Mjadala mpya: Ni nani aliwaokoa abiria 24 wa ndege ya Precision Air?

Mjadala mpya: Ni nani aliwaokoa abiria 24 wa ndege ya Precision Air?

Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi, majeruhi na vifo kama habari husika inahusika na ajali, uharibifu mwingine huja mwishoni.. Na hapo katikati ya tarahuki kuna mengi hutokea ya ukweli ya kuzusha na ya uongo pia.. Na kuna wakati kuna kikundi ama vikundi ndio hufanya haya kwasababu zozote zile.

Taharuki ikishakoma, kuna ukweli na uhalisia ambao haukusemwa kabla hujifunua taratibu. Maana uongo hupanda lift na kufika haraka lakini ukweli hukwea ngazi na kufika mwishoni.

Ajali ya ndege ya Precision iliyotokea pale Bukoba na kuondoka na roho za watanzania 19 nayo imepitia mlolongo huo huo. Sasa hali imetulia, waliosalimika wamesalimika, majeruhi wanaendelea na matibabu (tunawaombea nafuu ya mapema) na waliopoteza maisha wameshazikwa na kuacha simanzi, majonzi na maumivu kwenye familia, kwa ndugu jamaa hata marafiki. Natanguliza kuwapa pole sana katika kipindi hiki kigumu.

Ajali haina ratiba! Ajali hii ilitokea tayari mama akiwa na ratiba ya kusafiri nje ya nchi kikazi.. Kuahirisha pengine isingewezekana hivyo alifanya alipoweza na kuwaachia wa chini yake waendelee. Pamoja na lawama nyingi za kwanini taifa limepata tukio kama hilo na yeye ni kama hakuonesha kujali sana lakini mjadala mkubwa zaidi ukawa kwenye ishu nzima ya uokoaji. Vifaa duni, kuchelewa kufika eneo la tukio timu ya uokoaji, kutojali uzembe nknk.. Serikali ya CCM ikasakamwa kila kona. Kwahiyo ilibidi kutafutwa haraka matukio ya kuchepusha hii mijadala.

Haya ndio matukio mawili yenye kufikirisha maana yamepewa uzito mkubwa kuliko ajali yenyewe.

Tukio la kwanza ni MWOKOZI MAJALIWA. Huyu ni mvuvi anayesemekana ndio alifungua mlango wa ndege kwa kasia lake na kuingia ndani na kuanza kuokoa abiria waliokwama katikati ya taharuki ya ajali hakuna waliojishughulisha kuhoji uwezo wa kasia kuweza kufungua mlango wa ndege. Katikati ya taharuki hakuna aliyehoji ni nani walimwokoa Majaliwa aliyezirai na kukimbizwa hospital. Katikati ya taharuki hakuna aliyekuwa na muda wa kuhoji kama kuna wahudumu wa ndege wenye ujuzi waliokuwa wakisaidiana na watu wengine kuokoa abiria waliokwama.

Ni katikati ya taharuki hii ndio mvuvi Majaliwa akaokota dodo la bure.. Kwa kasi ya ajabu akatajwa kuwa ndiye aliyewaokoa abiria wale 24. Kwa kasi ya ajabu UVCCM wakampongeza. Kwa kasi ya ajabu PM akatangaza kumpatia nafasi kwenye jeshi la uokozi Tanzania. Kwa kasi ya ajabu akapatiwa na ulinzi na kutembezwa huku na kule. Kuna picha zikisemwa alialikwa bungeni na ikulu. Ghafla bin vuu mijadala mitandaoni ikawa ni juu ya Majaliwa na zile habari za lawama na udhaifu kwenye uokoaji zikapigwa kikumbo kikubwa sana.

Tukio la pili uzinduzi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita milion 70 kwa siku. Sambamba na ajali lakini wiki ile hali ilikuwa mbaya sana kwenye upatikanaji wa maji jijini. Mgao ulikuwa mkali kwakweli. Mbaya zaidi haikuwa maji tu bali na hata umeme hali haikuwa nzuri.

Pamoja na tukio la Majaliwa kukawa na matamko ya viongozi wa kisiasa kwamba kuna maji ya kigamboni yataingizwa Dar haraka kufidia upungufu. Mara likaandiwa tukio la kuzindua kisima cha kigamboni na mgeni rasmi akapangwa kuwa rais ambaye bado alikuwa nje ya nchi.

Kiukweli Kisima tajwa limezinduliwa kisiasa zaidi.. Kisima hiki kikubwa kiko barabara ya kuelekea Mwasonga, kiko kilometer mbili toka Kibada.. Kiuhalisia huu mradi haukupaswa kuzinduliwa sasa kwakuwa maji hayawafikii wateja kwa Bluetooth bali kwa kupitia mabomba. Kazi inayoendelea sasa ni kutandaza mabomba na kujenga sub stations. Maji bado hayajawafikia walaji. Kazi iliyopo baso ni kubwa si kazi ya wiki 2 au mwezi
Kisima husika kiko jirani kabisa na viwanda kama saba hivi vya wachina, ambao waliambiwa kuvifunga siku hiyo ya uzinduzi.

Mshangao ulikuwa juu ya mgeni rasmi na wingi wa waalikwa. Kwa uwazi walisema ule mradi si wa kumuita rais auzindue ilikuwa ni kazi ya waziri wa maji na hakukuwa na haja ya kualika umati wote ule wa watu.

Matukio haya mawili yamepita na pengine yamesaidia sana kuzipa mamlaka nafasi ya kupumua na kujipanga. Lakini sasa kuna ukweli mwingi unajidhihiri hasa kwenye ajali ile ya ndege. Abiria wale walionusurika ambao sasa kiwewe na taharuki vimewaisha na akili zao kukaa sawa wanashangazwa kumuona mitandaoni na ndani ya CCM akitajwa kama ndiye aliyewaokoa! Wana simulizi nyingine tofauti kabisa hasa wakiwataja mabinti wawili wahudumu kuwa ndio waliowaokoa.

Tamati yangu
Mamlaka ziliharakisha mno kumkweza Majaliwa ambaye hata hivyo naye aliokolewa na kujikuta hospital! Lakini bado hatujachelewa tuna nafasi bado ya kujirudi na kujisahihisha ili tuwatambue na kuwapa heshima zao wale walioongoza uokoaji. Wavuvi waliomuokoa Majaliwa. Wahudumu wa ndege wale mabinti wawili. Na wengine wote muhimu kwa nafasi zao kwa siku ile husika! Kuwabeza hawa wengine kuwa walikuwa wapi siku zote hakulisaidii taifa kwakuwa ukweli na uhalisia huwa havifichiki.
Ukweli wanaujua waliojaaliwa
 
Kwa hayo ulizungumza nakanusha inaonyesha yakua huna uchambuzi sahihi juu ya hili..

CHAMBUZI MAKINI JUU YA AJALI YA NDEGE ZIWA VICTORIA MWANZA.
1: Huenda wengi wetu tulibaki na taharuki kubwa baada ya ajali kutokea.
2: Vyombo vingi vya habari vimechangia kutopata taarifa kwa usahihi kulingana na uwasilishwaji wa taarifa.
3: Tukumbuke Tanzania haijawahi kutokea ajali ya ndege yenye kubeba abiri wengi au ndege yenye ukubwa kama hiyo iliyoanguka.
4: Vyombo na vikosi vya uokozi kutofanya kazi kwa ufanisi na kutofika eneo husika kwa wakati.
5: Asilimia ya mashuhuda wa tukio walitokea eneo la kanda ya ziwa na baadae kuwa waokoaji na watoa msaada kwa wahanga wa ajali.

KWA NINI MAJALIWA ALIPASWA KUPONGEZWA NA SERIKALI.
Huyu kijana alijitoa kwa asilimia 100% kwenye swala zima la uokoaji na ukisikiliza baadhi ya mahojiano alifanyiwa na baadhi ya media’s utakundua sio yeye alifungua mlango ila alisaidiana na yule mhudumu wa ndege, Kwani inasemekana kuwa mhudumu alikua akihangaika kufanya kila jitihada kuufungua mlango ukaunamshinda ila baada ya majaliwa kufika na wenzake akasogea kwenye mlango na kuanza kusaidiana na mhudumu kwa kuelewana yule dada aliusuma kuja nje yeye majaliwa anauvuta baada ya kupata mwanya kidogo aliomba kasia kwa mwenzie na kuanza kuugonga ule mlango kisha kuupachua kwakua ulikua umejiloki kwa ndani ghafla kwenye hizo jitihada mlango ulifunguka na hapo ndipo shughuli ya uokozi wa abiria kutoka ndani ya ndege ilipo anza kwa kuwatoa na kuwaweka kwenye ngalawa na kuwavusha ng’ambo wakati huo hayo yanaendelea ilikua ni kundi la majaliwa likifanya hivyo pamoja na majaaliwa mwenyewe, Kilichompa credits ni baada ya kuzirahi kwenye tukio lkn kama sio hivyo angekuwa amebaki kama wenzie tu kwa walifanya shughuli ya uokoaji pamoja na ilipofika taarifa kwa PM ni kunakijana aliefanya kitendo cha ushujaa cha kuokoa abiria kwenye ndege iliyopata ajali na anafanana jina na yeye hicho kilichokua kigezo kikubwa cha Majaliwa kuendelea kupata credits nyingine nyingi kutoka kwa MH. WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA.
Na kwa yule dada mhudumu wa ndege kwa upande wake nadhani huwa tunafahamu kwamba kila kampuni inayokuaji huwa kuna zawadi na tuzo mbalimbali hutolewa kwa mfanyakazi au wafanyakazi bora kila mwaka pale kampuni inapokua ikifanya sherehe zake kwa kuongeza mwaka mwingine hivyo huyu dada yeye credits zake atapewa na kampuni anafanyia kazi na hata ikiwezekana bodi ya usimamizi wa safari za anga Tanzania kumtunuku TUZO kwa ujasiri aliufanya kwenye hilo tukio.
Nimesoma bandiko lako lote nashindwa kujua unakanusha nini kwa nilichoandika na pia umechagua kipengele kimoja tuu kati ya mambo mengi niliyoandika hapa
 
Nimesoma bandiko lako lote nashindwa kujua unakanusha nini kwa nilichoandika na pia umechagua kipengele kimoja tuu kati ya mambo mengi niliyoandika hapa
Nimeona hizo nyingine ni prediction zako juu ya siasa ya Tanzania hivyo sikuona haja ya kuweka mchango wangu kwani huna uhakika na mengi ulizungumza..
 
Maisha ndivyo yalivyoo bahati ndo kitu pekee kakutana nacho majaliwa so mengine hata yasemwe vipi hakuna anaejua ukweli wa kilichotokea ila majaliwa hakuwa sehemu ya ajali lakini kwa jitihada zake akajikuta nae yupo hopsital kama vile MAGU alivyokuwa rais wakati hata form alilazimishwa kuchukua dakika za mwisho
 
Nimeona hizo nyingine ni prediction zako juu ya siasa ya Tanzania hivyo sikuona haja ya kuweka mchango wangu kwani huna uhakika na mengi ulizungumza..
Ok basi sawa hapo utakuwa hujalitendea haki hili andiko kwakuwa litakosa mtiririko sahihi sasa
 
Maisha ndivyo yalivyoo bahati ndo kitu pekee kakutana nacho majaliwa so mengine hata yasemwe vipi hakuna anaejua ukweli wa kilichotokea ila majaliwa hakuwa sehemu ya ajali lakini kwa jitihada zake akajikuta nae yupo hopsital kama vile MAGU alivyokuwa rais wakati hata form alilazimishwa kuchukua dakika za mwisho
kama vile MAGU alivyokuwa rais wakati hata form alilazimishwa kuchukua dakika za mwisho[emoji23]
 
Watu wawili walizidi kwenye ndege.

Abiria kutoka mbio kuelekea pasipo julikana.

Mtu kumzuia Majaliwa asivunje kioo.

Kasia kuvunja mlango wa ndege.

Majaliwa kujikuta hospitali.
 
Kama mnajua kwanini ajali ilitokea wekeni wazi, maswali yasiyo na majibu yamekua mengi sana.
 
Mimi kuna muda huwa najiuliza swali moja tu, hivi kuna uwezekano gani kasia kuvunja mlango wa ndege, katika utengenezaji wa ndege wapo makini zaidi katika usalama wa vijaa vyake, leo iwe rahisi tu mtu avunje mlango tena sio kwa kitu kizito bali wa kasia. Hapa ndio napopata mashaka, emergency door ulifunguliwe na mhudumu wa ndani na kuokoa hawa 24.
Ukiachilia mbali maajabu hayo sisemi kwasababu ya wivu hapana najaribu kwe na uhalisiaa binafsi najua hata mlango wa daladala kuupiga mpk ufunguke kwa kasiaa sio jambo rahisi lakini sasa utakuaje mlango wa ndege ufunguke na ninavojuaa mimi huenda mlango wa ndege ni imara zaidi kwasababu ndege inapaa hewan kwaio ile forces of gravity ni kubwa na huenda mlango umetengenezwa kwa ubora mkubwa zaidi kwaio sio rahisi jambo la tatu ni kwamba mlango ule unaonekana umefunguliwa na haujabondeka wala kupasuka je majaliwa yeye alivunjaaa waaaap?
 
Mimi kuna muda huwa najiuliza swali moja tu, hivi kuna uwezekano gani kasia kuvunja mlango wa ndege, katika utengenezaji wa ndege wapo makini zaidi katika usalama wa vijaa vyake, leo iwe rahisi tu mtu avunje mlango tena sio kwa kitu kizito bali wa kasia. Hapa ndio napopata mashaka, emergency door ulifunguliwe na mhudumu wa ndani na kuokoa hawa 24.
Ndege ilishaangukia majini.. sio kila kitu kitakuwa kama mwanzo. pengine ulipinda ukafunguka wenyewe......,
 
Kutoka kerebe kisiwani mpaka bukoba leo kuja kuona na mimi hiyo ndege. Yaani niko bukoba na nimeiona muda si mrefu. Kama ule mlango wa nyuma ndo mlango wa dharura basi hauna hali ya kubondwabondwa.

Upande wa mbele wameifunika turubari na wima wa mlango wa abiria napo kuna turubari, kuhusu kasia ya kawaida kabisa ya mtumbwi wa kasia basi uzito wake hauzidi kilo tatu.

Kasia huwa zinapiga tu hata mtu zinavunjika hivyo haiwezi bomoa mlango wata wa passo sijui uimara wa mlango wa ndege ila kama unafika hata uimara wa mlango tu wa kirikuu basi kasia haitofua dafu.
Mkuu uimara wa mlango wa ndege sio wa kitoto...
Kwa tuliotumia usafiri huu sio rahisi kunidanganya eti kasia lilifungua mlango kwa kuugonga. Never
 
Kwa hayo ulizungumza nakanusha inaonyesha yakua huna uchambuzi sahihi juu ya hili..

CHAMBUZI MAKINI JUU YA AJALI YA NDEGE ZIWA VICTORIA MWANZA.
1: Huenda wengi wetu tulibaki na taharuki kubwa baada ya ajali kutokea.
2: Vyombo vingi vya habari vimechangia kutopata taarifa kwa usahihi kulingana na uwasilishwaji wa taarifa.
3: Tukumbuke Tanzania haijawahi kutokea ajali ya ndege yenye kubeba abiri wengi au ndege yenye ukubwa kama hiyo iliyoanguka.
4: Vyombo na vikosi vya uokozi kutofanya kazi kwa ufanisi na kutofika eneo husika kwa wakati.
5: Asilimia ya mashuhuda wa tukio walitokea eneo la kanda ya ziwa na baadae kuwa waokoaji na watoa msaada kwa wahanga wa ajali.

KWA NINI MAJALIWA ALIPASWA KUPONGEZWA NA SERIKALI.
Huyu kijana alijitoa kwa asilimia 100% kwenye swala zima la uokoaji na ukisikiliza baadhi ya mahojiano alifanyiwa na baadhi ya media’s utakundua sio yeye alifungua mlango ila alisaidiana na yule mhudumu wa ndege, Kwani inasemekana kuwa mhudumu alikua akihangaika kufanya kila jitihada kuufungua mlango ukaunamshinda ila baada ya majaliwa kufika na wenzake akasogea kwenye mlango na kuanza kusaidiana na mhudumu kwa kuelewana yule dada aliusuma kuja nje yeye majaliwa anauvuta baada ya kupata mwanya kidogo aliomba kasia kwa mwenzie na kuanza kuugonga ule mlango kisha kuupachua kwakua ulikua umejiloki kwa ndani ghafla kwenye hizo jitihada mlango ulifunguka na hapo ndipo shughuli ya uokozi wa abiria kutoka ndani ya ndege ilipo anza kwa kuwatoa na kuwaweka kwenye ngalawa na kuwavusha ng’ambo wakati huo hayo yanaendelea ilikua ni kundi la majaliwa likifanya hivyo pamoja na majaaliwa mwenyewe, Kilichompa credits ni baada ya kuzirahi kwenye tukio lkn kama sio hivyo angekuwa amebaki kama wenzie tu kwa walifanya shughuli ya uokoaji pamoja na ilipofika taarifa kwa PM ni kunakijana aliefanya kitendo cha ushujaa cha kuokoa abiria kwenye ndege iliyopata ajali na anafanana jina na yeye hicho kilichokua kigezo kikubwa cha Majaliwa kuendelea kupata credits nyingine nyingi kutoka kwa MH. WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA.
Na kwa yule dada mhudumu wa ndege kwa upande wake nadhani huwa tunafahamu kwamba kila kampuni inayokuaji huwa kuna zawadi na tuzo mbalimbali hutolewa kwa mfanyakazi au wafanyakazi bora kila mwaka pale kampuni inapokua ikifanya sherehe zake kwa kuongeza mwaka mwingine hivyo huyu dada yeye credits zake atapewa na kampuni anafanyia kazi na hata ikiwezekana bodi ya usimamizi wa safari za anga Tanzania kumtunuku TUZO kwa ujasiri aliufanya kwenye hilo tukio.
Sawasawa.......
 
Mkuu uimara wa mlango wa ndege sio wa kitoto...
Kwa tuliotumia usafiri huu sio rahisi kunidanganya eti kasia lilifungua mlango kwa kuugonga. Never
JamiiForums-1849398848.jpg
 
Back
Top Bottom