KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?
Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.
Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.
Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.
Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua nhistoria vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.
Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.
deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.