Luther hawezi kuumbuka alishalala mauti miaka mingi iliyopita anasubiri parapanda ya mwisho kuwaamsha waliolala mauti, wengine kwa uzima wa milele na wengine hukumu ya milele. " msistaajabie maneno hayo; kwa maana sa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.Nao watatoka,wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu" (Yohana 5:28-29). Siku hiyo wafu wote akiwemo Mariamu, Abrahamu, Daudi, Petro,Yakobo, Yohana na watakatifu wengine wataisikia sauti ya Bwana wao na kuamka toka kaburini.