MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Hivi unatambua kuwa Papa Yohana Paulo II aliomba radhi kwa wayahudi na watu wote walioteswa na kuuawa na kanisa katoliki? ikiwa kanisa katoliki ndilo lililopigwa mawe ilikuwaje papa aombe radhi kutokana na kanisa hilohilo kumwaga damu isiyo na hatia?
Ukiwa unauliza utajifunza. Iko hivi. Kuna kipindi kanisa liliwahi kupitia kipindi kigumu Sana. Kwani siasa ilichanganyika na Dini.Viongozi wa dini ilifikia wakati wanapewa nyadhifa za kisiasa na hata wanasiasa wanapewa baadhi ya nyadhifa kwenye dini. Sasa ilikuja kufikia kipindi wanasiasa wakawa wana influence maamuzi kwenye dini. Ndipo viongozi wakaona ni lazima kutenganisha haya mambo. Mf. Mfalme Henry alitaka kuongeza mke wa pili hivyo akataka Kanisa liidhinishe, Kanisa lilikataa. Ndo maana ukisema Kanisa liliwahi kufanya uovu ni kweli kwasababu wakati Huo hata baadhi ya viongozi wa kisiasa walitumia nguvu walizopewa katika dini kuhalalisha baadhi ya uovu wao.
 
Sawa hapo tuko pamoja, na kwa kuwa kanisa lilichanganyika na dola ambayo hapo awali walikuwa hawaupendi ukristo, viongozi haohao wa kisiasa walifanya hila ya kuleta mafundisho potofu kanisani. Ukweli huu unapaswa usemwe wazi na ndio maana kuliibuka vuguvugu kubwa la wanamatengenezo kupinga upotoshaji wa wazi wa Biblia.
 
Ndio maana Kanisa katoliki linabaki kuwa imara kwasababu liliisha pitia majaribu mengi na likarekebisha Makosa.
 
Ndio maana Kanisa katoliki linabaki kuwa imara kwasababu liliisha pitia majaribu mengi na likarekebisha Makosa.
Hitimisho lako linaashilia kuwa kanisa katoliki sio kazi ya Mungu. Ni kazi ya binadamu. Kwa sababu kazi ya Mungu haina makosa wala majaribu. Na hakuna kurekebisha.

Na kwa mtaji huu hata makanisa au dini nyingine, zitapitia majaribu na baadaye kujirekebisha na kuwa imara.
 
Huwezi ukasema Kanisa Katoliki sio mpango wa Mungu....!Kanisa Katoliki ni mpango wa Mungu kupitia mwanadamu na kushibitisha hilo lingekuwa sio mpango wa Mungu lingeshafutika.
 

Comment of the century...no one can top this....

Thanks for this wisdom brother!
 
Kwani Kanisa linaabudu sanamu...!sanamu ni ishara/kielelezo kuwakumbusha kwamba bwana watu Yesu Kristo aliwambwa msalabani yani ni kama kumbukumbu flani,hata kama imewekwa kanisani sio kwamba inaabudiwa hapana anayeabudiwa pale ni Mungu kwa njia ya msalaba wa mwanae Yesu Kristo kwani ule ndio ulikuwa ukombozi wa mwanadamu,cjui kama utanielewa kwa MTU mwenye mafundisho ya kisabato ni pagumu sana.
 
Kwenye hiyo amri kuna makatazo ya aina mbili:.
1.usijifanyie sanamu ya kuchonga mfano wa kitu chochote,juu mbinguni,duniani,ndani ya maji wala chini ya ardhi.
2.usifisujudie wala kuvitumikia.

Hapo msitafute kuhalalisha sanamu kanisani zimekatazwa. Ndio maana kwenye katekismo yenu amri inayokataza ibada ya sanamu mmeindoa na mkaigawanya amri ya kumi inayozungumzia kutokutamani mke wa mtu wala mali yake, Ninyi katika amri moja mmetoa amri 2 ili kufidia amri ya pili mliyoiondoa.Mbona hili liko wazi?linganisha amri kumi za Mungu katika Biblia Kutoka 20 na zile za kiroma kwenye katekismo yao.
 
Duh! kweli walimu wako walikuwa na kazi...sasa unakataa nini na unakubali nini? Neno la Mungu liko wazi, ibada ya sanamu yaani kutengeneza sanamu ya kitu chochote hata ukipe jina gani zuri
Kutengeneza ni kitu kimoja na kuabudu ni kitu kingine...

, hiyo ni ibada ya sanamu na imekatazwa
Kwani ibada ni nini...??

period. Na hapa Mungu alikuwa hawambii waebrania peke yao, bali maelfu na maelfu wampendao Mungu. Neno la Mungu halina ukomo wa muda.
Maelfu na maelfu ni wakina nani...? Hiyo amri ni kwa Waebrania...Unaishika wewe ni muebrania kwani...?
 
Hivi unatambua kuwa Papa Yohana Paulo II aliomba radhi kwa wayahudi na watu wote walioteswa na kuuawa na kanisa katoliki? ikiwa kanisa katoliki ndilo lililopigwa mawe ilikuwaje papa aombe radhi kutokana na kanisa hilohilo kumwaga damu isiyo na hatia?
Ellen G White alushaomba msamaha kwa mauaji aliyofanya...?
 
Kwenye hiyo amri kuna makatazo ya aina mbili:.
1.usijifanyie sanamu ya kuchonga mfano wa kitu chochote,juu mbinguni,duniani,ndani ya maji wala chini ya ardhi.
Niambie hiyo picha (back Ground pic ) Wakati Rais wa Kanisa la SDA amekuja Tz hapo ni uwanja wa Taifa ni picha ya nani....?

.usifisujudie wala kuvitumikia.

Niambie hiyo picha inafanya nini hapo...

Kitaja nataka jibu....
 
Kwa hio biblia yenu mtu akiamua kupunguza mistari anapunguza, tu bila ya hofu
Akiamua kuongeZA mistari anaongeza, tu bila hofu
Hizi dini zingine bwana

Lakini wacha, tuachie wenyewe tuone watakavyo shambulia mtoa mada, badala ya kujibu ada hisika
biblia yenu maana yake nini?
 
Huwezi ukasema Kanisa Katoliki sio mpango wa Mungu....!Kanisa Katoliki ni mpango wa Mungu kupitia mwanadamu na kushibitisha hilo lingekuwa sio mpango wa Mungu lingeshafutika.
Shule ukiisoma vizuri kitu kitamu sana. Nimetumia implication kimuonyesha cheichei kuwa ukisema kanisa lilijirekebisha kuondoa makosa unaondoa kazi ya Mungu na kazi ya binadamu. Huwezi kuwa divine na baadaye unaanza kufanya mabadiliko hili uende na wakati.

Na huu ndio mchango mkubwa wa Luther kwa wakatoliki. Vitu vingi vya Luther ambavyo vilipingwa, wakatoliki wamevikubali baadaye. Sasa hapo nani kaleta mabadiliko? Luther au Roho Mtakatifu?

Kudumu kwa Kanisa Katoliki sio hoja oriental churches nazo zimedumu kwa muda mrefu. Hindu nayo umedumu kwa muda mrefu. Huku Africa wengine bado tunaabudu mizimu toka dunia imeanza. Hivyo kudumu haimaanishi unafanya kitu sahihi.
 
oriental churches nazo zimedumu kwa muda mrefu.

Oriental churches most of them zina-bolong kwenye Eastern Orthodox Churches...

Sasa Eastern Churches (Orthodox) walijitenga na Kanisa Katoliki karne ya 11...
 
Martin Luther ni padre pekee aliyepewa maona ya kulikomboa kanisa na alioneshwa uhalisia wa kanisa linavyoasi. Soma vitabu vingi vya historia ya kanisa utamjua vizuri. Kuwa padre huyu alipewa kipawa cha ajabu
 
Martin Luther ni padre pekee aliyepewa maona ya kulikomboa kanisa na alioneshwa uhalisia wa kanisa linavyoasi.
Kulikomboa kanisa gani...? Lutheran Church limebaki Africa tuu....Ujerumani ni kama limekufa tayari, Sweden watu hata hajui kanisa nini..


Hayo maono, ndiyo yalipelekea yeye kupunguza vitabu 7 vya Agano la kale..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…