MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Kwani Yesu alipoambiwa mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona Yesu aliwajibu nini?.....mama wa Yesu alikuwa ni kama bahasha tu itumikayo kubeba barua basi na ndiyo maana hata Yesu hakumsifia sifia mama yake........
 
Kama sio uhasi wa Luther uenda haya makanisa ya wapiga dili na ibada za kutoa mapepo yasingekuwep.. Ok, yeye alijitoa kanisa Katoliki, mbona na yeye anapingwa na jamii ya walokole?
Huenda martin luther asingejitoa leo hii dunia nzima ingekuwa inaabudu masanamu kama wanavyoabudu wakatoliki
 
Duh kaaazi kweli kweli hapo ndo mlipo mpa cheo binadamu mwenzenu awe mwombezi. mmesahau kwamba mariam na yeye ni binadamu kama niniyi na alishakufa anasubiri ufufuo siku ya mwisho.. sasa sijui nani kawadanganya kwamba maria yuko hai...... Au ni katika kitabu gani kimemtaja Mariam Kwamba yi hai ambapo anaweza kusikia maombi yenu
Mkuu hao ndugu kuabudu wafu ni kawaida sana kwao na ni sehemu ya ibada ndo maana hawaoni taabu kumuabudu marehemu mama wa Yesu
 
Kwataarifa yako Biblia ya Martin Luther siyo tu ilikuwa na mapungufu ya vitabu 7 vya Agano la Kale, pia aliondoa vitabu vya Yakobo, Waebrania na kitabu cha Ufunuo..

Reformet mwenzake Calvin ndio alimzuia kuondoa vitabu hivyo vya Agano Jipya na ndipo Luther akavirejesha vitabu hivyo..
Huu ni uzishi wa kanisa katoliki ili tuone kwamba luther alikuwa pinga pinga
 
Mkuu we ninani hadi umpinge mtu ambaye aliweka agano na Mungu?unadhani uwepo wa bikra Mariam ni wakibahati mbaya?soma Bible vizuri,halafu tuliza akili yako vzr,achana na mapokeo ya mafundisho ya wachungaji wako,fikiri vizuri,Wakati Mungu akimtumia ujumbe Mariam hapakuwepo na wanawake wengine,kwanini bikra Mariam?,Yaani Mungu Baba aweke agano la milele na Na Mama yule wewe useme she is noboby,ama kweli,watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa!!!!
Kama kila alieweka agano na Mungu ni wakuabudiwa kama mnavyomwabudu maria bas mbona hammwabudu Ibrahimu Ester Isaka Nuhu Paulo n.k.....nyinyi wakatolik mnapotezwa na hayo mapokeo yakipagani kuliko kawaida.

Ndio maana wakatolik biblia wanazo lakin kusoma hawazsomi kiufasaha ispokuwa wamejikita katika visacrament ambavyo 100% viko kinyume na mafundisho ya biblia....unakuta mtu kashika rozari picha za bikira maria scapulari na mishumaa eti vitendea kaz vya sala.....jaman mnaangamia hivihivi kwa kumezeshwa uongo na mapapa wenu.
 
Otorong'ong'o,
Kwanini unaita uasi mkuu?....hivi mtu akikataa kuabudu sanamu kama ambavyo Abednego Shedrack na Meshac walijataa kuabudu sanamu hivyo walikuwa waasi? Anaepaswa kutuombea makosa yetu ili tusamehewe ni Yesu tu sasa iweje leo nyinyi mtuambie mama yake yesu ndiye mwombez wetu ilhali biblia haijasema hvyo na endapo tukikataa mnatuita waasi.

kwakweli shetani namuona anazd kukaa ndani ya kanisa katoliki maana yale makatazo yote wao kwao ni Ruksa mfano pombe ruksa kuabudu sanamu ruksa kuabudu wafu ruksa yaan adi imefikia hatua wanatambua mashoga na wasagaji
 
The Son of Man,
Historia inaonyesha wazi kuwa Mamlaka ya Papa ilitesa na kuangamiza Wakristo, hasa katika kilele cha utawala wake katika karne za kati. Wanahistoria wengi wanasema zaidi ya watu milioni hamsini waliuawa kwa ajili ya imani zao katika kipindi cha dhiki kuu.

Sababu kuu ya kuuawa na kuteswa kwao ilikuwa ni kupinga na kukataa kutambua kanisa KATOLIKI kama kanisa la Mungu ,hivyo walitakiwa kuuawa au kuteswa ili "wazushi" hawa wanyamazishwe
Dokezo la Biblia kuhusu ukatii huu,imeandikiwa

“Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili. Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake; na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na KUWASHINDA, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa. Ufunuon 13:5-7

PAPA FRANCIS AOMBA MASAMAHA

Papa Francis awaomba radhi Waprotestanti ,BBC WANARIPOTI

26 Januari 2016

Katika hatua ya kujumuisha umoja wa kikristo, Papa Francis amewaomba radhi waumini wa Kiprotestanti kutokana na unyanyasaji walioupata kutoka kanisa Katoliki miaka ya nyuma.

Papa Francis amewataka waumini wa kanisa Katoliki pia kuwasamehe wale ambao waliwakosea ili wasiruhusu makosa yaliyotendeka nyuma kuwa sumu ya mahusiano ya sasa. Kufuatia tamko hilo msemaji wa Vatcan ametangaza kuwa Papa Francis atazuru mji wa Lund uliopo Swedish eneo ambalo jumuiya ya Kilutheri ilianzishwa na kuanzisha thehebu la Kilutheri karne tano zilizopita.


KUHUSU Mauji ya RWANDA

PAPA FRANCIS AMEKUBALI KUWA KANISA KATOLIKI LILIHUSIKA KATIKA MAUAJI HAYO AMBAPO WATU ZAIDI YA 800,00O WALIUAWA ,BBC WANARIPOTI

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameomba msamaha kutoka kwa Mungu kwa "dhambi na makosa yaliyotekelezwa na Kanisa na waumini wake ambao walitekwa na chuki na ghasia" wakati wa mauaji ya kimbari Rwanda.

Alikuwa akiongea baada ya kukutana na Rais Paul Kagame mjini Vatican.

Ombi lake la msahama limetokea baada ya ombi la Rwanda Novemba mwaka jana kwa Vatican kuomba radhi kutokana na mchango wa mapadri wa kanisa Katoliki na baadhi ya viongozi wake wakati wa mauaji hayo ya mwaka 1994.
-----
haya ni machache yalifunuka hata tukayaona ,je kuna mangapi ambayo hatuyajuai ?

Je kanisa KATOLIKI limebadilika? ,LA HASHA ! hapana kanisa hili halitabadilika kamwe bali litabadili namna ya utendaji wake kulingana na wakati ,hii ni kwa sababu kanisa hili linapata nguvu KUTOKA kwa shetani mwenyewe soma,Ufunuo wa Yohana 13 : 2


BIBLIA INASEMA NINI KUHUSU KANISA HILI KATILI

Note:mwanamke katika unabii humaanisha kanisa ,hapa Mungu analielezea kanisa KATOLIKI na watoto wake [makanisa yote yanayopinga amri za Mungu] kwa kutumia mwanamke kahaba na binti zake ,kama kuna mahali hutaelewa uliza

Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake. Akanichukua katika Roho hata jangwani, nikaona mwanamke, ameketi juu ya mnyama mwekundu sana, mwenye kujaa majina ya makufuru, mwenye vichwa saba na pembe kumi -

Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI. - Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.Ufunuo wa Yohana 17 : 1-6

Mungu anajua mateso yanayosababishwa na kanisa KATOLIKI kwa watu wake ,hukumu yake inaafaliwa

Wakatoliki waaminifu wafanye nini ?

Mungu anasema

Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.- Kwa maana dhambi zake zimefika hata mbinguni, na Mungu amekumbuka maovu yake.Ufunuo wa Yohana 18 : 4-5
 
Deogratius Kisandu,
Mkuu umenielimisha kiasi asee!!
Nikuombe utuandikie kauzi kuhusu mambo yafuatayo ambayo huniacha njia panda sana:
1.Kwanini katoliki humwita Maria aliyemzaa Yesu "Mama wa Mungu"?
2.Kwanini wakatoliki humwomba Mungu kupitia Kwa Maria?
3. Kwanini wakatoliki humwita Maria Bikira hadi leo ili hali alishazaa watoto na isitoshe alikuwa mke halali wa mwanamume?
4.Kwanini wakatoliki wanamwita Maria Malkia wa mbingu? Kama ni Malkia Mfalme wake ni nani?
5.Kwanini wakatoliki wanapigia magoti(wanasujudia)sana ya wanayemwita Maria na kuipelekea maombi yao?
6.Somo la Rozari wakatoliki waliitoa wapi? Je ni kweli Maria aliagiza kanisa kusali rozari?
7.Kwanini katoliki kupitia michoro na sanamu zake Mara nyingi anayeitwa yesu huonesha akiwa mtoto tu na akibebwa na mama ambaye yeye(mama)kamwe hajawahi kuoneshwa akiwa katika hali ya utoto!!
8. Japo biblia haijasema kuhusu kufa na maziko ya Maria, bt Katoliki wanasema hakufa alipalizwa, please nifafanulie hapa Mkuu!!
9. Idea ya centralized church under cheo cha mtawala aitwaye pope katoliki waliitoa wapi hii Mkuu
10. Nitauliza baadae!

Natanguliza shukrani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Kwani Maria alipoombwa awaombee kwa Yesu , Yesu alimjibuje? Na alipojibiwa kwanini aliwageuzia kibao waliomwomba awaombee kwamba "lolote atakalowaambia fanyeni" Maria alijua fika kwamba sio yeye apaswae kuombwa bali Yesu mwenyewe tens moja kwa moja ndio maana akawajibu kuwa watekeleze lile wanaloambiwa na Yesu.

We jamaa hebu let's andiko jingine linalosapoti andiko lako kwanini hili andiko la harusi ya kana kamwe halimhalalishii marehemu Maria kupelekewa maombi, lakini awe maria mwingine lakini sio wa bibliani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Lakini pia sio mbaya ukitujulisha Maria anayeombwa alikuwa na kiwango gani cha Elimu, Kadhalika Yesu, Petro, Yakobo, Yohane, Mathayo n.k walikuwa na elimu kiwango gani mpaka leo hii tuwaamini?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biblia inasema Bikra Maria ataitwa mbarikiwa, na dunia itamsifu kuwa yeye ni mbarikiwa. Bikra Maria kwa mujibu wa kumbukumbu za kanisha hakufa, alipaazwa. Ujui historia, huyu mama ni the special, hata waprotestant wakimtupa sisi Wakatoliki tutaendelea kutimiza unabii kwa kumuita mbarikiwa
Mkuu kumbukumbu za kanisa au kumbukumbu za Roman Catholic?

Kumbuka kumbukumbu za kanisa zote zapaswa kuwa maandiko matakatifu ya neno la Mungu. Kama Mtume Paul aliyeandika nyaraka nyingi zaidi za agano jipya hajamshadidia maria kwa namna yoyote ile hii Catholic ilishadidia issue za Maria kivipi!! Nahisi kuna Maria Mwingine hivi Mkuu, manake sifa za maria wa Catholic kamwe hazi Match kabisa na sifa za Maria wa kwenye Biblia Takatifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanisa Katolik limekuwepo hata kabla ya uislam. Hivyo maktaba ya Vatican imeshiba
Lakini Kristo, ukristo wala mitume na manabii walioandika Vitabu ndani ya biblia hawakuwahi kuwa wenyeji wa Vatican na pengine wengine hadi wanakufa hawakuwahi kuijua Vatican wala Italy.

Lakini sambamba na hill ukristo pia haukuwahi kutajwa kuwa umechimbukia Italy, kanisa Catholic kamwe halijawahi kuwa kanisa wala dhehebu la kwanza la Kikristo.

Rejea nyaraka saba kwa Malaika wa makanisa saba katika kitabu cha Ufunuo, kisha utuambie waraka wa kanisa Catholic uliisahaulikaje kutambulikana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma Ufunuo uone jinsi Yohane anapata ufunuo..

"Tazama ishara ikaonekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota 12 juu ya kichwa chake"
Wee jamaa huko unakoelekea siko kabisa! Ukituambia huwa mwanamke ni maria itabidi utufungulie fumbo hili gumu pasi na shaka vinginevyo usitumie mafunuo ambayo huyaelewi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu we ninani hadi umpinge mtu ambaye aliweka agano na Mungu?unadhani uwepo wa bikra Mariam ni wakibahati mbaya?soma Bible vizuri,halafu tuliza akili yako vzr,achana na mapokeo ya mafundisho ya wachungaji wako,fikiri vizuri,Wakati Mungu akimtumia ujumbe Mariam hapakuwepo na wanawake wengine,kwanini bikra Mariam?,Yaani Mungu Baba aweke agano la milele na Na Mama yule wewe useme she is noboby,ama kweli,watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa!!!!
Mkuu unajitahidi kueleza kwa hekima za kibinadamu tu japo Si vibaya. Lakini kwa hekima za Mungu kazi ya Maria ilikuwa ni kumzaa Yesu baada ya hapo Maria hakuwa na mamlaka yoyote juu ya kumcontrol Yesu katika Utendaji wake.

Bila biblia Inakiri Maria alipata upendeleo wa kumpitisha Masihi kwaneema tu, sio kwamba alistahili kuliko binadamu wengine, lakini pia isingewezekana wanawake wote wacha Mungu wamzae mtu mmoja. Hivyo Neema(upendeleo)ulimtulia Maria. Kumbuka ukiacha Catholic pekee hamna mtume yeyote wa Yesu hata mwanae Maria mwenyewe mdogo wake Yesu aitwae mtume Yakobo hakuwahi kumhubiri mama yake kwa lolote.

Injili ilichapwa kumu address Yesu kristo wa Nazareth na Si vinginevyo. Ndio maana huwa najiuliza mbona sifa za Catholic Mary hazifanani na sifa za Biblical Mary?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Otorong'ong'o,
Mkuu imani kwamba kulikuwa na kanisa moja tu ni fix kuu!! Hebu soma nyaraka za mitume wa Yesu vizuri, kisha malizia Ufunuo sura ya 2 kuanzia mstari wa kwanza uniambie malaika wa Makanisa saba yalioandikiwa nyaraka saba Catholic iko wapi hapo Mkuu!

Mitume wa Yesu walianzisha makanisa mengi tu isipokuwa Catholic. Na how come Italy ianzishe kanisa na huku chimbuko la kanisa ni Yesu Myaudi, mwebrania? Hebu nipe elimu juu ya makanisa saba yaliyotajwa kwenye Revelation 2, uniambie,
Je, yalitajwa kabla au baada ya kuwepo kwa Catholic Church?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mkatoliki, nilibatizwa mwaka wa 1970, nilizaliwa mwaka 1968 NA sasa Nimefikisha miaka 50 na miezi kadhaa. Kwa kweli niseme tu, hizo kashifa dhidi ya kanisa letu hazikuanza Leo, zipo tangu zamani miaka ya nyuma sana na ziliasisiwa miaka 1880 NA waprostetant wa karne hizo NA baadaye walikuja wasabato akina Helen white na baadaye kabisa walikuja mathehebu ya kilokole ambapo mpaka wanaendeleza chuki zao NA kashifa zao dhidi ya kanisa NA Pope Francis.

Mimi nilibahatika kusoma baadhi ya nyaraka au vitabu mbalimbali vinavyoelezea historia ya mapapa NA ukatoliki, pope wa Kwanza kabisa ambaye kaburi lipo Vatican City pale Saint Peters Busilica, alikuwa mtume PETRO NA baadaye wengi wamekuja NA kuondoka duniani maana duniani tunapita tu, makao yetu ni mbinguni kwa Baba. Kuna suala LA kuwaombea materemu, waprotestanti wanalipinga hilo, lakini wanasahau kusoma MT 12:32, kumbe upo msamaha baada ya kifo. Kwahiyo, sisi hutuabudu sanamu na wala hatumtegemei mwanadamu kuishi bali tunayo SALA YA BABA YETU rejea misale ya waamini ambayo hiyo sala imerejea andiko LA biblia Mt 6:9-13.

Kuhusu sala ya bikira Maria, sisi hatumwabudi bali tunamwamba kupitia tu kwake kwa kuwa MUBGU mwenyewe kupitia malaika akimtamkia kuwa amebalikiwa NA kupewa NEEMA na Bwana NA Bwana yu pamoja naye na atamzaa MTOTO mwanaume NA jina lake ni YESU, mwana wa aliyejuu, Mungu mkuu rejea Lk 1:26-31, Isa 7:14, 9:6, MT 1:21-23, Lk 1:30-35.

Pia, Mama bikira watu walikuwa wakimfuata kumwomba amwambie mwanaye awatekelezee mahitaji yao, rejea wakati wa harusi ya Kana, hata DIVAI ilipokuwa ilipokuwa imewatindikia kwa biblia ya kiingereza by Gideon anasema when the wine ran out, the mother of Jesus said to the Jesus, they have no wine and Jesus said to his mother, my hour has not yet come and mother told the servants do whatever he tells you, Ina maana hawa watumishi wa waliomba kupitia kwa mama Maria na Yesu alifanya muujiza kwa kubadili maji kuwa divai, Yn 2:1-11.

Kwa Leo naishia hapa, nitaendelea tena kujibu hoja kwa kadiri MUNGU atakavyoniongoza.
 
[QUOTE="The Son of Man,
Mkuu hapo kwenye red correction,si kwamba vile vingine vinapingana na mafundisho yao bali vinapingana na maandiko mengine ya kwenye biblia so hazikuwa sababu za kibinadamu.Unajua kuna kitu watu hawajui,mambo mengine Mungu huruhusu kwa sababu zake.

Kwa mfano mchungaji aliyekutwa amelewa huko Dar,vipimo vikaonyesha amelewa,sasa hapo unataka Mungu afanye nini?Mungu anaonyesha watu kwamba hapo mimi sipo wewe bado upo tu,matokeo yake mchungaji anaulizwa redioni"je kunywa pombe ni dhambi?Anajibu inategemea mlivyokubaliana kanisani.Hawezi sema ni dhambi kwa kuwa yeye mwenyewe mnywaji.

Kasome kitabu cha ufunuo zile barua kwa makanisa saba,kuna makanisa Mungu hayupo ,aliyepo ni shetani.Hizo siyo hadithi hata leo kuna makanisa Mungu hayupo aliyepo ni shetani.
 
Back
Top Bottom