Maombolezo ya Yeremia...??

Soma theology angalau unaweza jibizana na mimi..
siyo theology tu nimepiga na eschatology, kitu ambacho wewe ulivyo shallow katika theology ni ngumu sana wewe kuitolea maelezo,vinginevyo unabaki ktk mafundisho mepesimepesi tu
 
Chimbuko la imani ya Katoliki ni Petro, pale alipoambiwa juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa, fuatilia. Kanisa katoliki lilianzishwa na Yesu
Nafikiri alitaka kumaanisha chimbuko la Dogma hiyo ya kupalizwa mbinguni
 
Huyu Bwana Degratius Nalimi Kisandu ni kichaa....certified lunatic...
 
siyo theology tu nimepiga na eschatology, kitu ambacho wewe ulivyo shallow katika theology ni ngumu sana wewe kuitolea maelezo,vinginevyo unabaki ktk mafundisho mepesimepesi tu
Sasa kweli wewe mbumbumbu wa kiwango cha mwisho...

Mtu aliyesoma Theology nikimwambia kitabu cha Maombolezo na Yeremia ni kitabu kimoja hawezi kukataa..

Ngoja nikuulize unazijua Apocripha books..?
 
Malizia thread make wengi sana ni wagonjwa wa historian ya kanisa
 
Hakuna kitabu kwenye bibilia kimeandikwa maria alipaizwa.na mafundisho ya katoliki yanasema alikufa lakini mwili wake ulipotea kwabla ya maazishi.kwenyebibilia watu wawil tu ndio walio paizwa wakiwa hai ni enoko na eliya tu.
 
Kanisa Katoliki limekuwa likifundisha kwa miaka na miaka kwamba tunaweza kuwaomba watakatifu walioko mbinguni watuombee kwa Mungu. Je, jambo hili lina ukweli kibiblia? Je, hili ni fundisho la Mungu au ni la wanadamu? Je, mtu anayefanya hivyo anampendeza Mungu au anamuudhi?

Hakuna mahali popote katika Biblia ambapo tumeagizwa kuwaomba watakatifu ili watuombee kwa Mungu. Sasa haya mafundisho yanatoka wapi? Unawezaje kuwafundisha watu kitu kisicho kwenye Biblia halafu usiwe na hatia ya kuongeza au kupunguza ujumbe wa Mungu; maana Bwana anasema kuwa atakayeongeza au kupunguza katika neno lake ana hatia. (Ufunuo 22:19).

Iweje basi leo watu wengine wafundishe kuwa Maria mtakatifu mama wa Yesu anaweza kutuombea msamaha kwa mwanawe? Yesu ndiyempatanishi pekee kati yetu na Mungu. Unataka hadi mtu aseme nini ndipo ujue kuwa fundisho hili ni la uongo na hili ni la kweli?

Maandiko pia yanasema: ... basi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. ... yeye, kwa kuwa anakaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee. (Ebr. 7:22-25).

Vipi sasa kuhusu watakatifu walio mbinguni?

Maandiko yanasema wazi: Asionekane kwako ... mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA. (Kumb. 18:10-12).

Je, wafu maana yake nini? Watakatifu walio mbinguni ni sehemu ya wafu au ni sehemu ya walio hai?

Labda utaniambia, “Ah, wafu maana yake ni watu wenye dhambi waliotengwa na Mungu.” Sikatai. Maana hiyo ni sawa. Ni mojawapo ya maana ya kuwa mfu. Lakini, Biblia inasema kuhusu maskini Lazaro: Ikawa yule maskini alikufa... (Lk 16:22).

Je, ‘alikufa’ maana yake si alikuwa mfu? Na tunafahamu kuwa Lazaro alienda mbinguni. Kwa hiyo, kwa sisi tulio duniani, Lazaro ni mfu aliye mbinguni. Ni vivyo hivyo kwa habari ya watakatifu wote ambao hawako duniani leo. Ni wafu! Je, haijaandikwa kwamba: Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. (Ufu. 14:13). Je, ‘wafu wafao’ katika Bwana ni watakatifu au si watakatifu?

Biblia inasema: Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa. (Hosea 4:6). “Wanaangamizwa”, sio “wanaangamia!” Siku ya mwisho hutasema, “Bwana, mimi sikujua.” Ni kweli hukujua, lakini hicho hakitakuwa kigezo cha kusamehewa. Kujua ni sehemu ya wajibu wa kila anayetarajia wokovu wa Bwana. Ni jukumu lake kujua! Ukimtumainia mwanadamu badala ya Neno la Mungu uko kwenye hatari kubwa ya kupotea kutokana na kudanganywa!

Mungu tunayemwabudu anaona yote, anasikia yote, anajua yote, na yuko mahali pote kwa wakati uleule. Sasa, unaponiambia kwamba mtakatifu Petro au Yohana au Maria anaweza kusikia maombi ya watu milioni moja wanaoomba Tanzania; milioni moja Kenya, milioni tano Marekani, nk, na kuweza kuyafanyia kazi; una maana kuwa mtakatifu huyo ni lazima awe na tabia zote hizo hapo juu ambazo ni za Mungu Mwenyezi peke yake!! Je, hilo ni jambo linaloingia akilini?

Acha kudanganywa kwa mafundisho ya uongo! Acha kuangalia wanadamu usoni na kusema, “Huyu kwa elimu aliyo nayo hawezi kunidanganya.” Elimu na cheo si hoja ya msingi. Hoja ni kuwa je, anachosema kinatokana na Neno la Mungu?

Mwisho nakuomba utafakari maneno yafuatayo kutoka kwa Bwana:

Kwa kuwa liko tumaini kwa yule aliyeambatana na wote walio hai (maana ni afadhali mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa); kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lolote lililofanyika chini ya jua. (Mhubiri 9:4-6).

Kazi kwako! Usiuze haki ya mzaliwa wa kwanza kwa ujira wa kunde za mlo mmoja kama alivyofanya Esau!

Tumeitwa kupokea wokovu; si kushikilia dini. Okoka leo. Mkaribishe Yesu awe Bwana na Mwokozi wako. Yesu hakuleta dini bali alileta wokovu.

Biblia inasema: Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. (Warumi 10:9).

Mafundisho mengine ya uongo ni ya watu kusema, “Hakuna kuokoka duniani.” Bwana Yesu alipoenda nyumbani kwa Zakayo, alitamka maneno haya: Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu. (Luka 19:9).

Maandiko pia yanasema: ... wakati uliokubalika nalikusikia, siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama,siku ya wokovu ndiyo sasa. (2 Wakorintho 6:2).

Sasa unaokokaje? Imeandikwa: Kwa maana, kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. (Warumi 10:10).

Tafuta watu wanaokiri wokovu nao watakusaidia. Mungu akubariki na kukufungua macho ya rohoni ili uweze kufanya yale aliyoagiza Bwana wetu Yesu Kristo na si kutumainia maagizo ya wanadamu na wanadini. Ubarikiwe na Bwana.

COPY & PASTE
Source: Yesu Ni Njia: Je, Watakatifu Hutuombea Tulio Duniani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…