Pole sana mkuu....,hawa jamaa umejitahidi sana kuwaelewesha lkn wanjitia manunda.....!ila natumaini wameelewa tatizo ni ununda wao
Hv huyu Kitaja ebu atuambie William Miller alitumia kifungu gani ktk biblia takatifu kutabiri mwisho wa dunia 1844.......?alafu tumpe maudhui ya hivyo vifungu alivyovitoa....!
Tafsiri zile za upotoshaji za 1844 za bwana Miller ndizo hizi anatuletea leo mjukuu wake bwana Kitaja,nimemuomba bwana Kitaja ebu nipe andiko alilotumia Miller kutabiri mwisho wa dunia na kama hajui aseme........?kukwepa swali sio ishu....
William Miller, aliyekuwa Mhubiri mashuhuri wa Kibaptisti alisoma katika kitabu cha Danil 8:13. "Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?
Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa." Daniel akiwa katika maono aliona yule asi akikanyaga mahala patakatifu na kuiangusha kweli kwa kuleta mafundisho yaliyo kinyume na Neno la mungu, na kisha kutesa watakatifu. Jambo hili lilimsononesha sana Daniel. Ndipo Malaika akampa ufafanuzi kwamba jambo hili lina mwisho wake. "Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri. Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga. Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa". Daniel 8:9-12.
Hii Pembe ndogo haina tofauti na pembe ndogo ya Daniel 7:19-27. " Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;
20. na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake. 21.
Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; 22 hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.
23. Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. 24. Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu. 25. Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
26. Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.
27. Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.
Kwa ulinganifu huu utajua wazi kuwa utawala wa nne unaosemwa hapa ni Rumi. Huu n Uatwala wa nne kuitawala dunia yote kuanzia Babeli, Wamedi na Waajemi, Wayunani na Kisha Warumi. Utawala wa kirumi ndio ambao hata Bwana Yesu aliukuta, hakujakuwa na mamlaka yeyote iliyotawala dunia baada ya Rumi. Baadae utawala huu uligawanyika katika mataifa kumi yanayounda Ulaya leo lakini ( pembe tatu kati ya hizo) yaani mataifa matatu yaliangamizwa na Utawala wa Papa baada ya kukataa kumtii hayo mataifa ni Ostrogoths, Vandals na Heruri. Hayapo kabisa " They were terminated by Roman Catholic Pope".
Sasa nirudi katika unabii wa Daniel 8:14. Siku 2300 zinazosemwa hapa huwakilisha miaka 2300. Miller na wenzie walijifunza unabii huu na kugundua kuwa Biblia husema kipindi kile wana israel walipoanza kujenga upya Hekalu la Yerusalemu ndipo unabii huu huanza na kipindi hiki kinaishia mwaka 1844. Biblia inasema baada ya miaka 2300 ndipo patakatifu patatakaswa. Na kwa wana wa Israel kutakaswa kwa patakatifu ilimaanisha hukumu,na kujitesa nafsi zao na kufanya upatnisho wa dhambi zao. Tazama Mambo ya Walawi 16:29, 30; 23:27-29. "Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za Bwana....Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. Nanyi msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Bwana, Mungu wenu. Kwa kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake".
Mwisho wa huduma hii ya patakatifu, dhambi ama zilisamehewa au kukataliwa kutokana na jinsi mdambi alivyojiwasilisha mbele za Mungu kwa sadaka za kuteketezwa. Kwa kuagalia muktadha huu, Miller na wenzie waliamini kuwa mwisho wa mika 2300 yaani mwaka 1844, Patakatifu patatakaswa yaani dunia hii iliyochafuliwa na utawala wa kirumi ingetakaswa. Kwa maana nyingine waliamini kuwa Yesu anakuja kutakasa dunia kipindi hiki. Tafsiri yao ilikuwa sahihi ila jambo hili lilifichwa kwao kwa wakati huu, kwani ilipaswa wapitie kipindi hiki ili wapate ufunuo kamili. Kipindi hiki ndipo Yesu Kristo Kwa muujibu wa Daniel 8: 14. Yesu aliingia katika chumba cha patakatifu katika hekalu la mbinguni. safari hii, si kwa damu ya mafahali au wanakondoo, bali kwa damu yake mwenyewe.
"Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele." (Waebrania 9:11).
Hapa ndipo hawa wanamarejeo walipoanza kujifunza upya unabii huu na kufunuliwa siri kubwa zaidi ikiwemo Sabato takatifu, Amri ya nne iliyokanyagwa na Romac Catholic Church.
Hii ndio siri ya unabii wa miaka 2300 na mahubiri ya Wiliiam Miller. habari hizi zilikuwa tamu kwao walipozipokea mara ya kwanza, lakini baadae zikawa chungu ( great dissapointment). Lakini Biblia inasema yakupasa kutoa unabii tena. Na hili Yohana aliliona."Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali. Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu. Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi." ( Ufunuo 10:9-11).