MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Hiyo hukumu ya upelelezi inafanywa na nani...?? Mbinguni tangu lini kukawa na mahakama ..? Huu upuuzi umetolea wapi..?

Usikute umeutolea kwenye kitabu cha Kichaa Ellen G White cha ' investigative judgement'....

Ndio maana tunasema Wasabato hawamini ktk Ufufuko wa Yesu...Wasabato siyo Wakristo...

Hukumu ya upelelezi...!!! Unakichaaa...?
Usipagawe bado kuna nondo zaidi zinakuja. " 1.Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni,
2. mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. ( Waebrania 8:1-2).

Bado huamini kuwa mbinguni kuna Hekalu? Haya soma na hii "5. watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.
6. Lakini sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. ( Waebrania 8:5-6).

Yesu ni Kuhani Mkuu, kwa mujibu wa Biblia upende usipende. Na hivi sasa anahudumu katika Chumba cha Patakatifu katika hekalu lile la Mbinguni, lile ambalo Musa alionyeshwa mlimani ili atengeneze mfano wake hapa duniani. Hekalu halisi liko mbinguni. Hivi karibuni, bado kitambo kidogo, Yesu akihitimisha huduma yake ya upatanisho katika Hekalu la Mbinguni, atarejea duniani kuwachukua aliowakomboa.

Wito: Mwamini Yesu uokolewe, kimbieni kutoka babeli kwani huko kumejaa machafuko yaani mafundisho ya uongo. Tokeni Kwake Mkajitenge nae. "1 Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.
2 Akalia kwa sauti kuu, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu mwenye kuchukiza;
3 kwa kuwa mataifa yote wamekunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake, na wafalme wa nchi wamezini naye, na wafanya biashara wa nchi wamepata mali kwa nguvu za kiburi chake.
4 Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.
5 Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.
6 Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni maradufu. ( Ufunuo 18:1-6)
 
Shetani kamwe kawezi kukubali kuwa yeye ni muongo. Biblia inasema hujifanya malaika wa nuru, sembuse wafuasi wake.
Nimekuuliza, unafahamu maudhui ya kitabu cha Ufunuo...?
Mambo ya Shetani ysmeingiaje hapa...?

Shetani ni yupi kati ya huyu bibi Ellen G White aliyeua maelfu ya watu kwa tabiri za kuzimu za ujio wa Yesu...?

Unaakili timamu kweli wewe..?
 
Bado huamini kuwa mbinguni kuna Hekalu? Haya soma na hii "5. watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni,
Nimekuuliza huyo anayefanya hukumu ni nani...?

Kwanini afanye hukumu ya upelelezi..? Anampeleleza nani...? Jibu maswali haya..

Unaweza ukaandika page na page ila upo out of topic...mimi kama mwalimu sutakuonea huruma kwa page ulizoandika, nitakupa sifuri..
 
William Miller, aliyekuwa Mhubiri mashuhuri wa Kibaptisti alisoma katika kitabu cha Danil 8:13. "Ndipo nikamsikia mtakatifu mmoja akinena, na mtakatifu mwingine akamwuliza huyo aliyenena,
Sasa umekuja kwenye kilengeo cha Historia ya Kisabato...

Ninakurudia..
 
Kwa kuagalia muktadha huu, Miller na wenzie waliamini kuwa mwisho wa mika 2300 yaani mwaka 1844, Patakatifu patatakaswa yaani dunia hii iliyochafuliwa na

Hiyo miaka 2300 ni kwa mujibu wa Kalenda gani...?

Kwanini atabiri ujio wa Yesu angali Yesu mwenyewe kasema hakuna ajuaye siku wa saa...?
 
Nimekuuliza huyo anayefanya hukumu ni nani...?

Kwanini afanye hukumu ya upelelezi..? Anampeleleza nani...? Jibu maswali haya..

Unaweza ukaandika page na page ila upo out of topic...mimi kama mwalimu sutakuonea huruma kwa page ulizoandika, nitakupa sifuri..
Ndiyo maan nakupa wito wa kumwmini Yesu. Ukimwamini atakupa ufahamu kuwa Yeye ndiye anahudumu katika Hekalu la mbinguni kama Kuhani Mkuu. Hukumu ya upelelezi, ulisema vizuri kuwa ni Investigative judgement, na ni vizuri kuwa ulisoma hicho ktabu sasa huna la kujitetea kuwa hukujua. Kabla ya Kurudi Kristo lazima makundi mawili yatambulike. Watakao uirithi uzima wa milele na watakaongamia milele. Na ndiyo ya kubagua kondoo na mbuzi inaendelea sasa katika hekalu la mbinguni, kazi hii ikisha Mwana wa Adamu atarejea.

31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;
32 na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi;
33 atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto.
34 Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;
35 kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;
36 nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.
37 Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?
38 Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?
39 Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?
40 Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
41 Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
42 kwa maana nalikuwa na njaa, msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;
43 nalikuwa mgeni, msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni, msije kunitazama.
44 Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa, au u kifungoni, tusikuhudumie?
45 Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia, Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea mimi.
46 Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa milele.

Yesu akija hafanyi tena maombezi bali anatekeleza hukumu ambayo inaendelea sasa. Jisalimishe kwa Yesu kabla mlango haujafungwa ndugu.
 
Waliamini yeye na nani...? Wapi imeandikwa au kunenwa dunia ingetakaswa...?

Nyie Wasabato mnakichaa..
Naona mistari ya Biblia inakupa shida maana umelewa mvinyo wa uasherati wa yule "kahaba mkuu". Hadi utoke uko ndipo utapata ufahamu.
 
Nimekuuliza, unafahamu maudhui ya kitabu cha Ufunuo...?
Mambo ya Shetani ysmeingiaje hapa...?

Shetani ni yupi kati ya huyu bibi Ellen G White aliyeua maelfu ya watu kwa tabiri za kuzimu za ujio wa Yesu...?

Unaakili timamu kweli wewe..?
Maudhui ndiyo hayo ninayokupa hapa, hakuna muadhui zaidi ya yale yaliyoelezwa humo. Tatizo ule mvinyo umekuchanganya hata huwezi kuelewa. Wewe unadhani unaweza kubishana na Neno la Mungu kwa kutumia maarifa yako? mnasikitisha sana.Ndio maana mmekazana kuabudu sanamu na kuwaomba wafu wawaombee, huku mkimwacha Yesu Kristo Kuhani wetu Mkuu anayetuombea sasa kwa Baba.
 
umeanza vizuri,ukaharibu mwishoni!
aya ya kwanza uko sahihi,zilizobakia zote umepotosha!
ila kabla ya kuendelea,nenda kasoma zile 95 thesis za luther,halafu uje hapa!
Nashangaa sana wakati hizi no muhimu katika U-protestant
 
Ndiyo maan nakupa wito wa kumwmini Yesu. Ukimwamini atakupa ufahamu kuwa Yeye ndiye anahudumu katika Hekalu la mbinguni kama Kuhani Mkuu.
Nataka uniambie ni wapi pameandikwa Yesu anafanya hukumu ya Upelelezi...? Ana mpelelezs nanni...?

Kazi aliyoifanya pale msalabani ilikuwa ni bure...?
 
Naona mistari ya Biblia inakupa shida maana umelewa mvinyo wa uasherati wa yule "kahaba mkuu". Hadi utoke uko ndipo utapata ufahamu.
Hili ndio jibu la swali nililokuuliza..

Turudi kwa Miller maana huko ndio tutaufukunyua Usabato kwa undani....
 
Maudhui ndiyo hayo ninayokupa hapa,
maudhui gani...??

hakuna muadhui zaidi ya yale yaliyoelezwa humo.
Hapo umesema unanipa....Ila hapa unasema hakuna maudhui...una akili timamu...?

Tatizo ule mvinyo umekuchanganya hata huwezi kuelewa.
Kuelewa kitu gani...? Nielewe porojo za Ellen G White...?

Wewe unadhani unaweza kubishana na Neno la Mungu kwa kutumia maarifa yako? mnasikitisha sana.Ndio maana mmekazana kuabudu sanamu na kuwaomba wafu wawaombee, huku mkimwacha Yesu Kristo Kuhani wetu Mkuu anayetuombea sasa kwa Baba.
Unafahamu maudhui ya kitabu cha Ufunuo...? Swali la msingi hilo
 
Yesu ni Mungu....Mungu anamuombea nani.. na kwa nani...???
Huwezi kuelewa siri hii ya ukombozi kupitia kwa Yesu Kristo. Yesu ni Mungu ndiyo, na ni mwandamu pia ndiyo maana alitwaa mwili huu unaokufa, kwani Mungu hapatikani na mauti,Lakini Mungu alimfufua katika wafu. Ndiyo maana Paulo anasema yu hai siku zote atuombee.

Pitia hapa Waebrania 7:24-26.
24 bali yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka.
25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee.
26 Maana ilitupasa sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii aliye mtakatifu, asiyekuwa na uovu, asiyekuwa na waa lo lote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;

Soma tena 1 Yohana 2:1-2.
1 Watoto wangu wadogo, nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda dhambi tunaye Mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki,
2 naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu; wala si kwa dhambi zetu tu, bali na kwa dhambi za ulimwengu wote.

Bado unabisha kuwa Yesu ni mwombezi wetu kwa Baba?
 
Nataka uniambie ni wapi pameandikwa Yesu anafanya hukumu ya Upelelezi...? Ana mpelelezs nanni...?

Kazi aliyoifanya pale msalabani ilikuwa ni bure...?
Naona ssa unakuja katika msitari. mwanzo ulikuwa unakataa kuwa Hakuna hekalu mbinguni, Biblia imekujibu kuwa hekalu liko mbinguni na ndio lile Musa alionyeshwa mlimani. Ukaja na Hoja kuwa Yesu ni Mungu hivyo anaomba kwa nani? Biblia imekujibu kuwa Yesu ni Kuhani wetu Mkuu akituombea kwa Baba. Naona sasa umeng'an'gana na hukumu ya upelelezi. Yesu Yuko katika hekalu la mbinguni akifanya huduma ya upatanisho kabla ya kurejea duniani kuwachukua wale waliotubu na kumuamini, hao ndio waliomwamini na kutubu dhambi zao kupitia kwa Yesu Kristo. Hii ndio huitwa hukumu ya upelelezi, matendo yetu wote yanachunguzwa ikiwa ni mema au mabaya, kama tumemkiri Yesu Kristo ama tumemkataa. Lengo la hukumu hii, ni kuwabagua kondoo na mbuzi. Hii huduma inaendelea upende usipende na kadri mnavyozidi kumkataa Yesu Kristo na huduma yake hii, ndivyo mnavyojitenga naye. Mafungu ya wapi pameandikwa yapo tele nilishaweka humu pitia kwa faida yako na wenzio.
 
B/Maria ni Mtakatifu hivyo....
Sio Bikira Maria Pekee, Watakatifu wote jukumu lao ni kutuombea....Soma Ufunuo 5:8 uone Wazee 24 , wakizunguka kiti cha Mwana Kondo(Yesu) wanafanya nini..?

Ngoja nikuandikie
Ufunuo 5:8
Hata alipokitwa kile kitabu, hao wenye uhai 4 na wazee 24, walianguka mbele za mwana kondoo, kila mmoja na kinubi na vitasa vya dhabu vilivyojaa manukato, ambayo ni MAOMBI YA WATAKATIFU


Hivyo ni wazi, watakatifu kazi yao ni kutuombea...Sasa sijui utapingana na hapo pia...
Je bikra Maria ni miongoni mwa hawa wazee 24?
 
Huwezi kuelewa siri hii ya ukombozi kupitia kwa Yesu Kristo.
Kuna mtu mwingine aliyefanya ukombozi zaidi ya Yesu...? Ni nani huyo...?

Yesu ni Mungu ndiyo, na ni mwandamu pia
Hii kauli ilitumika kipindi Yesu akiwa hapa duniani....Kwasasa Yesu ni Mungu...

ndiyo maana alitwaa mwili huu unaokufa, kwani Mungu hapatikani na mauti,Lakini Mungu alimfufua katika wafu. Ndiyo maana Paulo anasema yu hai siku zote atuombee.
Yesu anakuombea kwa nani...?
 
Back
Top Bottom