Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani shida nini, ungempinga kwa hoja maana ye ameleta uzi uliojaa hoja kibao fikirishi ila wewe umemjibu kwa matusi! Hivyo ndivyo mnavyofundishwa huko Lumumba?Punguza kujifanya unajua kila kitu,unakopi thd za JF kuhusu hii issue,unaziunganisha kisha unaanzisha Thd kwa ID yako! huu ni zaidi ya ujinga aisee.
Hoja zimeshajibiwa,kuna thd kibao kuhusu hiyo issue,huyo kakopi thd za JF hapa hapa akaziunganisha na kuanzisha thd yake,Kwani shida nini, ungempinga kwa hoja maana ye ameleta uzi uliojaa hoja kibao fikirishi ila wewe umemjibu kwa matusi! Hivyo ndivyo mnavyofundishwa huko Lumumba?
Wapuuzi huwa wanapuuzwa hawajibiwi..kwakuwa hawana uwezo wa kuandika hata theluthi ya kitu chenye hojaKwani shida nini, ungempinga kwa hoja maana ye ameleta uzi uliojaa hoja kibao fikirishi ila wewe umemjibu kwa matusi! Hivyo ndivyo mnavyofundishwa huko Lumumba?
Sasa kulikuwa na haja gani kumshambulia mtoa mada!? Kama aliyoandika umeshakutana nayo kwingine ungepita kimya utuache wengine tuchangie. Kumtusi mtu usiyemfahamu ni kiwango cha juu kabisa cha ukosefu wa busara.Hoja zimeshajibiwa,kuna thd kibao kuhusu hiyo issue,huyo kakopi thd za JF hapa hapa akaziunganisha na kuanzisha thd yake,
Halafu usiwe zuzu wewe,Lumumba ndio nini? unafikiri kila mtu humu ni shabiki wa mambo ya kisiasa?
Wewe ndio mpuuzi,hoja gani umeweka hapo zaidi ya kukopi mawazo ya watu wa humu JF? ni mara nyingi tu hapa JF kitu kikitrend unasubiri watu wakijadili hapa kisha unakuja kukopi idea za watu na kuanzisha thd kisha watu wanakuona bonge la GT.Wapuuzi huwa wanapuuzwa hawajibiwi..kwakuwa hawana uwezo wa kuandika hata theluthi ya kitu chenye hoja
Wewe uliposema "Ndio mnavyofundishwa hivyo Lumumba" ulikua unamtusi nani? au hiyo ndio busara unayoiongelea hapa?Sasa kulikuwa na haja gani kumshambulia mtoa mada!? Kama aliyoandika umeshakutana nayo kwingine ungepita kimya utuache wengine tuchangie. Kumtusi mtu usiyemfahamu ni kiwango cha juu kabisa cha ukosefu wa busara.
Tusi liko wapi hapo kwenye sentensi yangu? Naona unataka kuchepusha mada, acha watu wajadiliane wawezavyo usiwavuruge.Wewe uliposema "Ndio mnavyofundishwa hivyo Lumumba" ulikua unamtusi nani? au hiyo ndio busara unayoiongelea hapa?
Tulia.Tusi liko wapi hapo kwenye sentensi yangu? Naona unataka kuchepusha mada, acha watu wajadiliane wawezavyo usiwavuruge.
Mshana Jr. kama ukiamua kwa thati kutia mchango katika baadhi ya mambo ni dhahiri shahiri ungeleta matokeo chanya kwa kiasi kikubwa, katika uzi wa awali uliokuwa unahusiana na mvuvi aliyeokoa watu 24, nilidoubt kwa kuuliza kuwa kwanini mvuvi huyo amulikwe kuliko wavuvi wengine waliosaidia kuwaokoa watu, kwa bahati mbaya sana hakuna aliyenijibu, sasa kama na mleta mada kaliona hili na kuamua kulianzishia uzi labda linaweza kusaidia kuleta mwanga wa sintofahamu iliyogubika suala hili.Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi, majeruhi na vifo kama habari husika inahusika na ajali, uharibifu mwingine huja mwishoni.. Na hapo katikati ya tarahuki kuna mengi hutokea ya ukweli ya kuzusha na ya uongo pia.. Na kuna wakati kuna kikundi ama vikundi ndio hufanya haya kwasababu zozote zile.
Taharuki ikishakoma, kuna ukweli na uhalisia ambao haukusemwa kabla hujifunua taratibu. Maana uongo hupanda lift na kufika haraka lakini ukweli hukwea ngazi na kufika mwishoni.
Ajali ya ndege ya Precision iliyotokea pale Bukoba na kuondoka na roho za watanzania 19 nayo imepitia mlolongo huo huo. Sasa hali imetulia, waliosalimika wamesalimika, majeruhi wanaendelea na matibabu (tunawaombea nafuu ya mapema) na waliopoteza maisha wameshazikwa na kuacha simanzi, majonzi na maumivu kwenye familia, kwa ndugu jamaa hata marafiki. Natanguliza kuwapa pole sana katika kipindi hiki kigumu.
Ajali haina ratiba! Ajali hii ilitokea tayari mama akiwa na ratiba ya kusafiri nje ya nchi kikazi.. Kuahirisha pengine isingewezekana hivyo alifanya alipoweza na kuwaachia wa chini yake waendelee. Pamoja na lawama nyingi za kwanini taifa limepata tukio kama hilo na yeye ni kama hakuonesha kujali sana lakini mjadala mkubwa zaidi ukawa kwenye ishu nzima ya uokoaji. Vifaa duni, kuchelewa kufika eneo la tukio timu ya uokoaji, kutojali uzembe nknk.. Serikali ya CCM ikasakamwa kila kona. Kwahiyo ilibidi kutafutwa haraka matukio ya kuchepusha hii mijadala.
Haya ndio matukio mawili yenye kufikirisha maana yamepewa uzito mkubwa kuliko ajali yenyewe.
Tukio la kwanza ni MWOKOZI MAJALIWA. Huyu ni mvuvi anayesemekana ndio alifungua mlango wa ndege kwa kasia lake na kuingia ndani na kuanza kuokoa abiria waliokwama katikati ya taharuki ya ajali hakuna waliojishughulisha kuhoji uwezo wa kasia kuweza kufungua mlango wa ndege. Katikati ya taharuki hakuna aliyehoji ni nani walimwokoa Majaliwa aliyezirai na kukimbizwa hospital. Katikati ya taharuki hakuna aliyekuwa na muda wa kuhoji kama kuna wahudumu wa ndege wenye ujuzi waliokuwa wakisaidiana na watu wengine kuokoa abiria waliokwama.
Ni katikati ya taharuki hii ndio mvuvi Majaliwa akaokota dodo la bure.. Kwa kasi ya ajabu akatajwa kuwa ndiye aliyewaokoa abiria wale 24. Kwa kasi ya ajabu UVCCM wakampongeza. Kwa kasi ya ajabu PM akatangaza kumpatia nafasi kwenye jeshi la uokozi Tanzania. Kwa kasi ya ajabu akapatiwa na ulinzi na kutembezwa huku na kule. Kuna picha zikisemwa alialikwa bungeni na ikulu. Ghafla bin vuu mijadala mitandaoni ikawa ni juu ya Majaliwa na zile habari za lawama na udhaifu kwenye uokoaji zikapigwa kikumbo kikubwa sana.
Tukio la pili uzinduzi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita milion 70 kwa siku. Sambamba na ajali lakini wiki ile hali ilikuwa mbaya sana kwenye upatikanaji wa maji jijini. Mgao ulikuwa mkali kwakweli. Mbaya zaidi haikuwa maji tu bali na hata umeme hali haikuwa nzuri.
Pamoja na tukio la Majaliwa kukawa na matamko ya viongozi wa kisiasa kwamba kuna maji ya kigamboni yataingizwa Dar haraka kufidia upungufu. Mara likaandiwa tukio la kuzindua kisima cha kigamboni na mgeni rasmi akapangwa kuwa rais ambaye bado alikuwa nje ya nchi.
Kiukweli Kisima tajwa limezinduliwa kisiasa zaidi.. Kisima hiki kikubwa kiko barabara ya kuelekea Mwasonga, kiko kilometer mbili toka Kibada.. Kiuhalisia huu mradi haukupaswa kuzinduliwa sasa kwakuwa maji hayawafikii wateja kwa Bluetooth bali kwa kupitia mabomba. Kazi inayoendelea sasa ni kutandaza mabomba na kujenga sub stations. Maji bado hayajawafikia walaji. Kazi iliyopo baso ni kubwa si kazi ya wiki 2 au mwezi
Kisima husika kiko jirani kabisa na viwanda kama saba hivi vya wachina, ambao waliambiwa kuvifunga siku hiyo ya uzinduzi.
Mshangao ulikuwa juu ya mgeni rasmi na wingi wa waalikwa. Kwa uwazi walisema ule mradi si wa kumuita rais auzindue ilikuwa ni kazi ya waziri wa maji na hakukuwa na haja ya kualika umati wote ule wa watu.
Matukio haya mawili yamepita na pengine yamesaidia sana kuzipa mamlaka nafasi ya kupumua na kujipanga. Lakini sasa kuna ukweli mwingi unajidhihiri hasa kwenye ajali ile ya ndege. Abiria wale walionusurika ambao sasa kiwewe na taharuki vimewaisha na akili zao kukaa sawa wanashangazwa kumuona mitandaoni na ndani ya CCM akitajwa kama ndiye aliyewaokoa! Wana simulizi nyingine tofauti kabisa hasa wakiwataja mabinti wawili wahudumu kuwa ndio waliowaokoa.
Tamati yangu
Mamlaka ziliharakisha mno kumkweza Majaliwa ambaye hata hivyo naye aliokolewa na kujikuta hospital! Lakini bado hatujachelewa tuna nafasi bado ya kujirudi na kujisahihisha ili tuwatambue na kuwapa heshima zao wale walioongoza uokoaji. Wavuvi waliomuokoa Majaliwa. Wahudumu wa ndege wale mabinti wawili. Na wengine wote muhimu kwa nafasi zao kwa siku ile husika! Kuwabeza hawa wengine kuwa walikuwa wapi siku zote hakulisaidii taifa kwakuwa ukweli na uhalisia huwa havifichiki.
Zama deep kidogo mkuu liwe neno la leotime and chance happeneth to them all.
Tufani ikishatulia na taharuki kwisha ndio kuna ukweli halisi hutamalaki.. Hiki ndio kipindi chake sasa...!Mshana Jr. kama ukiamua kwa thati kutia mchango katika baadhi ya mambo ni dhahiri shahiri ungeleta matokeo chanya kwa kiasi kikubwa, katika uzi wa awali uliokuwa unahusiana na mvuvi aliyeokoa watu 24, nilidoubt kwa kuuliza kuwa kwanini mvuvi huyo amulikwe kuliko wavuvi wengine waliosaidia kuwaokoa watu, kwa bahati mbaya sana hakuna aliyenijibu, sasa kama na mleta mada kaliona hili na kuamua kulianzishia uzi labda linaweza kusaidia kuleta mwanga wa sintofahamu iliyogubika suala hili.
Machadomo huwa Yana shida sanaAcheni wivu kijana mdogo nyota imeenda kwake mishipa inawatoka
Kuhusu uchunguzi Black box itasema kila kitu bahati nzuri ufaransa wekejitolea kufanya uchunguzi
Mkuu hatukatai kuhusiana na ngekewa, lakini pia tukubali kuwa ngekewa zinaweza kuchochewa na baadhi ya watu kwa masirahi binafsiNina uhakika Majaliwa hakufanya uokozi peke yake, walikuwepo wengine na bila shaka walifanya kazi kubwa, ila tujue jambo moja dhahiri ni kwamba kila mtu ana bahati yake hapa duniani, Mungu ndio hupanga yote, muacheni kijana apate sifa anayopata, hata Nyerere hakutafuta Uhuru peke yake, na bado tunamuita Baba wa Taifa.
Kwa hayo ulizungumza nakanusha inaonyesha yakua huna uchambuzi sahihi juu ya hili..Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi, majeruhi na vifo kama habari husika inahusika na ajali, uharibifu mwingine huja mwishoni.. Na hapo katikati ya tarahuki kuna mengi hutokea ya ukweli ya kuzusha na ya uongo pia.. Na kuna wakati kuna kikundi ama vikundi ndio hufanya haya kwasababu zozote zile.
Taharuki ikishakoma, kuna ukweli na uhalisia ambao haukusemwa kabla hujifunua taratibu. Maana uongo hupanda lift na kufika haraka lakini ukweli hukwea ngazi na kufika mwishoni.
Ajali ya ndege ya Precision iliyotokea pale Bukoba na kuondoka na roho za watanzania 19 nayo imepitia mlolongo huo huo. Sasa hali imetulia, waliosalimika wamesalimika, majeruhi wanaendelea na matibabu (tunawaombea nafuu ya mapema) na waliopoteza maisha wameshazikwa na kuacha simanzi, majonzi na maumivu kwenye familia, kwa ndugu jamaa hata marafiki. Natanguliza kuwapa pole sana katika kipindi hiki kigumu.
Ajali haina ratiba! Ajali hii ilitokea tayari mama akiwa na ratiba ya kusafiri nje ya nchi kikazi.. Kuahirisha pengine isingewezekana hivyo alifanya alipoweza na kuwaachia wa chini yake waendelee. Pamoja na lawama nyingi za kwanini taifa limepata tukio kama hilo na yeye ni kama hakuonesha kujali sana lakini mjadala mkubwa zaidi ukawa kwenye ishu nzima ya uokoaji. Vifaa duni, kuchelewa kufika eneo la tukio timu ya uokoaji, kutojali uzembe nknk.. Serikali ya CCM ikasakamwa kila kona. Kwahiyo ilibidi kutafutwa haraka matukio ya kuchepusha hii mijadala.
Haya ndio matukio mawili yenye kufikirisha maana yamepewa uzito mkubwa kuliko ajali yenyewe.
Tukio la kwanza ni MWOKOZI MAJALIWA. Huyu ni mvuvi anayesemekana ndio alifungua mlango wa ndege kwa kasia lake na kuingia ndani na kuanza kuokoa abiria waliokwama katikati ya taharuki ya ajali hakuna waliojishughulisha kuhoji uwezo wa kasia kuweza kufungua mlango wa ndege. Katikati ya taharuki hakuna aliyehoji ni nani walimwokoa Majaliwa aliyezirai na kukimbizwa hospital. Katikati ya taharuki hakuna aliyekuwa na muda wa kuhoji kama kuna wahudumu wa ndege wenye ujuzi waliokuwa wakisaidiana na watu wengine kuokoa abiria waliokwama.
Ni katikati ya taharuki hii ndio mvuvi Majaliwa akaokota dodo la bure.. Kwa kasi ya ajabu akatajwa kuwa ndiye aliyewaokoa abiria wale 24. Kwa kasi ya ajabu UVCCM wakampongeza. Kwa kasi ya ajabu PM akatangaza kumpatia nafasi kwenye jeshi la uokozi Tanzania. Kwa kasi ya ajabu akapatiwa na ulinzi na kutembezwa huku na kule. Kuna picha zikisemwa alialikwa bungeni na ikulu. Ghafla bin vuu mijadala mitandaoni ikawa ni juu ya Majaliwa na zile habari za lawama na udhaifu kwenye uokoaji zikapigwa kikumbo kikubwa sana.
Tukio la pili uzinduzi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita milion 70 kwa siku. Sambamba na ajali lakini wiki ile hali ilikuwa mbaya sana kwenye upatikanaji wa maji jijini. Mgao ulikuwa mkali kwakweli. Mbaya zaidi haikuwa maji tu bali na hata umeme hali haikuwa nzuri.
Pamoja na tukio la Majaliwa kukawa na matamko ya viongozi wa kisiasa kwamba kuna maji ya kigamboni yataingizwa Dar haraka kufidia upungufu. Mara likaandiwa tukio la kuzindua kisima cha kigamboni na mgeni rasmi akapangwa kuwa rais ambaye bado alikuwa nje ya nchi.
Kiukweli Kisima tajwa limezinduliwa kisiasa zaidi.. Kisima hiki kikubwa kiko barabara ya kuelekea Mwasonga, kiko kilometer mbili toka Kibada.. Kiuhalisia huu mradi haukupaswa kuzinduliwa sasa kwakuwa maji hayawafikii wateja kwa Bluetooth bali kwa kupitia mabomba. Kazi inayoendelea sasa ni kutandaza mabomba na kujenga sub stations. Maji bado hayajawafikia walaji. Kazi iliyopo baso ni kubwa si kazi ya wiki 2 au mwezi
Kisima husika kiko jirani kabisa na viwanda kama saba hivi vya wachina, ambao waliambiwa kuvifunga siku hiyo ya uzinduzi.
Mshangao ulikuwa juu ya mgeni rasmi na wingi wa waalikwa. Kwa uwazi walisema ule mradi si wa kumuita rais auzindue ilikuwa ni kazi ya waziri wa maji na hakukuwa na haja ya kualika umati wote ule wa watu.
Matukio haya mawili yamepita na pengine yamesaidia sana kuzipa mamlaka nafasi ya kupumua na kujipanga. Lakini sasa kuna ukweli mwingi unajidhihiri hasa kwenye ajali ile ya ndege. Abiria wale walionusurika ambao sasa kiwewe na taharuki vimewaisha na akili zao kukaa sawa wanashangazwa kumuona mitandaoni na ndani ya CCM akitajwa kama ndiye aliyewaokoa! Wana simulizi nyingine tofauti kabisa hasa wakiwataja mabinti wawili wahudumu kuwa ndio waliowaokoa.
Tamati yangu
Mamlaka ziliharakisha mno kumkweza Majaliwa ambaye hata hivyo naye aliokolewa na kujikuta hospital! Lakini bado hatujachelewa tuna nafasi bado ya kujirudi na kujisahihisha ili tuwatambue na kuwapa heshima zao wale walioongoza uokoaji. Wavuvi waliomuokoa Majaliwa. Wahudumu wa ndege wale mabinti wawili
Na wengine wote muhimu kwa nafasi zao kwa siku ile husika! Kuwabeza hawa wengine kuwa walikuwa wapi siku zote hakulisaidii taifa kwakuwa ukweli na uhalisia huwa havifichiki.
Mkuu kwa kutumia elimu yako ya kiroho uliyonayo nina imani Kuna mengi umeyaona, ingawa uzi huu umeuleta kwa lugha ya kawaida ili kila mmoja ashiriki kwa amani tunaomba utusanue walau hata kwa dokezo.Tufani ikishatulia na taharuki kwisha ndio kuna ukweli halisi hutamalaki.. Hiki ndio kipindi chake sasa...!