Mjadala: Maisha yamekufundisha nini mpaka umri huo uliofikia?

Mjadala: Maisha yamekufundisha nini mpaka umri huo uliofikia?

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
Mimi ni kuhusu kutomuamini mlevi - maisha yamenifundisha kutomuamini mlevi kabisa, hasa akiongea wakati kalewa!

Pili, maisha yamenifundisha mafanikio yanakuhitaji wewe moja kwa moja bila kutegemea msaada kutoka kwa mtu yoyote ili tu akushike mkono uinuke hapo ulipo, sio kweli.

Maisha haya yamenifundisha kutokuamini ahadi mtu anazokuwekea kabisa, yaani kutokuweka matarajio makubwa kutokana tu na ahadi ya mtu.

Wewe yamekufundisha nini mpaka umri huo umefikia? Bado tunajifunza!
 
Ukifanikiwa jijengee mizizi ya kupata pesa kwanza saidia kwa kiasi watu hawatakumbuka ulijinyima kiasi gani kuwasaidia...wataona kufeli kwakuo utaambiwa huna akili ya maisha hata huna starehe utaambiwa ni mpenda starehe kwasababu tu uko chini kiuchumi,usiseme mafanikio yako mbele za watu mipango yako au chochote wewe fanya tu.....watu ni wanafiki san sana....Sali sana
 
Maisha yamenifundisha kumwamini mwenyezi Mungu na hakuna linalishindikana kwake. Ukipata mtihani lia na Mwenyzi Mungu bila kuchoka hakika njia zinafunguka na ukiona hupati mwanga basi jua bado hujamwomba sawa sawa zidisha kumwomba na kua na imani naye kwa ukubwa.
 
Back
Top Bottom