kiboksi manyoya
JF-Expert Member
- Nov 16, 2016
- 377
- 311
Imeshiba usanii na utapeli,sielewi uislam umeingiaje hapa.Kanisa Katolik limekuwepo hata kabla ya uislam. Hivyo maktaba ya Vatican imeshiba
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imeshiba usanii na utapeli,sielewi uislam umeingiaje hapa.Kanisa Katolik limekuwepo hata kabla ya uislam. Hivyo maktaba ya Vatican imeshiba
KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?
Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.
Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.
Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.
Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua historia vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.
Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.
deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.
Ndio maana sala zote za kikatoliki mwisho tunamalizia "tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu amen"
Mkuu na wewe umeanza kua mfia dini [emoji3] [emoji3] [emoji3]Kaka unajua kila siku huwa tunawaambia kuwa, wawe wanasoma Biblia na kujaribu kuitafakari kila andiko lina maana gani, pili wanatakiwa kujifunza sana kwa nini wenye Biblia (Wakatoliki) wanafanya hiki au kile na wao hawakifanyi
Shida kubwa ya hawa jamaa ni ya kumfanya Mungu hana uwezo, yaani wanampa Mungu mipaka, wanafanya dhambi kubwa sana kwenye hilo
Musa alikufa na Kuzikwa kabla ya kuingia nchi ya ahadi, lakini pale mlimani Yesu alikuwa na Musa, huyo Musa alitokea wapi? Eliya alipaa kwenda Mbinguni huku Elisha akishuhudia, Pale Mlimani Elia aliyokea wapi? Hao sio watakatifu? Na wale watakatifu wanaofanya maombi (kwenye ufunuo) wanatokea wapi?
Lakini pia, baada ya Saul kufail kila kitu alienda kwa mganga kumuomba ampandishie Samwel, je Samwel alipandishwa?, Alipandishwa kutoka wapi?, je Samwel aliongea mambo ya ukweli au uongo? Kama Mganga aliweza kumtoa Samwel alipo na kuongea nae, iweje watu wa Mungu wasiweze? Hivi kweli watu wa Mungu hatuna Nyoka kama wa Moses atakae weza kumeza nyoka wa Farao?
Ukiona mtu ambaye huwezi kumdanganya kirahisi unamwogopa.Unachagua watu wepesi wa kupotosha.
Hili ni jukwaa huru,ukileta mada mezani inachambuliwa na yeyote.Kama hujiamini kaa kimya kabisa.
Lete hoja sio kirahisi hivyoHuna jipya kajipange urudi tena ukiujua ukweli nayo kweli itakuweka huru kweli kweli.
Historia gani nisiyoijua? Ya Kanisa? Ya kipindi gani? Ancient? Medieval? Au Modern? Ama intertestamental times? Ipi? Kwa kuwa nimenena ya Luther tofauti na mtazamo wako? Nilijibu mwingine kabisa naye hajanijibu bado. Unajua kilichotokea Katika ngazi wakati Luther anapanda kwa magoti kwenda kwa Papa? Unajua andiko la Biblia mbalo lilimjia Luther likamwinua pale na akarudi kwake na usiku huo akapost hoja 95 langoni? Andiko hilo hilo ndilo lililomwongoza hadi wokovu John Wesley akaokoka pale Kanisani Adelsgate akaachana na the Church of England. Unazifahamu hizo hoja 95?Hivi we kiumbe unaijua historia kweli wewe..? Au bwabwaja tu hapa?
Maelezo yana virutubisho vya kila namna .
Sijapanga kukosa muendelezo wa maelezo yako
Wewe si Anglican. Anglican high church hawana tofauti na Catholic Church. Wanasali Rozali na wanapiga ishara ya msalaba. Mtu anayesali High Church hawezi zubaa kwenye misa za Catholic Church sababu vitu vingi vinaendana and vice versa.kha wew jamaa mbona mbishi hata kwa mambo usiyo yajua? Anglikana haitumii biblia sawa ma wakatoliki, anglikana inatumia biblia sawa na wa protestant wenzake, narudia tena am Anglican na ni muumini mzuri wa miaka mingi nimeshiriki semina makomgamano na mafunzo mbali mbali ya kanisa biblia tinayotumia ni sawa na wapentekoste kama hujui kaa kimya, u ar not Anglican halaf wanglikana tunakwambia unabisha, endeleeni kumezeshwa mivifungu iliyotengenezwa na watu
Soma kitabu cha ufunuo. Shida hua mnakaririshwa mstari mmoja bila kujua kuna mstari mwingine unapinga ulichokaririMmechanganyikiwa,ni andiko gani linasema bikra maria alipaa mbinguni?
Leta vifungu acha kukariri yasiyokuwepo ni kifungu gani ktk ufunuo kupalizwa kwa Bikira maria?Soma kitabu cha ufunuo. Shida hua mnakaririshwa mstari mmoja bila kujua kuna mstari mwingine unapinga ulichokariri
Historia ya Biblia ni kuwa ni Kitabu kilichotengenezwa na Kanisa Katoliki na kukamilika mwaka 300 Ad...Ilikamilika ilkiwa na vitabu 72/73 ila baadae Martni Luther aliondoa vitabu 7 na kubakiwa na vitabu 66.,
Hakuishia hapo, aliondoa vitabu 3 vya Agano jipya....Biblia ya Martin Luther ilikuwa na vitabu 39 vya Agano La Kale na Vitabu 24 vya Agano jipya..
Reformer mwenzake Calvin ndiye aliyemsihi kuvirudisha vitabu 3 ya Agano jipya..