MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Limesema Kanisa Katoliki na Ndo lenye mamlka hayo na Ndo maana Biblia Ilitoka Huko... Kwani Yesu aliagiza Mjenge Makanisa? Ni wapi pameandikwa Mjenge kanisa.. yeye si Alikuwa anaabudu Yerusalem
Ngoja nikuache maana umeamua kujitoa ufahamu
 
Acha maneno lete maandiko
 
Embu niambie mstari ndani ya biblia ulioandikwa hivyo Hata meno katoliki tusiongeze neno wala kupunguza leta mstari.
Biblia Si kila Kitu Kwahy Si Biblia Pekee yenye Majibu... Mengine utayapata Kanisani na Ni kanisa Katoliki pekee nyie Wengine Hamna Hilo.. maana Roho Wenu ni Mfu.. Ameshaacha Kuwafunulia mmebakia na Biblia tu ,mambo mapya hamna.. mkaamua mkatoa na Vitabu vingine....

Fuata Historia ya Kanisa Lako halina Tofauti na Gwajima na Rwakatale yote yameanzishwa na Watu badala ya Kristo Mwenyewe..
 
Unajua maana ya neno Catholic?...
We unajua..?? Kwanini unahisi sijui....Haya ngoja nikuekeze
Catholic ni neno la Kigiriki (Katolikos)linalomaanisha -eny, -iliyo enea....Universal....Ukisoma Biblia ya kigiriki pale Yesu anawambia wafuasi wake enendeni ulimmwenguni "kote".... Hapo kwenye "Kote" utapata inaandikwa " Katolikos".... Na neno hilo ndio likatoolewa jina la Kanisa na kuanza kuitwa rasmi Catholic Church ......

Kama ulikua hujui
Aliyekuambia sijui ni nani...??

anglikana nao wanaitwa Anglican Catholic
Anglican hawaitwi Anglucan Catholic... Ila Watu hupenda kuwapachika au kujipachika Anglo-Catholic, na hii ni kutokana Liturujia ya Anglican haina tofauti na ya Catholic...mfanano huo ndio ukawafanya waanglikana wajione kama Wakatoliki....

, Orthodox Catholic
Hakuna kina kinaitwa Orthodox Catholic....
, na ndiyo maana hakuna dhehebu linaloitwa Catholic
Catholic siyo dhehebu ni Kanisa Kamili...
ila lipo Roman Catholic..
Hakuna kitu kinaitwa Roman Catholic ila kuna Catholic Church

nenda kasome maana ya Catholic
Nimeshakueleza hapo juu....

Nafikiri wewe ndio unapaswa kusoma...
 
Lakini Wa kristo ambao siyo wakatoliki kuna swala mnanitatiza sana ivi kwanini mnakua wazito kuutambua mchango Wa mama maria katika ukombozi Wa dunia hii, ivi unawezaje kuumwabudu mwana na ukaacha kumweshimu mama , kuusu mama maria nadhani niwakati Wa maadhehebu mengine ya kikristo kujitazama na kuumpa nafasi katika maisha yao, sikia nikwambie karne zilizo pita mwana mmke alidharauliwa sana na nadhani ndiyo sababu ya madhehebu mengi kutokumpa huyu mama nafasi katika makanisa yao
 
ichumu lya,
Wayahudi wa hawakivichukua kutokana na mapokeo yake yalikuwa kwa lugha ya Kigiriki...Wao walikuwa wanataka vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya kiebrania pekee...

Na hivi vitabu viliandika na Wayahudi walioishi Misri....

Pia hujatueleza ni kwanini Luther alipunguza vitabu vya Yakobo, Waebrania na Ufunuo wa Yohana ..
 
kumbe hata maana ya wa protestant hujui....

Hata Anglican nae ni m protestant halaf Biblia na idadi ya vitabu wanaliyo nayo wa anglikana na hiyo hiyo ya wa Pentecoste na Assembles
Kakudanganya nani.. ?? Anglican high Church/Episcopal Church hayanatofauti na Catholic Church hata mafundisho yao..Ndio maana sometimes huwa wanapenda jiita Anglo-catholic...Na biblia yao inavitabu 73/72
 

Sitakujibu hili, ili nisiharibu mada...
 
Dhambi inawatafuna,
 

Asante kaka, ntachangia na mimi nikikaa vizuri, lakini cha muhimu hapo ni kuwa wakati hilo la Martin Luther la kukengeuka na kuangaika na vitabu vya Biblia, kulikua hakuna Dini ya Bi Helen, wala hawa "wapakwa" mafuta, Biblia ilikuwa chini ya himaya ya Wakatoliki na walikuwa wanailinda, na hata Luther alipotoa vitabu alivyovitoa, Biblia halisi bado iko Mikononi mwa Wakatoliki
 
Any way acha nendelee ku stick kwenye swali langu la msingi,,,, katika biblia ni wapi tumeambiwa maombi yetu yapitie kwa Bikra Maria?
B/Maria ni Mtakatifu hivyo....
Sio Bikira Maria Pekee, Watakatifu wote jukumu lao ni kutuombea....Soma Ufunuo 5:8 uone Wazee 24 , wakizunguka kiti cha Mwana Kondo(Yesu) wanafanya nini..?

Ngoja nikuandikie
Ufunuo 5:8
Hata alipokitwa kile kitabu, hao wenye uhai 4 na wazee 24, walianguka mbele za mwana kondoo, kila mmoja na kinubi na vitasa vya dhabu vilivyojaa manukato, ambayo ni MAOMBI YA WATAKATIFU


Hivyo ni wazi, watakatifu kazi yao ni kutuombea...Sasa sijui utapingana na hapo pia...
 
Kakudanganya nani.. ?? Anglican high Church/Episcopal Church hayanatofauti na Catholic Church hata mafundisho yao..Ndio maana sometimes huwa wanapenda jiita Anglo-xatholic...Na biblia yao inavitabu 73/72
Acha uongo wew am Anglican na nimezaliwa na kubatizwa low church na sasa ninasali high church hiyo biblia unayoisema wew haipo
 
kwa hiyo kumbe katoliki ni dini dola huko italia na spain pia anglikan ni dini dola kule uingereza
 
Acha uongo wew am Anglican na nimezaliwa na kubatizwa low church na sasa ninasali high church hiyo biblia unayoisema wew haipo
High Church ndugu halina tifauti na Catholic Church...Na Rozari kule tunasali vizuri....

Low Church walitaka kujifananisha na Lutherans hivyo waka-copy kila kitu kutoka Lutheran

Kama kweli wewe ni Anglican High Church nenda pale Cathedral ya St. Alban posta DSM, then angalia mandhari ya ndani ya Kanisa, kisha Nenda St. Joseph Cathedral posta ungalie uone kama utaona tofauti ....Hakuna tofauti
 
Yesu ni Mungu sawa na Baba na Roho Mtakatifu...Mungu anatuombeaje sasa....??

Kuwa makini, ndio maana Waislam wanawasumbua kuwa Yesu si Mungu....
Mtu hawez kwenda kwa baba ila kwa njia yangu.. Yesu anejiweka kuwa mtu wa kwanza kumuona kabla ya kufika kwa baba ni kama receptionist.. Sio koss kumuomba Mungu moja kwa moja,

habari za kumtaka mtu akuombee zilikua enzi hizo ambapo makuhani hiyo ndiyo ilikua kazi yao kwamba mtu wa kawaida alikua hana uwezo wa kupiga magoti na kumuomba Mungu isipokua alipaswa kupeleka sadaka yake kwa kuhani na mahitaji yake kuhani ndio anamuombea, lakiniujio wa Yesu ulivunja vifungo vyote na ndio maana anasema Ombeni nanyi mtapewa halaf anasema ni nani ambae anaweza kumpa nyoka mwanae amuombae samaki.

maana yake ni kuwa sisi ni watoto yeye ni baba haina haja ya kupita pita sijui kwa maria au kwa nani, pray direct yupo aliyepewa jukumu la kutusaidia kuomba ambae ni Roho mtakatifu huyu hutusaidia kuomba maana peke yetu hatuwez kuomba ipasavyo....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…