Hadithi za kutunga kivipi...? Nani katunga..? Historia inatungwa...???
Nani anaabudu sanamu...? Unajua maana ya kuabudu...?
Lingekuwa na manufaa kama umgejibu au kunipa ufafunuzi wa yale niliyokuuliza..
Umebaki unarukaruka kama kuku mwenye kideri...Utatu Mtakatifu hujanipa jibu, picha hujanipa jibu...
Nikikuuliza hiki unarukia hiki...hopeless
Sitatochoka kukupa Theology halisi iliyojikita katika Biblia Takatifu, sio ile uliyokaririshwa tangu utoto kutoka kanisa lilioasi. Umekuwa na uelewa finyu wa Waadvesntista wasabato, na umekaririshwa uongo mwingi kiasi cha kuamini propaganda kuwa wasabato hawaamini kuwa Yesu ni Mungu na pia umedai hawaamini kuwa Roho Mtakatifu ni Mungu.Hizo ni propaganda chafy dhidi ya kanisa la Mungu, jiepushe nazo hiyo ni kazi ya mwovu ibilisi kwani yeye ni muongo tangu mwanzo.
Baada ya utangulizi huo nakuletea baadhi ya misisngi ya waadventista wasabato ili kuthibityisha kuwa kanisa hili linaegemea mafundisho yake kwa muujibu wa Biblia wala sio nje ya Hapo.
1.
Maandiliko Matakatifu
Maandiko Matakatifu, yaani Agano la kale na Jipya ndiyo Neno la Mungu lililoandikwa,
likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia kwa watu watakatifu walionena na kuandika kama
walivyoagizwa na Roho Mtakatifu. Ndani ya neno hili, Mungu amemkabidhi mwanadamu
maarifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu. Maandiko matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa
wa mapenzi yake. Ndiyo upeo wa tabia, kipimo cha uzoefu, ufunuo thabiti wenye mamlaka
wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu aminifu ya matendo ya Mungu katika historia.
(2Petro 1:20,21. 2Timotheo 3:16,17. Zaburi 119: 105. Mithal 30: 5,6. Isaya 8:20. Yoh
17:17. 1Wathe 2:13. Waeb4:12.)
2.Utatu Mtakatifu
Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, umoja wa nafsi tatu za milele.
Mungu hapatikani na mauti, mwenye nguvu zote, ajuaye yote, zaidi ya yote, na aliyeko
daima. Yeye hana mwisho na ni zaidi ya ufahamu wa kibinadamu, hata hivyo anafahamika
kupitia kujifunua kwake binafsi. Milele zote yu astahili kuabudiwa, kusujudiwa, kutumikiwa
na viumbe vyote. (kumb 6:4. Mith 28:19. 2kor 13:14. Waef 4:4-6. 1Petr 1:2 1Tim 1:17
Ufunuo 14:7)
3.Baba
Mungu Baba wa milele ndiye muumbaji, Chimbuko, Mtengenezaji, na Mfalme wa viumbe
wote. Ni mwenye haki na Mtakatifu, Mwingi wa rehema,, mwenye fadhili, si mwepesi wa
hasira, na mwingi wa uthabiti wa upendo na uaminifu. Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa
ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni ufunuo wa Baba. (Mwanzo 1:1 Ufu 4:11.
1wakor 15:28. Yoh 3:16. 1Yoh 4:8. 1Tim 1:17. Kut 34:6,7. Yoh 14:9).
4.Mwana
Mungu Mwana wa milele alifanya mwili katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote
viliumbwa, tabia ya mungu imefunuliwa, wokovu wa wanadamu unakaribishwa na
ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu
aliye kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira
Mariamu. Akaishi na kupitia uzoefu majaribu kama mwanadamu, lakini kwa ukamilifu
alioonyesha kwa mfano wa haki na upendo wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha
uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama Masihi aliyeahidiwa. Aliteseka na kufa kwa hiari
msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kama mbadala wetu, Alifufuliwa kutoka kwa wafu,
na akapaa kuhudumu katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika
utukufukwa ajili ya ukombozi wa mwisho wa watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote. (Yoh 1: 1-3,14. Wakol 1: 15-19,. Wafil 2:5-11. Yoh 10:30, 14:9 Warum 6:23. 2Wakor 5:17-19.
Yoh 5:22. 1Wakor 15:3,4. Luka 1:35. Yoh 14:1-3)
5.Roho Mtakatifu
Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji,
kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa mabadiliko matakatifu.
Alijaza maisha ya kristo na uwezo. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu, na wale
wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba
na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa,
huliwezesha kumshuhudia kristo, na kwa upatano wa maandiko huliongoza kwenye ukweli
wote. (Mwa 1,2. Luka 1:35, 4:18. Mdo 10:38. 2Petr 1:21. 2Wakor 3:18. Yoh 14:16-18,26,
15:26,27, 16:7-13)
Hii ni baadhi ya misingi mikuu ya imani ya Waadvenstista Wasabato, kama una swali zaidi kuhusu mismamo wa Waadvenstista Wasabato kuhusu Utatu Mtakatifu, niulize sitachoka kukuelimisha kwa kutumia Maadikiko Matakatifu "sola scriptura" wala sio hadithi za kutunga.