MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

mbona wapo wengi mkuu wa 27-34 ambao hawajaolewa na hawana watoto kama uchaguzi wako ulivyo.
kuchagua sana sio tatizo, tatizo ni kuchagua bila kuwa na standards, weka viwango vyako vioivyohalisi chagua mwenye afadhali.
Maisha hwyasubiri, wengi huoa nusu wakqmilifu kama wao walivyo nusu wakamilifu. hizo nusu mbili ndio zinafanya ndoa kamilifu mkuu.

ila hata hao uliowwtaja kama wadogo sana ukikuta kaivishwa vizuri na wazazi ni bora sana tena saana
Message delivered. Received.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Habari za jumatatu. Ni changamoto gani unazipata katika harakati za kutafuta mke kama wewe ni wale waliochelewa kuoa. Kwa mtazamo wa jamii zetu za kiTz mwanaume au mwanamke aliezidi miaka 35 hajaoa au kuolewa ni kuwa amechelewa. Hii sio sheria mwingine anaweza kuwa na mtazamo tofauti.

Mimi binafsi changamoto ninazopata ni hizi

1.Umri-wanawake wengi kwenye jamii zetu ambao hawajaolewa umri wao ni 22-26. Kwangu mimi bado wadogo yaani tofauti ya umri naiona kubwa.

2.Siko tayari kuoa mwanamke mwenye mtoto-naomba nisieleweke vibaya, huu ni msimamo tu nimeamua hivy. Changamoto kubwa sasa ni kuwa wale ambao naona ndio umri sahihi wa kuolewa na mimi wengi wao wana mtoto/watoto

3.Nachagua sana (Naambiwa hivyo inabidi nikubali)-kuoa bila kuchagua inawezekana kweli? Huyu ni mtu nitakaekuwa nae kwa maisha yangu yote sasa inabidi nipate mtu nilieridhika nae.

Tuchangie thread hii kwa lengo la kusaidiana,kurekebisha na kushauria.
Kijana kuna kitu unamiss siku hizi naona, nakumbuka ule uzi wako mtoto wa maid anakupenda sana, na ule wa umekua mkubwa, saa nne usiku uko nyumbani licha ya kwamba hela ipo!
Taratiiibu!!
 
Binti wa miaka 22-26 mbona ni mkubwa kabisa kwa kuoa Ila inategemea na mazingira aliyokuwa anaishi ndo yanaweza kumfanya awe mwanamke bora hvy umri huo pia c mbaya

Kuoa mwanamke asiye na mtoto Kama ndo msimamo wako Sawa ni bora ili uishi kwa amani zaid

Aisee punguza kuchagua kaka yangu(kuchamba kwingi kutoka na mavi)Angalia chenye afadhali bac
Kikwazo tofauti ya umri.
 
Kijana kuna kitu unamiss siku hizi naona, nakumbuka ule uzi wako mtoto wa maid anakupenda sana, na ule wa umekua mkubwa, saa nne usiku uko nyumbani licha ya kwamba hela ipo!
Taratiiibu!!
Ha ha ha ha ile ni akili ya weekend mkuu....
 
Mimi cha kwanza sitaki kuolewa na mwanaume mwenye mtoto we mungu nisaidie,
--sitaki kuolewa na mwanaume chini ya miaka 27
--sitaki kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma ee mungu nisaidie.....

Lkn bado sijaona sababu ya mimi kuolewa coz kwangu siyo lazimaa
 
hii tafiti uliifanyia wapi ?
Nina zaidi ya milongo miwili katika hii dunia tangu nimepevuka, nimeishi mikoa karibia yote hapa nchini zaidi ya hapo nimewahi kuishi mpaka nchi jirani yaani Kenya na Mozambique, nimekutana na watu kibao wenye umri mkubwa waliochelewa kuoa na kuolewa na kujionea wanayokutana nayo kwenye mahusiano.

Kwa hiyo siwezi kukwambia nimefanyia wapi tafiti yangu isipokuwa life experience niliyonayo inatosha kabisa kunifanya mimi nije hilo hitimisho kama ukivyo ona hapo
 
Mimi cha kwanza sitaki kuolewa na mwanaume mwenye mtoto we mungu nisaidie,
--sitaki kuolewa na mwanaume chini ya miaka 27
--sitaki kuolewa na mwanaume ambaye hajasoma ee mungu nisaidie.....

Lkn bado sijaona sababu ya mimi kuolewa coz kwangu siyo lazimaa

[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nilitaka kusema the same nikaogopa kushushuliwa[emoji85] [emoji85] [emoji85]
Kwa thread ninazoandika lately i expected this. Siwezi kushangaa mtu kusema hivyo, hata ningekuwa mimi ningemfikiria huyo mtu hivyo. ila trust me naandika makusudi, lately hamna thread za aina hii.
 
Back
Top Bottom