Mjadala: Matatizo ya Makocha WA mpira wa miguu Tanzania

Mjadala: Matatizo ya Makocha WA mpira wa miguu Tanzania

mjasiriamali mdogo

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2013
Posts
258
Reaction score
110
Wanamichezo naomba tujadili Kwa kina Matatizo ya Makocha wetu WA mpira miguu hapa nchini.

Kwanini Makocha wetu hawaendi kufundisha nje ya Tanzania.

Wana udhaifu gani na ni changamoto zipi wanazokumbuna ambazo huwafanya washindwe kutekeleza majukumu yao Kwa ufasaha.
 
Cha kwanza hawaamini katika Sayansi ya mpira na teknolojia katika soka, wenyewe wanaamini kwamba ushindi wa Timu ni mipango ya Mungu/Uchawi.

Jaribu kufatilia interview za makocha wa Tanzania baada ya mechi huwa wanasema tumeshinda kwa uwezo wa mwenyezi mungu na bla blah nyingine hapo zisizo za kiufundi.
 
Sayansi ya mpira ni ipi au nini naombaa ufafanuzi nipate kujifunza?
 
Sayansi ya mpira ni ipi au nini naombaa ufafanuzi nipate kujifunza?
Tactical formations na maelekezo yake, Training sessions(sio kila siku inapaswa watu kufanya mazoezi ya kukimbia au Gym) pia kila mchezaji inapaswa afundishwe zaidi mazoezi fulani kulingana na nafasi anayocheza,

Game analysis kabla na baada ya mechi(kujua mpinzani wako na kulinganisha na wachezaji wako na ubora wao),...Kujua uwezo wa wachezaji na nafasi wanazostahili kucheza,

Kuwa mshauri mkuu kwa wachezaji wako na kuzingatia nidhamu,

Kuwaelekeza wachezaji kwa kutumia hisabati(hii ni pana zaidi) ila kwa kufupisha wachezaji kuna kipimo cha nafasi huwa wanatakiwa wapishane kutoka mchezaji mmoja mpka mwingine yani mfano kutoka Beki wa kati mpka wa Kushoto kuna space wanatakiwa wapishane.

Hayo ni baadhi tu ya mambo yaliyopo kwenye Football science
 
Naomba takwimu za makocha wageni wanaofundisha nje ya nchi zao, ili nifahamu ni wengi kwa kiasi gani! Halafu kabla ya kukimbilia kwa hao makocha, tujiulize ni kitu gani tumefanikiwa ndani ya hii nchi kiasi cha kututangaza Kimataifa?
 
Ili uajiliwe nje ya nchi kwanza wanaangalia cv yako, elimu ya ukocha, vilabu ulivyofundisha na matokeo uliyopa. Hapo wanaangalia vikombe ulivyochukua, au kupandisha timu daraja. Sio Kama huku Kiemba anateuliwa kocha wa taifa wakati hajawahi kufundisha hata timu moja.
Pia anaweza kuanza timu ndogo huku akijenga cv yake.
Kinachowqkwqmisha makocha wetu ni elimu, lugha na utamaduni wetu.
 
tatizo linaanzia hata kuongea na waandishi lazima utasikia 'nashukuru nungu mechi imeisha salama mpira unamatokeo matatu.' yani hiyo ni kila kocha wa bongo kaimeza
Vilaza mno mpaka wachezaji wao
 
1. Unauhakika hakuna makocha wa Tanzania wanaofundisha mpira nje ya nchi?
2. kama kwa makocha wetu kuna shida, kwanini makocha wanatoka nje ya nchi kuja kusoma kozi za makocha za hapa kwetu?
3. watanzania huwa tunajichukulia poa sana, hadhi ya makocha wetu kwa sasa ni kubwa ila bado hatuupi mpira wetu heshima inayotakiwa.
 
Makocha wa bongo hata simba na yanga hawapewi. Unataka wapewe man city?
HAKUNA KOCHA BONGO

Halafu wanabet mpaka timu zao!!
kutopewa simba na yanga haimaanishi hatuna makocha wazuri, mbona hata hao mnaosema wameendelea kwenye mpira bado tim zao hazina makocha wazawa kwenye timu kubwa.. mfano madrid, barcelona, man city, liverpool, PSG, man U, wote wanamakocha wakigeni
 
tactics za kisasa,training pia na kuandaa mechi kulingana na mpinzani
mbona timu za vijana za taifa zinaongozwa na makocha wazawa na zinafika hadi kombe la dunia.. sijajua ukisema tactic za kisasa unamaanisha nini, kila tim inafanya ivyo kujiandaa na mpinzan tofauti inakuja kwenye quality ya wachezaji wetu, wanaweza kutimiza majukumu yao ya kifundi vile inatakiwa, wachezaji wengi quality ni ndogo kulingana na mahitaji wa waalim
 
Ili uajiliwe nje ya nchi kwanza wanaangalia cv yako, elimu ya ukocha, vilabu ulivyofundisha na matokeo uliyopa. Hapo wanaangalia vikombe ulivyochukua, au kupandisha timu daraja. Sio Kama huku Kiemba anateuliwa kocha wa taifa wakati hajawahi kufundisha hata timu moja.
Pia anaweza kuanza timu ndogo huku akijenga cv yake.
Kinachowqkwqmisha makocha wetu ni elimu, lugha na utamaduni wetu.
usikariri kaka.. kiemba analeseni B ya CAF.
1. mpaka unapewa leseni B ni umefundisha chini ya uangalizi si chini ya miaka 4 mpaka 5. kiemba kafundisha tim tofauti tofauti za vijana na hata za kimashindano ni kwamba haujawahi mfuatilia. tatizo watanzania tunahisi mtu amekuja tu ghafla wakati watu wanatumia muda kutengeneza CV zao wakifanikiwa mnahisi wametokea tu ghafla wakapewa tim.
2. huwezi pewa nafasi kwenye tim ya taifa kama hawajui uwezo wako, ile nafasi sio upendeleo kapambana na ameonekana ana uwezi ndio maana kupewa.. HAKUNA KOCHA KWENYE MPIRA ANATOKEA GHAFLA, WATU WANATENGENEZWA
3. kuna kundi kubwa la wachezaji vijana linatengenezwa kwenye vituo vya TFF ninauhakika wakija kuitwa kucheza tim ya taifa mtasema hawachezi ligi kuu kwann wanaitwa
 
Back
Top Bottom