Mjadala mkubwa wa wanachama, washabiki na wapenzi wa Yanga waliopo JF (Wana Simba hawaruhusiwi)

Mjadala mkubwa wa wanachama, washabiki na wapenzi wa Yanga waliopo JF (Wana Simba hawaruhusiwi)

Kuisifu Simba kufanya vizuri kwa sababu ya usajili wa bilioni 1.3 ni kupotoka. Ukweli ni kwamba kile si kikosi cha hicho kiasi cha fedha.

Simba amechukua kombe msimu huu si kwa sababu ina kikosi bora, bali ni kwa sababu ya ubovu wa washindani wake (hususani Yanga na Azam)

Back to the topic. Tatizo la Yanga ni kubwa kuliko usajili wa msimu unaokwisha, tatizo la Yanga mfumo mbovu wa kutegemea fedha za mtu ili kuendesha timu.
Simba imekuwa bora mkuu, usipingane na hili. Angalia point walizofikisha ukilinganisha na bingwa wa misimu iliyopita.
 
...
Simba amechukua kombe msimu huu si kwa sababu ina kikosi bora, bali ni kwa sababu ya ubovu wa washindani wake (hususani Yanga na Azam).
Bado unarudi pale pale. Kama sababu ni ubovu wa washindani wake, kuna namna nyingine ya kuondoa ubovu huo zaidi ya kuwekeza katika kikosi? Kumbuka, huo uwekezaji unapangiwa bajeti si ya usajili tu, bali hadi malipo ya mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi. Hao ndio direct labor. Sasa huo mfumo wa uwekezaji uwe rasmi na kutambulika kisheria, kama ni hisa au vinginevyo, sio mambo yategemee mawazo au uamuzi wa mtu mmoja
 
Simba imekuwa bora mkuu, usipingane na hili. Angalia point walizofikisha ukilinganisha na bingwa wa misimu iliyopita.
Wamekuwa bora ukilinganisha na nani? Kama ni bora kuliko simba ya msimu uliopita nitakubaliana na wewe. Lakini ninaomba uniruhusu nikatae kwa nguvu zote kwamba akina boko ni kikosi cha bilioni 1.3.

Yanga wana kikosi kizuri, lakini wote tunajua kilichotokea mwanzo wa msimu kwa kiongozi na mtoa hela wa Yanga.

Sababu nyingine kama majeruhi ya muda mrefu pia vimechangia kushusha kiwango cha Yanga. Lakini sababu ya msingi ni mtikisiko wa kiuchumi waliopata Yanga msimu huu.
 
Bado unarudi pale pale. Kama sababu ni ubovu wa washindani wake, kuna namna nyingine ya kuondoa ubovu huo zaidi ya kuwekeza katika kikosi? Kumbuka, huo uwekezaji unapangiwa bajeti si ya usajili tu, bali hadi malipo ya mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi. Hao ndio direct labor. Sasa huo mfumo wa uwekezaji uwe rasmi na kutambulika kisheria, kama ni hisa au vinginevyo, sio mambo yategemee mawazo au uamuzi wa mtu mmoja
Uwekezaji wa bilioni 1.3 hauusiki na fedha za mishahara, zile ni fedha za usajili tu....kwa mujibu msemaji wa simba, utanisahihisha kama msemaji wa Simba katoa takwimu Mpya, nyingine. Hivyo uwekezaji ninaongelea ni huo wa usajili.

Uwekezaji mwingine, kama fedha za benchi la ufundi, mishahara n.k hata Yanga waliuweka, kwenye makaratasi. Lakini utekelezaji ukawa mgumu baada ya Manji kupata misukosuko.
 
Simba imekuwa bora mkuu, usipingane na hili. Angalia point walizofikisha ukilinganisha na bingwa wa misimu iliyopita.
Hahaaaaaaa yanga mwaka 2015-16 ilichukua ubingwa na point 72. So simba angevuka hapo tungekubali. Simba kachukua ubingwa kwa uzembe au kupotea kwa wapinzani wake yanga na Azam ila sio kwa usajili mzuri. Maana wafugaji mnao wawili tu unadhani ungekuwa vizuri kwa kupotea wa watani zako ulipaswa uwe na magoli zaidi ya 60
 
Kwa kweli hatua za haraka sana kwa sisi wanayanga inabidi tufanye ili kuinusuru hali hii.
 
Timu yetu inahitaji stable income na utaona matokeo,wachezaji hawawezi kucheza kwa moyo na kujituma huku wanadai hela za usajili na mishahara ya miezi 3,Yanga ina wapenzi na washabiki wasiopungua millioni sita tanzania nzima ,tukichukua wapenzi na wanachama 1,000,000 kila mwezi tuchange TZS 1000 au buku timu itaingiza billion moja na hutasikia njaa tena na hapo watapata na hela za kuwekeza kwenye miradi inayolipa.
 
Mimi ni simba damu ila huu mjadala nauvamia kibabe kabisa, mmetuonea sana misimu minne mfululizo,. Sasa nasema hivi nawaombea njaa iendelee kulitafuna litimu lenu na jumatano taifa mfungwe 4G nyingine.
 
Vyura wameususia Uzi wako Kama walivyoisusia kandambili fc!

Kwa ufupi Mimi natamani njaaa iendelee mpaka msambaratike na timu lenu lifeee! Na mwakani lishuke daraja rasmi! Shuuubamit!

[HASHTAG]#Kima[/HASHTAG] wa Taifa#

Mkuu wakishuka daraja tutakua wapweke sana, wabaki tu ligi kuu ila wapigike kidogo kidogo ha ha
 
Mimi ni simba damu ila huu mjadala nauvamia kibabe kabisa, mmetuonea sana misimu minne mfululizo,. Sasa nasema hivi nawaombea njaa iendelee kulitafuna litimu lenu na jumatano taifa mfungwe 4G nyingine.
Sio misimu mnne ni misimu 5 hamjulikani mnashiriki ligi gani
 
Tatizo la yanga ni uongozi, kile kikosi ni kizuri kuliko hata cha Simba
 
Tatizo la yanga ni uongozi, kile kikosi ni kizuri kuliko hata cha Simba
Eti kikosi kuliko cha simba kwani viongozi ndo wanacheza Mpira? . hebu kubarini tu msimu huu mmekuwa vibogoyo hamna meno.
 
...Maana wafugaji mnao wawili tu unadhani ungekuwa vizuri kwa kupotea wa watani zako ulipaswa uwe na magoli zaidi ya 60
Kwa nini watani waonekane kuwa na haki ya kupotea? Kwa nini ni sawa kwa Yanga kuwa na magoli 40, lakini si sawa kwa Simba kuwa na magoli 60?
 
Sio misimu mnne ni misimu 5 hamjulikani mnashiriki ligi gani
Zungumzia msimu huu, maana mleta mada amefungua uzi kutathmini Yanga ilipokwama msimu huu wa 2017/2018, na wala hajasema tutathmini misimu iliyopita
 
Tunataka kufikia wakati Washabiki tufungue Account ambayo italipa
wachezaji moja kwa moja na Kocha bila kupitia kwa uongozi wa
Klabu, itapitia kwenye uongozi wetu Mashabiki.
 
Hahaaaaaaa yanga mwaka 2015-16 ilichukua ubingwa na point 72. So simba angevuka hapo tungekubali. Simba kachukua ubingwa kwa uzembe au kupotea kwa wapinzani wake yanga na Azam ila sio kwa usajili mzuri. Maana wafugaji mnao wawili tu unadhani ungekuwa vizuri kwa kupotea wa watani zako ulipaswa uwe na magoli zaidi ya 60

Simba ina kikosi bora, ina timu bora uwanjani, ina benchi bora kuliko zote. Yanga ya 2015/2016 ilikuwa bora lakini ligi ilikuwa dhaifu kuliko mwaka huu. Tumeona timu zaidi ya 5 nzuri msimu huu, haijawahi kutokea huko nyuma ambako kulikuwa na timu 3 tu tena Simba ikiwa hoi pia.

Leo angalia Singida United, Prisons, Lipuli, Mwadui, Stand United, Mtibwa Sugar na hata Masao Bwire FC. Ni timu nzuri bila ubishi. Msimu ujao inaweza kuwa balaa zaidi
 
Hahaaaaaaa yanga mwaka 2015-16 ilichukua ubingwa na point 72. So simba angevuka hapo tungekubali. Simba kachukua ubingwa kwa uzembe au kupotea kwa wapinzani wake yanga na Azam ila sio kwa usajili mzuri. Maana wafugaji mnao wawili tu unadhani ungekuwa vizuri kwa kupotea wa watani zako ulipaswa uwe na magoli zaidi ya 60
Hata Yanga ilichukua ubingwa miaka hiyo sababu Simba ilikuwa hoi kifedha.
 
Back
Top Bottom