Mjadala mpya: Ni nani aliwaokoa abiria 24 wa ndege ya Precision Air?

Mjadala mpya: Ni nani aliwaokoa abiria 24 wa ndege ya Precision Air?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi, majeruhi na vifo kama habari husika inahusika na ajali, uharibifu mwingine huja mwishoni.. Na hapo katikati ya tarahuki kuna mengi hutokea ya ukweli ya kuzusha na ya uongo pia.. Na kuna wakati kuna kikundi ama vikundi ndio hufanya haya kwasababu zozote zile.

Taharuki ikishakoma, kuna ukweli na uhalisia ambao haukusemwa kabla hujifunua taratibu. Maana uongo hupanda lift na kufika haraka lakini ukweli hukwea ngazi na kufika mwishoni.

Ajali ya ndege ya Precision iliyotokea pale Bukoba na kuondoka na roho za watanzania 19 nayo imepitia mlolongo huo huo. Sasa hali imetulia, waliosalimika wamesalimika, majeruhi wanaendelea na matibabu (tunawaombea nafuu ya mapema) na waliopoteza maisha wameshazikwa na kuacha simanzi, majonzi na maumivu kwenye familia, kwa ndugu jamaa hata marafiki. Natanguliza kuwapa pole sana katika kipindi hiki kigumu.

Ajali haina ratiba! Ajali hii ilitokea tayari mama akiwa na ratiba ya kusafiri nje ya nchi kikazi.. Kuahirisha pengine isingewezekana hivyo alifanya alipoweza na kuwaachia wa chini yake waendelee. Pamoja na lawama nyingi za kwanini taifa limepata tukio kama hilo na yeye ni kama hakuonesha kujali sana lakini mjadala mkubwa zaidi ukawa kwenye ishu nzima ya uokoaji. Vifaa duni, kuchelewa kufika eneo la tukio timu ya uokoaji, kutojali uzembe nknk.. Serikali ya CCM ikasakamwa kila kona. Kwahiyo ilibidi kutafutwa haraka matukio ya kuchepusha hii mijadala.

Haya ndio matukio mawili yenye kufikirisha maana yamepewa uzito mkubwa kuliko ajali yenyewe.

Tukio la kwanza ni MWOKOZI MAJALIWA. Huyu ni mvuvi anayesemekana ndio alifungua mlango wa ndege kwa kasia lake na kuingia ndani na kuanza kuokoa abiria waliokwama katikati ya taharuki ya ajali hakuna waliojishughulisha kuhoji uwezo wa kasia kuweza kufungua mlango wa ndege. Katikati ya taharuki hakuna aliyehoji ni nani walimwokoa Majaliwa aliyezirai na kukimbizwa hospital. Katikati ya taharuki hakuna aliyekuwa na muda wa kuhoji kama kuna wahudumu wa ndege wenye ujuzi waliokuwa wakisaidiana na watu wengine kuokoa abiria waliokwama.

Ni katikati ya taharuki hii ndio mvuvi Majaliwa akaokota dodo la bure.. Kwa kasi ya ajabu akatajwa kuwa ndiye aliyewaokoa abiria wale 24. Kwa kasi ya ajabu UVCCM wakampongeza. Kwa kasi ya ajabu PM akatangaza kumpatia nafasi kwenye jeshi la uokozi Tanzania. Kwa kasi ya ajabu akapatiwa na ulinzi na kutembezwa huku na kule. Kuna picha zikisemwa alialikwa bungeni na ikulu. Ghafla bin vuu mijadala mitandaoni ikawa ni juu ya Majaliwa na zile habari za lawama na udhaifu kwenye uokoaji zikapigwa kikumbo kikubwa sana.

Tukio la pili uzinduzi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita milion 70 kwa siku. Sambamba na ajali lakini wiki ile hali ilikuwa mbaya sana kwenye upatikanaji wa maji jijini. Mgao ulikuwa mkali kwakweli. Mbaya zaidi haikuwa maji tu bali na hata umeme hali haikuwa nzuri.

Pamoja na tukio la Majaliwa kukawa na matamko ya viongozi wa kisiasa kwamba kuna maji ya kigamboni yataingizwa Dar haraka kufidia upungufu. Mara likaandiwa tukio la kuzindua kisima cha kigamboni na mgeni rasmi akapangwa kuwa rais ambaye bado alikuwa nje ya nchi.

Kiukweli Kisima tajwa limezinduliwa kisiasa zaidi.. Kisima hiki kikubwa kiko barabara ya kuelekea Mwasonga, kiko kilometer mbili toka Kibada.. Kiuhalisia huu mradi haukupaswa kuzinduliwa sasa kwakuwa maji hayawafikii wateja kwa Bluetooth bali kwa kupitia mabomba. Kazi inayoendelea sasa ni kutandaza mabomba na kujenga sub stations. Maji bado hayajawafikia walaji. Kazi iliyopo baso ni kubwa si kazi ya wiki 2 au mwezi
Kisima husika kiko jirani kabisa na viwanda kama saba hivi vya wachina, ambao waliambiwa kuvifunga siku hiyo ya uzinduzi.

Mshangao ulikuwa juu ya mgeni rasmi na wingi wa waalikwa. Kwa uwazi walisema ule mradi si wa kumuita rais auzindue ilikuwa ni kazi ya waziri wa maji na hakukuwa na haja ya kualika umati wote ule wa watu.

Matukio haya mawili yamepita na pengine yamesaidia sana kuzipa mamlaka nafasi ya kupumua na kujipanga. Lakini sasa kuna ukweli mwingi unajidhihiri hasa kwenye ajali ile ya ndege. Abiria wale walionusurika ambao sasa kiwewe na taharuki vimewaisha na akili zao kukaa sawa wanashangazwa kumuona mitandaoni na ndani ya CCM akitajwa kama ndiye aliyewaokoa! Wana simulizi nyingine tofauti kabisa hasa wakiwataja mabinti wawili wahudumu kuwa ndio waliowaokoa.

Tamati yangu
Mamlaka ziliharakisha mno kumkweza Majaliwa ambaye hata hivyo naye aliokolewa na kujikuta hospital! Lakini bado hatujachelewa tuna nafasi bado ya kujirudi na kujisahihisha ili tuwatambue na kuwapa heshima zao wale walioongoza uokoaji. Wavuvi waliomuokoa Majaliwa. Wahudumu wa ndege wale mabinti wawili. Na wengine wote muhimu kwa nafasi zao kwa siku ile husika! Kuwabeza hawa wengine kuwa walikuwa wapi siku zote hakulisaidii taifa kwakuwa ukweli na uhalisia huwa havifichiki.
 
20221114_120603.jpg
 
Mimi kuna muda huwa najiuliza swali moja tu, hivi kuna uwezekano gani kasia kuvunja mlango wa ndege, katika utengenezaji wa ndege wapo makini zaidi katika usalama wa vijaa vyake, leo iwe rahisi tu mtu avunje mlango tena sio kwa kitu kizito bali wa kasia. Hapa ndio napopata mashaka, emergency door ulifunguliwe na mhudumu wa ndani na kuokoa hawa 24.
 
Watambuliwe wote waliokuwa na mchango. Kuna wanaosema hao wakina Dada walitimiza tu majukumu yao wakisahau kwamba kwenye ajali inatakiwa ujasiri mkubwa.

Ni vizuri ifahamike walifanya nini na watambulike ipasavyo. Kama inabidi iwe majaliwa na hostess iwe hivyo. Sio lazima iwe majaliwa au mahostess. Na kama wako wengine wajumuishwe pia.
 
Nendeni mkawatafuate waathirika wa hiyoo ajali zaidi ya 20 wapo hai..wawekeni meza moja na majaliwa mtawahoji..wanaocomments umu hakuna wahusika,mnachoshana tu
Tumeshawahoji tumeongea nao wametueleza kilichotokea ndio maana jamii inahoji
 
Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi,
Mhubiri 9:11 (September Eleven)

[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all.
 
Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi, majeruhi na vifo kama habari husika inahusika na ajali, uharibifu mwingine huja mwishoni.. Na hapo katikati ya tarahuki kuna mengi hutokea ya ukweli ya kuzusha na ya uongo pia.. Na kuna wakati kuna kikundi ama vikundi ndio hufanya haya kwasababu zozote zile.
Mhubiri 9:11 (September Eleven)

[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all.
 
Nina uhakika Majaliwa hakufanya uokozi peke yake, walikuwepo wengine na bila shaka walifanya kazi kubwa, ila tujue jambo moja dhahiri ni kwamba kila mtu ana bahati yake hapa duniani, Mungu ndio hupanga yote, muacheni kijana apate sifa anayopata, hata Nyerere hakutafuta Uhuru peke yake, na bado tunamuita Baba wa Taifa.
 
Mhubiri 9:11 (September Eleven)

[11]Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all.
Asante sana kwa hiki kifungu, maana naona sasa wafanyakazi wa Jeshi la uokoaji baada ya kunangwa sasa wanataka Majaliwa aonekane si chochote.
 
Back
Top Bottom