Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,382
Usipagawe bado kuna nondo zaidi zinakuja. " 1.Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,Hiyo hukumu ya upelelezi inafanywa na nani...?? Mbinguni tangu lini kukawa na mahakama ..? Huu upuuzi umetolea wapi..?
Usikute umeutolea kwenye kitabu cha Kichaa Ellen G White cha ' investigative judgement'....
Ndio maana tunasema Wasabato hawamini ktk Ufufuko wa Yesu...Wasabato siyo Wakristo...
Hukumu ya upelelezi...!!! Unakichaaa...?
2. mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. ( Waebrania 8:1-2).
Bado huamini kuwa mbinguni kuna Hekalu? Haya soma na hii "5. watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
6. Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. ( Waebrania 8:5-6).
Yesu ni Kuhani Mkuu, kwa mujibu wa Biblia upende usipende. Na hivi sasa anahudumu katika Chumba cha Patakatifu katika hekalu lile la Mbinguni, lile ambalo Musa alionyeshwa mlimani ili atengeneze mfano wake hapa duniani. Hekalu halisi liko mbinguni. Hivi karibuni, bado kitambo kidogo, Yesu akihitimisha huduma yake ya upatanisho katika Hekalu la Mbinguni, atarejea duniani kuwachukua aliowakomboa.
Wito: Mwamini Yesu uokolewe, kimbieni kutoka babeli kwani huko kumejaa machafuko yaani mafundisho ya uongo. Tokeni Kwake Mkajitenge nae. "1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.
6 Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu. ( Ufunuo 18:1-6)