MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

sinodi ya africa 1990 iliyoandikwa na Karol Luangwa akisaidiana na eusebius
Hiyo Sinod inahusiano gani na Martin Luther kupunguza vitabu...???

Kabla martin luther hajapunguza, biblia hiyo unayosema ilikuwa inasomwa na watu wa chache ilikuwa na jumla ya vitabu vingapi..?
 
Ndio maana sala zote za kikatoliki mwisho tunamalizia "tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu amen"
unafikiri wote wanaoapa kwa kusema haki ya Mungu wana sema ukweli siku zote,vivyohivyo kumalizia maombi na jina la Yesu siyo uhalali wa maombi yako kukubalika mbele za Mungu,bali ni sawa na kulipaka tu kaburi kwa nje ndani ni mifupa
 
Sasa hoja yako ipo wapi hapa??
 
Hiyo Sinod inahusiano gani na Martin Luther kupunguza vitabu...???

Kabla martin luther hajapunguza, biblia hiyo unayosema ilikuwa inasomwa na watu wa chache ilikuwa na jumla ya vitabu vingapi..?
66
 
Otorong'ong'o,
Duh wew jamaa mbishi kweli, hivi tangu lini Anglikana wakasali rozali, niko na comment hapa na litrugia ya kanisa ninayo hapa mezani hakuna kitu kinachitwa rozali wew acha uongo na nimekwambka mimi nasali high church hakuna kitu kinachoitwa rozali kwenye anglikana acha kupotosha wew... biblia tunayotumia ni hii hii wanyotumia wakristo wengine wa kipentekoste ma ndiyo maana ukipitia reference ya litugia ya kanisa na kalenda ya mwaka huwez kukuta kutab eti cha paulo na sila.. Na comment hapa nikiwa na bible, Litrugia na kalenda ya kanisa ya mwaka.. acha uongo wewe kama hauijui anglikana kaa kimya usipotoshe
 
KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?
deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.

Ikiwa mnapenda kujadili kwa kina mambo ya ndani ya Biblia nendeni mkasome Katika vyuo vya Biblia ndipo mtaandika habari za usahihi. Luther alitafsiri Biblia sio kwa kibiashara bali alihoji kwa nini Neno la Mungu libakie katika lugha wasioielewa watu wengi? Aliwapa Wajerumani Biblia katika lugha Yao. Hakupunguza kitu kutoka Hebrew Old Testament na Greek New Testament alivyotumia Kama Source Text.

Sana aliongeza vitabu vya Apokrifa vile 6 vilivyokuwemo katika Latin Vulgate. Unaposema deutero-canonical unaelewa una maana gani? Unasema kusoma Historia ya Kanisa? Sema soma Biblical Studies, sema soma Historical Criticism ya vitabu vya Biblia, sema soma Textual Criticism ya hayo Maandiko. Sema soma Canonical texts za Biblia. Hapo ndipo utaelewa mengi kuhusu Maandiko ya Biblia. Luther si mfanya biashara.

Luther ni msomi aliyebobea katika Theolojia na kuona mapungufu na makengeufu ya Kanisa na kudiriki kusema. Luther aligundua kuwa wokovu ni kwa Imani na si kwa matendo ya kidini ama kazi za mtu. Unasema nini juu ya Luther Mwana mageuzi mkubwa alienusuru Imani sahihi ya kanisa kwa enzi hizo. Acha kabisa!!!!
 
Hahahahahahaha......

Hebu nenda kule jukwaa la celebrity na jokes bana ..

Biblia imekamiliks mwaka 300Ad....ikiwa na jumla ya vitabu 72/73... Sasa hiyo ya vitabu 66 imetokea wapi..?

Hivi unajielewa kweli wewe..?
 
Leta hoja sio vioja mama maria she is nobody on this world "mama tuna mini Mimi nawe" alisema yesu karamuni
Kiongozi kaa sawa kusoma bible. That lady was trusted by God to handle Jesus. To me she is some one. Why not other women? About her praying for us... That's debatable.

Have a wonderful year.
 
Luther alitafsiri Biblia sio kwa kibiashara bali alihoji kwa nini Neno la Mungu libakie katika lugha wasioielewa watu wengi
Hoja siyo kufasiri kutoka Kilatini kwenda kijerumani, hoja ni kwanini alipunguza vitabu 7 vya Agano la kale...??

Kwanini Complete biblia ya Martin Luther, kabla calvin hajamshauri ilikuwa na vitabu pungufu vya Agano jipya....Yani, kwann aliondoa kitabu cha Yakobo, ufunuo na Waebrania..?
 
Hahahahahahaha......

Hebu nenda kule jukwaa la celebrity na jokes bana ..

Biblia imekamiliks mwaka 300Ad....ikiwa na jumla ya vitabu 72/73... Sasa hiyo ya vitabu 66 imetokea wapi..?

Hivi unajielewa kweli wewe..?
wewe ndo hujitambui naona hujui mambo vizuri eti 72/73....... kesho utakuja hapa tena na hoja dhaifu zaidi ya hizi kutuaminisha bibilia inavitabu 80
 
wewe ndo hujitambui naona hujui mambo vizuri eti 72/73....... kesho utakuja hapa tena na hoja dhaifu zaidi ya hizi kutuaminisha bibilia inavitabu 80
Toka mwanzo hata mwisho wa dunia biblia itabaki kuwa na vitabu 72/73..,

Ndugu ninapoandika 72/73 na maana hii..

Kitabu cha Maombolezo kiuhalisia ni kitabu cha Yeremia...Huwa kinaitwa Maombolezo ya Yeremia...

Sasa Biblia zingine huwa zinaweka kama kitabu Kimoja yani ' Yeremia na maombolezo ya Yeremia"

Biblia zingine (nyingi) hutengenisha na kufanya kuwa vitabu viwili yani Maombolezo na Yeremia...(Ila kimsingi ni kitabu kimoja)
Ndio maana huwa naandika 72/73..., usiogope..Najua ulikuwa hujui nasasa nimekujuza
 
Nimejaribu kuconnect hoja yako na niliyoyaandika sijapata connection.... Hebu isome tena mkuu halafu ucomment bila kutumia lugha kali bro. Well, kama hujawahi kutenda dhambi ya uasherati au uzinzi, hongera sana mkuu!!! Nadhani moyo wako utasema zaidi ya vidole vyako!!!
Hujaelewa nini kasome Biblia msituchoshe
 
Hoja siyo kufasiri kutoka Kilatini kwenda kijerumani, hoja ni kwanini alipunguza vitabu 7 vya Agano la kale...??

Kwanini Complete biblia ya Martin Luther, kabla calvin hajamshauri ilikuwa na vitabu pungufu vya Agano jipya....Yani, kwann aliondoa kitabu cha Yakobo, ufunuo na Waebrania..?

Umeisoma Guttenberg Bible ukakuta vitabu hivyo havipo?
 
Deogratius Kisandu,

Heshima kwako mkuu,

Huwa najiuliza hivi mtu ukitulia na Imani yako unapungukiwa na nini? kuna ulazima gani kuchokonoa Imani za watu wengine ? Kama wewe unaamini huko ulipo ndio sahihi si utulie hukohuko? Tukumbuke wengi wetu hizi Imani hatukuzichagua, tunaabudu pale wazazi wetu wanapoabudu, tujifunze kuheshimu Imani za wengine hata kama tunafikiri wanapotoka.
 
Hoja siyo kufasiri kutoka Kilatini kwenda kijerumani, hoja ni kwanini alipunguza vitabu 7 vya Agano la kale...??

Kwanini Complete biblia ya Martin Luther, kabla calvin hajamshauri ilikuwa na vitabu pungufu vya Agano jipya....Yani, kwann aliondoa kitabu cha Yakobo, ufunuo na Waebrania..?

Unapozungumzia vitabu hivyo unazungumzia NT Canon ambayo ilikamilika kwa series na halikuwa Suala la Luther kwanini Mark na Hebrews vilichelewa kukubalika na Kanisa. Hata Job ilichukua muda kukubalika. Umerudi Kwangu tena wewe na nilikuwa sikujibu wewe hata kidogo, umedakia tu. Sipendagi mijadala na wewe. Approach yako ya arguing siipendi kabisa.
 
Back
Top Bottom