Mjadala mpya: Ni nani aliwaokoa abiria 24 wa ndege ya Precision Air?

Hivi ule mlango wa ndege upigwe na kasia la mbao ufunguke hamna nakata mpaka mwisho ni kitu hakiwezekani
 
Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi, majeruhi na vifo kama habari husika inahusika na ajali, uharibifu mwingine huja mwishoni.. Na hapo katikati ya tarahuki kuna mengi hutokea ya ukweli ya kuzusha na ya uongo pia.. Na kuna wakati kuna kikundi ama vikundi ndio hufanya haya kwasababu zozote zile.

Taharuki ikishakoma, kuna ukweli na uhalisia ambao haukusemwa kabla hujifunua taratibu. Maana uongo hupanda lift na kufika haraka lakini ukweli hukwea ngazi na kufika mwishoni.

Ajali ya ndege ya Precision iliyotokea pale Bukoba na kuondoka na roho za watanzania 19 nayo imepitia mlolongo huo huo. Sasa hali imetulia, waliosalimika wamesalimika, majeruhi wanaendelea na matibabu (tunawaombea nafuu ya mapema) na waliopoteza maisha wameshazikwa na kuacha simanzi, majonzi na maumivu kwenye familia, kwa ndugu jamaa hata marafiki. Natanguliza kuwapa pole sana katika kipindi hiki kigumu.

Ajali haina ratiba! Ajali hii ilitokea tayari mama akiwa na ratiba ya kusafiri nje ya nchi kikazi.. Kuahirisha pengine isingewezekana hivyo alifanya alipoweza na kuwaachia wa chini yake waendelee. Pamoja na lawama nyingi za kwanini taifa limepata tukio kama hilo na yeye ni kama hakuonesha kujali sana lakini mjadala mkubwa zaidi ukawa kwenye ishu nzima ya uokoaji. Vifaa duni, kuchelewa kufika eneo la tukio timu ya uokoaji, kutojali uzembe nknk.. Serikali ya CCM ikasakamwa kila kona. Kwahiyo ilibidi kutafutwa haraka matukio ya kuchepusha hii mijadala.

Haya ndio matukio mawili yenye kufikirisha maana yamepewa uzito mkubwa kuliko ajali yenyewe.

Tukio la kwanza ni MWOKOZI MAJALIWA. Huyu ni mvuvi anayesemekana ndio alifungua mlango wa ndege kwa kasia lake na kuingia ndani na kuanza kuokoa abiria waliokwama katikati ya taharuki ya ajali hakuna waliojishughulisha kuhoji uwezo wa kasia kuweza kufungua mlango wa ndege. Katikati ya taharuki hakuna aliyehoji ni nani walimwokoa Majaliwa aliyezirai na kukimbizwa hospital. Katikati ya taharuki hakuna aliyekuwa na muda wa kuhoji kama kuna wahudumu wa ndege wenye ujuzi waliokuwa wakisaidiana na watu wengine kuokoa abiria waliokwama.

Ni katikati ya taharuki hii ndio mvuvi Majaliwa akaokota dodo la bure.. Kwa kasi ya ajabu akatajwa kuwa ndiye aliyewaokoa abiria wale 24. Kwa kasi ya ajabu UVCCM wakampongeza. Kwa kasi ya ajabu PM akatangaza kumpatia nafasi kwenye jeshi la uokozi Tanzania. Kwa kasi ya ajabu akapatiwa na ulinzi na kutembezwa huku na kule. Kuna picha zikisemwa alialikwa bungeni na ikulu. Ghafla bin vuu mijadala mitandaoni ikawa ni juu ya Majaliwa na zile habari za lawama na udhaifu kwenye uokoaji zikapigwa kikumbo kikubwa sana.

Tukio la pili uzinduzi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita milion 70 kwa siku. Sambamba na ajali lakini wiki ile hali ilikuwa mbaya sana kwenye upatikanaji wa maji jijini. Mgao ulikuwa mkali kwakweli. Mbaya zaidi haikuwa maji tu bali na hata umeme hali haikuwa nzuri.

Pamoja na tukio la Majaliwa kukawa na matamko ya viongozi wa kisiasa kwamba kuna maji ya kigamboni yataingizwa Dar haraka kufidia upungufu. Mara likaandiwa tukio la kuzindua kisima cha kigamboni na mgeni rasmi akapangwa kuwa rais ambaye bado alikuwa nje ya nchi.

Kiukweli Kisima tajwa limezinduliwa kisiasa zaidi.. Kisima hiki kikubwa kiko barabara ya kuelekea Mwasonga, kiko kilometer mbili toka Kibada.. Kiuhalisia huu mradi haukupaswa kuzinduliwa sasa kwakuwa maji hayawafikii wateja kwa Bluetooth bali kwa kupitia mabomba. Kazi inayoendelea sasa ni kutandaza mabomba na kujenga sub stations. Maji bado hayajawafikia walaji. Kazi iliyopo baso ni kubwa si kazi ya wiki 2 au mwezi
Kisima husika kiko jirani kabisa na viwanda kama saba hivi vya wachina, ambao waliambiwa kuvifunga siku hiyo ya uzinduzi.

Mshangao ulikuwa juu ya mgeni rasmi na wingi wa waalikwa. Kwa uwazi walisema ule mradi si wa kumuita rais auzindue ilikuwa ni kazi ya waziri wa maji na hakukuwa na haja ya kualika umati wote ule wa watu.

Matukio haya mawili yamepita na pengine yamesaidia sana kuzipa mamlaka nafasi ya kupumua na kujipanga. Lakini sasa kuna ukweli mwingi unajidhihiri hasa kwenye ajali ile ya ndege. Abiria wale walionusurika ambao sasa kiwewe na taharuki vimewaisha na akili zao kukaa sawa wanashangazwa kumuona mitandaoni na ndani ya CCM akitajwa kama ndiye aliyewaokoa! Wana simulizi nyingine tofauti kabisa hasa wakiwataja mabinti wawili wahudumu kuwa ndio waliowaokoa.

Tamati yangu
Mamlaka ziliharakisha mno kumkweza Majaliwa ambaye hata hivyo naye aliokolewa na kujikuta hospital! Lakini bado hatujachelewa tuna nafasi bado ya kujirudi na kujisahihisha ili tuwatambue na kuwapa heshima zao wale walioongoza uokoaji. Wavuvi waliomuokoa Majaliwa. Wahudumu wa ndege wale mabinti wawili. Na wengine wote muhimu kwa nafasi zao kwa siku ile husika! Kuwabeza hawa wengine kuwa walikuwa wapi siku zote hakulisaidii taifa kwakuwa ukweli na uhalisia huwa havifichiki.
Kimeumana!😀
 
Sie ambao hatujakiwepo eneo la tukio n ngumu kumjua aliye fungua mlango, na kama kuna mtu aliyetoka na kuanza kukimbiakimbia ovyo pengine hata waliokuwepo kwenye ndege nao wanaweza kuwa wanamjua au wanadhania kuwa wanamjua kumbe hawamjui sababu katika hali ile huenda akili zao Kwa wakati huo hazikuwa sawa.
 
Mkuu Mshana, kama Majaliwa hajahusika kuwaokoa wahanga wa precision tujiulize haya:-

1. Kwamba alipangwa ili azungumze uongo? Kama jibu ni ndio hatuwezi kumdondoa ili kufahamu uwezo wake katika propaganda.

2. Abiria (manusura) ambao waliwepo kwenye ndege hawana kumbukumbu yoyote kuhusu Majaliwa katika uokoaji?
 
Hatuwezi kamwe kumkana Majaliwa kwenye uokoaji na tukisema kwamba alipangwa kucheza muvi tutakuwa hatuna akili na tunaweza kuitwa wazushi wa aina yake! Majaliwa na waokoaji wengine walifanya walichofanya mpaka wakasalimika abiria 24
Kilichotokea ni kwamba kuna kikundi cha watu kwa sababu zao wenyewe wakaamua kutembea na bit ya Majaliwa na kuipa verse za kutosha kisha wakaipromote pakubwa
 
Wizara ya Afya imeendelea kuboresha mikakati ya kuokoa maisha ya watu kutokana na majanga na ajali kwa kuanzisha Kitengo mahsusi kitakachoshughulika na kuokoa maisha ya watu kutokana na ajali.' Kitengo kipya cha majanga ajali kushughulika katika kuokoa maisha ya watu
E21423B0-4F99-4FE8-BABC-A7D1543ED3C6.jpeg

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alipowatembelea majeruhi wa ajali iliyohusisha Basi la Arusha Express kugongana na Lori eneo la Mzakwe, Dodoma.
 
Mkuu Mshana, kama Majaliwa hajahusika kuwaokoa wahanga wa precision tujiulize haya:-

1. Kwamba alipangwa ili azungumze uongo? Kama jibu ni ndio hatuwezi kumdondoa ili kufahamu uwezo wake katika propaganda.

2. Abiria (manusura) ambao waliwepo kwenye ndege hawana kumbukumbu yoyote kuhusu Majaliwa katika uokoaji?
2. Abiria (manusura) ambao waliwepo kwenye ndege hawana kumbukumbu yoyote kuhusu Majaliwa katika uokoaji[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Eng Victor amesema baada ya Ndege ya Precision Air kuanguka alijaribu mara 3 kufungua mlango Bila mafanikio ndipo akaja Muhudumu wa Ndege na kubonyeza mahali mlango ukafunguka

Victor anasema muda wote wa Uokoaji alikuwa ameuzuia mlango kwa mkono takribani Dakika 40-60 na baada ya kuhakikisha Watu wote wametoka aliuachia mlango Ukajifunga kwa sababu ni wa hydroulic

Kabla sijauachia mlango nilimtuma mvuvi mmoja " mdogo mdogo hivi" aokoe mabegi yanayoelea ndani ya Ndege na anitafutie na begi langu lakini begi langu hakuliona

Victor anasema anajisikia maumivu ya hapa na pale na amekubaliana na madaktari wa Bukoba aende Muhimbili kwa Uchunguzi zaidi

Victor anasema Wavuvi wote walimfata na kumkumbatia baada ya zoezi la uokoaji kukamilika naye aliwaambia Nguvu walizomuona nazo kule kwenye Maji siyo zake bali ni muujiza wa Mungu.

Victor alihojiwa na Wasafi tv akiwa ndani ya Ndege ya Precision Air alirejea DSM tayari kwenda Muhimbili

Source: WASAFI TV
 
Kila jambo huanza na tetesi, tetesi ikithibitishwa huwa breaking news.. Breaking news ndio huleta taharuki hasa kwenye uokozi, majeruhi na vifo kama habari husika inahusika na ajali, uharibifu mwingine huja mwishoni.. Na hapo katikati ya tarahuki kuna mengi hutokea ya ukweli ya kuzusha na ya uongo pia.. Na kuna wakati kuna kikundi ama vikundi ndio hufanya haya kwasababu zozote zile.

Taharuki ikishakoma, kuna ukweli na uhalisia ambao haukusemwa kabla hujifunua taratibu. Maana uongo hupanda lift na kufika haraka lakini ukweli hukwea ngazi na kufika mwishoni.

Ajali ya ndege ya Precision iliyotokea pale Bukoba na kuondoka na roho za watanzania 19 nayo imepitia mlolongo huo huo. Sasa hali imetulia, waliosalimika wamesalimika, majeruhi wanaendelea na matibabu (tunawaombea nafuu ya mapema) na waliopoteza maisha wameshazikwa na kuacha simanzi, majonzi na maumivu kwenye familia, kwa ndugu jamaa hata marafiki. Natanguliza kuwapa pole sana katika kipindi hiki kigumu.

Ajali haina ratiba! Ajali hii ilitokea tayari mama akiwa na ratiba ya kusafiri nje ya nchi kikazi.. Kuahirisha pengine isingewezekana hivyo alifanya alipoweza na kuwaachia wa chini yake waendelee. Pamoja na lawama nyingi za kwanini taifa limepata tukio kama hilo na yeye ni kama hakuonesha kujali sana lakini mjadala mkubwa zaidi ukawa kwenye ishu nzima ya uokoaji. Vifaa duni, kuchelewa kufika eneo la tukio timu ya uokoaji, kutojali uzembe nknk.. Serikali ya CCM ikasakamwa kila kona. Kwahiyo ilibidi kutafutwa haraka matukio ya kuchepusha hii mijadala.

Haya ndio matukio mawili yenye kufikirisha maana yamepewa uzito mkubwa kuliko ajali yenyewe.

Tukio la kwanza ni MWOKOZI MAJALIWA. Huyu ni mvuvi anayesemekana ndio alifungua mlango wa ndege kwa kasia lake na kuingia ndani na kuanza kuokoa abiria waliokwama katikati ya taharuki ya ajali hakuna waliojishughulisha kuhoji uwezo wa kasia kuweza kufungua mlango wa ndege. Katikati ya taharuki hakuna aliyehoji ni nani walimwokoa Majaliwa aliyezirai na kukimbizwa hospital. Katikati ya taharuki hakuna aliyekuwa na muda wa kuhoji kama kuna wahudumu wa ndege wenye ujuzi waliokuwa wakisaidiana na watu wengine kuokoa abiria waliokwama.

Ni katikati ya taharuki hii ndio mvuvi Majaliwa akaokota dodo la bure.. Kwa kasi ya ajabu akatajwa kuwa ndiye aliyewaokoa abiria wale 24. Kwa kasi ya ajabu UVCCM wakampongeza. Kwa kasi ya ajabu PM akatangaza kumpatia nafasi kwenye jeshi la uokozi Tanzania. Kwa kasi ya ajabu akapatiwa na ulinzi na kutembezwa huku na kule. Kuna picha zikisemwa alialikwa bungeni na ikulu. Ghafla bin vuu mijadala mitandaoni ikawa ni juu ya Majaliwa na zile habari za lawama na udhaifu kwenye uokoaji zikapigwa kikumbo kikubwa sana.

Tukio la pili uzinduzi wa kisima cha maji chenye uwezo wa kutoa lita milion 70 kwa siku. Sambamba na ajali lakini wiki ile hali ilikuwa mbaya sana kwenye upatikanaji wa maji jijini. Mgao ulikuwa mkali kwakweli. Mbaya zaidi haikuwa maji tu bali na hata umeme hali haikuwa nzuri.

Pamoja na tukio la Majaliwa kukawa na matamko ya viongozi wa kisiasa kwamba kuna maji ya kigamboni yataingizwa Dar haraka kufidia upungufu. Mara likaandiwa tukio la kuzindua kisima cha kigamboni na mgeni rasmi akapangwa kuwa rais ambaye bado alikuwa nje ya nchi.

Kiukweli Kisima tajwa limezinduliwa kisiasa zaidi.. Kisima hiki kikubwa kiko barabara ya kuelekea Mwasonga, kiko kilometer mbili toka Kibada.. Kiuhalisia huu mradi haukupaswa kuzinduliwa sasa kwakuwa maji hayawafikii wateja kwa Bluetooth bali kwa kupitia mabomba. Kazi inayoendelea sasa ni kutandaza mabomba na kujenga sub stations. Maji bado hayajawafikia walaji. Kazi iliyopo baso ni kubwa si kazi ya wiki 2 au mwezi
Kisima husika kiko jirani kabisa na viwanda kama saba hivi vya wachina, ambao waliambiwa kuvifunga siku hiyo ya uzinduzi.

Mshangao ulikuwa juu ya mgeni rasmi na wingi wa waalikwa. Kwa uwazi walisema ule mradi si wa kumuita rais auzindue ilikuwa ni kazi ya waziri wa maji na hakukuwa na haja ya kualika umati wote ule wa watu.

Matukio haya mawili yamepita na pengine yamesaidia sana kuzipa mamlaka nafasi ya kupumua na kujipanga. Lakini sasa kuna ukweli mwingi unajidhihiri hasa kwenye ajali ile ya ndege. Abiria wale walionusurika ambao sasa kiwewe na taharuki vimewaisha na akili zao kukaa sawa wanashangazwa kumuona mitandaoni na ndani ya CCM akitajwa kama ndiye aliyewaokoa! Wana simulizi nyingine tofauti kabisa hasa wakiwataja mabinti wawili wahudumu kuwa ndio waliowaokoa.

Tamati yangu
Mamlaka ziliharakisha mno kumkweza Majaliwa ambaye hata hivyo naye aliokolewa na kujikuta hospital! Lakini bado hatujachelewa tuna nafasi bado ya kujirudi na kujisahihisha ili tuwatambue na kuwapa heshima zao wale walioongoza uokoaji. Wavuvi waliomuokoa Majaliwa. Wahudumu wa ndege wale mabinti wawili. Na wengine wote muhimu kwa nafasi zao kwa siku ile husika! Kuwabeza hawa wengine kuwa walikuwa wapi siku zote hakulisaidii taifa kwakuwa ukweli na uhalisia huwa havifichiki.
Mkuu Mshana ukweli ulio wazi nikwamba you can not operate any system in the aircraft including opening emergency exit which are hydrological operating if engines are already not operating unless if yes what happened is miracle
 
Sasa n niNI kilifungua mlango ni Kasia(mwiko) au jiwe la fatuma

Huyu Kijana tena Wajina wangu Majaliwa Jackson ni Shujaa kweli na lazima tumpe Asante kwani Yeye ndiyo alienda ilipo Ndege na kwa Kutumia Makasia aliyokuwa nayo akafungua Mlango wa Ndege na peke yake Kuokoa Abiria wote" Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.
 
Hatuwezi kamwe kumkana Majaliwa kwenye uokoaji na tukisema kwamba alipangwa kucheza muvi tutakuwa hatuna akili na tunaweza kuitwa wazushi wa aina yake! Majaliwa na waokoaji wengine walifanya walichofanya mpaka wakasalimika abiria 24
Kilichotokea ni kwamba kuna kikundi cha watu kwa sababu zao wenyewe wakaamua kutembea na bit ya Majaliwa na kuipa verse za kutosha kisha wakaipromote pakubwa
Kwa mantiki hiyo ni kwamba mlango haukufunguliwa na kasia!!!

Kama ni hivyo kwa nini Majaliwa ndiye staring wa movie yetu (kama kweli ni movie).?

Je, ana capacity hiyo ya kuwa staring au amepandishwa juu ya mti?
 
Kuna kitu kinaitwa nyenzo ... Hiki hukusaidia kurahisisha kazi ambayo ungeifanya kwa ugumu! Ngazi huwa ni nyenzo muhimu sana ya kukupeleka juu
 
2. Abiria (manusura) ambao waliwepo kwenye ndege hawana kumbukumbu yoyote kuhusu Majaliwa katika uokoaji[emoji1541][emoji1541][emoji1541]

Eng Victor amesema baada ya Ndege ya Precision Air kuanguka alijaribu mara 3 kufungua mlango Bila mafanikio ndipo akaja Muhudumu wa Ndege na kubonyeza mahali mlango ukafunguka

Victor anasema muda wote wa Uokoaji alikuwa ameuzuia mlango kwa mkono takribani Dakika 40-60 na baada ya kuhakikisha Watu wote wametoka aliuachia mlango Ukajifunga kwa sababu ni wa hydroulic

Kabla sijauachia mlango nilimtuma mvuvi mmoja " mdogo mdogo hivi" aokoe mabegi yanayoelea ndani ya Ndege na anitafutie na begi langu lakini begi langu hakuliona

Victor anasema anajisikia maumivu ya hapa na pale na amekubaliana na madaktari wa Bukoba aende Muhimbili kwa Uchunguzi zaidi

Victor anasema Wavuvi wote walimfata na kumkumbatia baada ya zoezi la uokoaji kukamilika naye aliwaambia Nguvu walizomuona nazo kule kwenye Maji siyo zake bali ni muujiza wa Mungu.

Victor alihojiwa na Wasafi tv akiwa ndani ya Ndege ya Precision Air alirejea DSM tayari kwenda Muhimbili

Source: WASAFI TV
"Kabla sijauachia mlango nilimtuma mvuvi mmoja mdogo mdogo hivi"
Je, hapa ndo chanzo cha ushujaa wa Majaliwa?
Kwamba yeye alitumwa kwa jambo dogo kutoka jambo kubwa!!!

Mshana hebu tumuachie dogo naye akafaidi mema ya nchi.
 
Nimenukuu sio maandishi yangu na wala sina wivu na Majaliwa ila ni lazima ukweli usemwe
 
Nimekuelewa sana mkuu pia nafahamu kwamba huna roho ya (kilingeni kwa sasa - jocking) na siyo vibaya kureason.

Hata hivyo kama amepandishwa juu tumuache naye ale matunda ya nchi yetu usije onekana mchoyo na mchochezi.
 
Namuombea sana ila nina hofu yasije kumkuta kama ualiyowakuta kina Piere liquid
 
HII nchi Jamani....Lakini tuwaze tu hivi inawezekana mlango wa ndege ukawa sawa na wa Toyota allex ukipigwa Kasia unasambaratika......!
Only in bongo salidalamu
 
Back
Top Bottom