Nenda hispital utapata ushauri murua kabisa. Na watajua ni njia gan ya kukusaidia. Kama meno yame oza kabisa wata ng'oa ila kama yameathirika kidogo. Watakusafisha na kuziba yaliyo toboka. Pesa yako tu
Brother, hujawahi kwenda hospitali kwa tiba ya meno ukayaona yale mapatasi ya kungolea? au unaongea tuu kiurahisi kama ule usemi " uwe unapenda kwenda kucheki afya yako hospitalini hata kama huumwi , ukifika kule unakuta wagojwa wamejaaa, sasa docta atakuhudumia wewe mzima au wale wagojwa ambao hawajapata hata nafasi kwa wingi wao?''
Madaktari wa meno wanasoma muda mwingi tena nasikia wakishamaliza kozi ya udactari wa kawaida wanaoneza miaka mingine ya kulisomea jino, sasa inakuwaje hawajapata suluisho la kudumu?mbona ni kungoa tuu, na madaktari wa macho, pua, wangekuwa hivyo tungekuwaje? kama ni kungoa tuu kwa nini kozi isitolewe tuu VETA?
Uzibaji wa meno, uwe wanaoita wa muda au wa kudumu bado haujaleta suluhu.
Meno ya badia baada ya kungoa meno bado hakuna yaliyopatikana kumsaidia huyu kibohgoyo, haya ya kuweka na kutoa kula huwezi, kuongea ni kuchezesha ulimi tuu.
Haya wanayosema wanayagandisha kwenye fizi ni hatari tupu, ukiyatafunia yanaenda kukgusa mishipa ya fahamu....maumivu utakayoyapata.......omera utatamani uyapige ngumi yasambaratike.
Nashauri, madactari wa sekta hii waongeze juhudi kufanya utafiti kuliondoa hili tataizo sugu ambalo linaweza kushababisha idadi ya vibogoyo kuongezeka kwa kasi.