Mkuu kwa hili huna data.... Martine hakuwa Askofu, alikuwa Padre na miongoni mwa sababu zilizomuondoa kwenye kanisa Katoliki ni hili la Uaskofu, alipinga hairakia ya Kanisa na vyeo kama Uaskofu, Upapa na mengineyo. Sema tu mengi aliyoyapinga aliishia kuayatenda akiwa kwenye kanisa lake. Mengine ni suala la Useja, hakutaka kabisa kulisikia na alipoondoka aliondoka na Mtawa wa kike aliyeishia kuwa mkewe.
Mambo ni mengi sana na yanahitaji muda wa kutosha. Lakini niseme tu kwamba "siyo kila alilolipinga lilikuwa baya" mengine aliyapinga kihalali kabisa japo njia aliyoitumia haikuhalalisha kitendo chake!!!
Pili, Biblia za wapeotestanti na wapentekoste zina vitabu 66 wakati biblia ya Wakatoliki ina vitabu 72. Hili lilitokana na kuwa baadhi ya yaliyomo kwenye vitabu hivyo (deuterokanoni) vinapingana na mafundisho yao. Sababu nyingi ni za kibinadamu tu!!! Hili lilikuwa rahisi sana kwake kwani suala zima la "Utaifa" liliingizwq kwenye huu mchakato wa Luther kujiondoa kanisa, matokeo yake kwa vile alikuwa Mjerumani, dhehebu lake likawa "dini dora" ya Ujerumani, katika hali kama hii, ni rahisi kwa uwezo wa kifedha kuchapisha Biblia zenye vitabi 66 na kuviondoa vile vingine!!!!