MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Porojo nyingi za nani? Kama hawaabudu sanamu kuna haja gani ya kuweka sanamu kanisani? Nipe jibu hapo.
 
Porojo nyingi za nani? Kama hawaabudu sanamu kuna haja gani ya kuweka sanamu kanisani? Nipe jibu hapo.
Good, umeshasema wameziweka kanisani... Ishu unaelewa kwanza maana ya kuabudu au unakurupuka usingizini??? Wenyewe wanasema wanaamini kwa Mungu mmoja aliyezifanya mbingu na nchi we unawaforce wanaabudu sanamu....kama kweli wanaabudu sanamu waje hapa waseme wenyewe...
Mbona wewe unamswalia mtume lakini hawakuingilii....Jaman ombeni neema ya kuijua kweli na kweli itawawek huru..
 
Unawazimu..?
Pole sana mkuu....,hawa jamaa umejitahidi sana kuwaelewesha lkn wanjitia manunda.....!ila natumaini wameelewa tatizo ni ununda wao

Hv huyu Kitaja ebu atuambie William Miller alitumia kifungu gani ktk biblia takatifu kutabiri mwisho wa dunia 1844.......?alafu tumpe maudhui ya hivyo vifungu alivyovitoa....!

Tafsiri zile za upotoshaji za 1844 za bwana Miller ndizo hizi anatuletea leo mjukuu wake bwana Kitaja,nimemuomba bwana Kitaja ebu nipe andiko alilotumia Miller kutabiri mwisho wa dunia na kama hajui aseme........?kukwepa swali sio ishu....
 
MTAZAMO,
Naona unaukaribia ukweli kwa kuwa unapenda kutumia maandiko katika hoja zako.wenzio wengi hawapendi kabisa nukuu za Biblia bali hupenda tusikilize hadithi zao za kutunga.

Sasa nirejee kwenye hoja na nukuu ulizotuwekea hapa.
Nukuu ya Ufunuo 6:9-11 inazungumzia hatima ya watakatifu waliouawa kwa ajili ya Neno la Mungu.Kitabu cha Ufunuo kinatumia lugha ya mafumbo na inahitajika uongozi wa Roho Mtakatifu kuelewa kitabu hiki. Hizo roho zonazolia zinathibitisha kuwa Mungu ni mhukumu wa haki na atawapatia haki watoto wake waliouawa kwa ajili yake. Kwa ufupi mafungu haya humaanisha kwamba Mungu anatambua mateso ya wafia dini na muda si mrefu atalipa kisasi.Mamlaka ile ile iliyohusika kutesa watakatifu wa awali itapata nguvu tena na kuendeleza mateso yake kwa watu wa Mungu wanaotii amri za Mungu."

Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu,nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao,watakaouawa vile vile kama wao." Ufunuo 6:11. Fungu hili huthibitisha kuwa kuna mateso zaidi yatakuja kabla ya Yesu kurudi.Lakini watakatifu wanafarijiwa kuwa bado muda kidogo, wapewe haki yao hii ikiwakilishwa na nguo ndefu, nyeupe.Vazi huwakilisha haki ya Kristo.

Hizo roho pia zinawakilisha hukumu ya upelelezi inayoendelea kwenye madhabahu mbinguni, hao wafia dini wamehakikishiwa wokovu na Mwanakondoo aliyekufa kwa ajili yao. Hata wale watakaouawa kwa namna ile ile pia fungu hili linawahakikishia wokovu. Mamlaka ya kipapa ilitesa watu wa Mungu waliokuwa wamesimama katika kweli.Wale watakatifu waliouawa na kanisa katoliki ndio husemwa hapa.

Hivi karibuni, mamlaka ya kanisa katoliki itarudi kwa nguvu kubwa chini ya new world order.Mateso yatarejea kama zamani." Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, walio huru kwa watumwa,watiwe chapa katika mkono wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao.Tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza,isipokuwa ana ana chapa ile, yaani jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.

Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu.Na hesabu yake ni mia sita,sitini na sita".Ufunuo 13:16-18.
 
Hv huyu Kitaja ebu atuambie William Miller alitumia kifungu gani ktk biblia takatifu kutabiri mwisho wa dunia 1844.......?alafu tumpe maudhui ya hivyo vifungu alivyovitoa....!
Badala ya kukupa jibu, ataingiza mambo ya B/Maria, wafu..nk.nk.

Ni kwamba hakuna msabato atakayeweza kukupa jibu kuwahusu kina Miller, Joseph Bates na wenzake
 
Mateso yatarejea kama zamani." Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, walio huru kwa watumwa,watiwe chapa katika mkono wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao
Aliyekuambia yatarejea kama zamani ni nani ..? Yatarejea lini..? Kwa watu gani...? Bado mnendelezs zile tabiri zenu za kuzimu za kina Miller na EGW...?

Chapa gani hiyo unayoongelea kwa dunia hii ya sasa ..?? Unatuletea mambo ya lesson hapa...?
 
Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo maana ni hesabu ya kibinadamu.Na hesabu yake
Unaelewa dhima ya kitabu cha Ufunuo..? Unafahamu kiliandikwa kuwahusu watu gani..? Unadhani mimi kukuita unawazimu nilikosea..?


Kwanini unatuletea mafundisho ya Miller hapa..?
 
Ufunuo 6:11. Fungu hili huthibitisha kuwa kuna mateso zaidi yatakuja kabla ya Yesu kurudi.
Biblia inatuambia hakuna ajuaye siku wa saa ajaye mwana wa Adamu... Yesu anarudi lini...?

Lakini watakatifu wanafarijiwa kuwa bado muda kidogo
Watakatifu gani hao unaongelea wewe...?

Unataka kuturudisha kule mwaka 1844(Great disappointment)...

Nakuuliza tena unawazimu..?
 
Kitabu cha Ufunuo kinatumia lugha ya mafumbo na inahitajika uongozi wa Roho Mtakatifu kuelewa kitabu hiki. Hizo roho zonazolia zinathibitisha
Yes! Kina tumia mafumbo ambayo maana yake umeshang'amuliwa toka zamani..

Apokalpse ya Yohana haijawahi kuekezea mambo ya nyakati za sasa kamwe...

Ndio maana nimekuuliza unajua dhima ya kitabu hiki..?

Unataka tuanze kukichambua tukianfalia ni lini kiluandikwa, kiliwahusu kina nani...? Walengwa wa kitabu hiki walikuwa wanaishi ktk mazingira gani..?

Bila kuyajua haya utaingia chaka na kuturudisha kwwnye mafundisho pitofu ya William Miller na Ellen G White...

Njoo tujadiliane hapa...
 
Unajificha kwenye chaka la rohomtakatifu na chuki mlizokaririshwa dhidi ya Kanisa katoliki. Huo ufunuo uliosoma, unasema mwisho wa dunia utakapokaribia Kanisa la Kristo litaungana na kuwa moja. Ilimaanisha nini?
 
uongozi wa Roho Mtakatifu kuelewa kitabu hiki. Hizo roho zonazolia zinathibitisha kuwa Mungu ni mhukumu wa haki na atawapatia haki watoto wake waliouawa kwa ajili yake.
Hivi wewe unahitaji Roho Mtakatifu au Manuscript za Ellen G White, Joseph Bates na Hiram....?

Wasabato tangu lini mkamjua Roho Mtakatifu..?
 
Unajificha kwenye chaka la rohomtakatifu na chuki mlizokaririshwa dhidi ya Kanisa katoliki. Huo ufunuo uliosoma, unasema mwisho wa dunia utakapokaribia Kanisa la Kristo litaungana na kuwa moja. Ilimaanisha nini?
Nafikiri alimaanisha kikundi cha Kisabato...

Teh teh teh
 
Hizo roho pia zinawakilisha hukumu ya upelelezi inayoendelea kwenye madhabahu mbinguni, hao wafia dini wamehakikishiwa wokovu na
Hiyo hukumu ya upelelezi inafanywa na nani...?? Mbinguni tangu lini kukawa na mahakama ..? Huu upuuzi umetolea wapi..?

Usikute umeutolea kwenye kitabu cha Kichaa Ellen G White cha ' investigative judgement'....

Ndio maana tunasema Wasabato hawamini ktk Ufufuko wa Yesu...Wasabato siyo Wakristo...

Hukumu ya upelelezi...!!! Unakichaaa...?
 

William Miller, aliyekuwa Mhubiri mashuhuri wa Kibaptisti alisoma katika kitabu cha Danil 8:13. "Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari ya sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lini, kukanyagisha patakatifu na jeshi?
Akamwambia, Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa." Daniel akiwa katika maono aliona yule asi akikanyaga mahala patakatifu na kuiangusha kweli kwa kuleta mafundisho yaliyo kinyume na Neno la mungu, na kisha kutesa watakatifu. Jambo hili lilimsononesha sana Daniel. Ndipo Malaika akampa ufafanuzi kwamba jambo hili lina mwisho wake. "Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri. Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga. Naam, ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaiangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa". Daniel 8:9-12.

Hii Pembe ndogo haina tofauti na pembe ndogo ya Daniel 7:19-27. " Kisha nalitaka kujua maana ya yule mnyama wa nne, aliyekuwa mbali na wenziwe wote, mwenye kutisha sana, ambaye meno yake yalikuwa ya chuma, na makucha yake ya shaba; aliyekula, na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake;
20. na habari za zile pembe kumi zilizokuwa kichwani mwake, na ile pembe nyingine iliyozuka, ambayo mbele yake zilianguka pembe tatu; yaani, pembe ile yenye macho, na kanwa lililonena makuu, ambayo kuonekana kwake kulikuwa hodari kuliko wenzake. 21. Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda; 22 hata akaja huyo mzee wa siku, nao watakatifu wake Aliye juu wakapewa hukumu; na majira yakawadia watakatifu waumiliki ufalme.
23. Akanena hivi, Huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia, utakaokuwa mbali na falme zile zote, nao utakula dunia yote, na kuikanyaga, na kuivunja vipande vipande. 24. Na habari za zile pembe kumi, katika ufalme huo wataondoka wafalme kumi; na mwingine ataondoka baada ya hao; naye atakuwa mbali na hao wa kwanza; naye atawashusha wafalme watatu. 25. Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.
26. Lakini hukumu itawekwa, nao watamwondolea mamlaka yake, kuipoteza na kuiangamiza, hata milele.
27. Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.

Kwa ulinganifu huu utajua wazi kuwa utawala wa nne unaosemwa hapa ni Rumi. Huu n Uatwala wa nne kuitawala dunia yote kuanzia Babeli, Wamedi na Waajemi, Wayunani na Kisha Warumi. Utawala wa kirumi ndio ambao hata Bwana Yesu aliukuta, hakujakuwa na mamlaka yeyote iliyotawala dunia baada ya Rumi. Baadae utawala huu uligawanyika katika mataifa kumi yanayounda Ulaya leo lakini ( pembe tatu kati ya hizo) yaani mataifa matatu yaliangamizwa na Utawala wa Papa baada ya kukataa kumtii hayo mataifa ni Ostrogoths, Vandals na Heruri. Hayapo kabisa " They were terminated by Roman Catholic Pope".

Sasa nirudi katika unabii wa Daniel 8:14. Siku 2300 zinazosemwa hapa huwakilisha miaka 2300. Miller na wenzie walijifunza unabii huu na kugundua kuwa Biblia husema kipindi kile wana israel walipoanza kujenga upya Hekalu la Yerusalemu ndipo unabii huu huanza na kipindi hiki kinaishia mwaka 1844. Biblia inasema baada ya miaka 2300 ndipo patakatifu patatakaswa. Na kwa wana wa Israel kutakaswa kwa patakatifu ilimaanisha hukumu,na kujitesa nafsi zao na kufanya upatnisho wa dhambi zao. Tazama Mambo ya Walawi 16:29, 30; 23:27-29. "Kwa maana siku hiyo upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, ili kuwatakasa; nanyi mtatakaswa na dhambi zenu zote mbele za Bwana....Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto. Nanyi msifanye kazi yo yote siku hiyo; kwa kuwa ni siku ya upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Bwana, Mungu wenu. Kwa kuwa mtu awaye yote asiyejitesa mwenyewe siku iyo hiyo, atakatiliwa mbali na watu wake".

Mwisho wa huduma hii ya patakatifu, dhambi ama zilisamehewa au kukataliwa kutokana na jinsi mdambi alivyojiwasilisha mbele za Mungu kwa sadaka za kuteketezwa. Kwa kuagalia muktadha huu, Miller na wenzie waliamini kuwa mwisho wa mika 2300 yaani mwaka 1844, Patakatifu patatakaswa yaani dunia hii iliyochafuliwa na utawala wa kirumi ingetakaswa. Kwa maana nyingine waliamini kuwa Yesu anakuja kutakasa dunia kipindi hiki. Tafsiri yao ilikuwa sahihi ila jambo hili lilifichwa kwao kwa wakati huu, kwani ilipaswa wapitie kipindi hiki ili wapate ufunuo kamili. Kipindi hiki ndipo Yesu Kristo Kwa muujibu wa Daniel 8: 14. Yesu aliingia katika chumba cha patakatifu katika hekalu la mbinguni. safari hii, si kwa damu ya mafahali au wanakondoo, bali kwa damu yake mwenyewe.

"Lakini Kristo akiisha kuja, aliye kuhani mkuu wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema iliyo kubwa na kamilifu zaidi, isiyofanyika kwa mikono, maana yake, isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele." (Waebrania 9:11).

Hapa ndipo hawa wanamarejeo walipoanza kujifunza upya unabii huu na kufunuliwa siri kubwa zaidi ikiwemo Sabato takatifu, Amri ya nne iliyokanyagwa na Romac Catholic Church.

Hii ndio siri ya unabii wa miaka 2300 na mahubiri ya Wiliiam Miller. habari hizi zilikuwa tamu kwao walipozipokea mara ya kwanza, lakini baadae zikawa chungu ( great dissapointment). Lakini Biblia inasema yakupasa kutoa unabii tena. Na hili Yohana aliliona."Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, Kitwae, ukile, nacho kitakutia uchungu tumboni mwako, bali katika kinywa chako kitakuwa kitamu kama asali. Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu. Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi." ( Ufunuo 10:9-11).
 
Unaelewa dhima ya kitabu cha Ufunuo..? Unafahamu kiliandikwa kuwahusu watu gani..? Unadhani mimi kukuita unawazimu nilikosea..?


Kwanini unatuletea mafundisho ya Miller hapa..?
Shetani kamwe kawezi kukubali kuwa yeye ni muongo. Biblia inasema hujifanya malaika wa nuru, sembuse wafuasi wake.
 
Unaelewa dhima ya kitabu cha Ufunuo..? Unafahamu kiliandikwa kuwahusu watu gani..? Unadhani mimi kukuita unawazimu nilikosea..?


Kwanini unatuletea mafundisho ya Miller hapa..?
Shetani kamwe kawezi kukubali kuwa yeye ni muongo. Biblia inasema hujifanya malaika wa nuru, sembuse wafuasi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…