Mjadala: Ni ipi dawa ya kutibu maumivu ya jino bila kung'oa?

Salaam JF,

Nimeleta uzi huu kwenu nikijaribu kupata ushauri kwa wataalamu au watu ambao mlipitia hali hii ya maumivu makali ya meno, je mlitatua vp hali hizo?

Nina mdogo wangu anasumbuliwa sana, yaani mno na maumivu ya meno. Ameshawahi Kung'oa baadhi, na ameshaenda hospital na kutumia dawa kadhaa. Lakini hali hii imekuwa ikijirudia kwake.

Siku mbili zilizopita ameumwa usiku kucha bila kulala kwa maumivu ya jino/gego ambalo kwa nje hata halijatoboka, namuonea huruma kwa jinsi anavyoteseka.

Kwa mwenye kufahamu dawa, daktari, ushauri wa kadhia hii ushauri wenu ni wathamani, kabla ya kufikiria Kung'oa.

Ahsanteni
 
Dawa za hospitali zipo japo sijawahi kuzitumia binafsi.

Ila kwa kienyeji kuna dawa moja matata sana inaitwa, mgomba.

Unachukua kipande cha mgomba, wengi wanapendelea mzizi wake au hata lile danda la ndani lenye unyevu nyevu, unaliweka kwenye moto kidogo, dhen likianza kuungua yale maji maji unayachukua unayaweka kwenye jino linalouma.

Baada ya muda, maumivu yatakata na utasahau milele yote.
 
Jino kuuma ni kuwa limetoboka au Lina maambukizi (Infection). Ingawa halijatoboka inawezekana Infection imeingia kutoka jino la pili.
Nenda kwa dentist anaweza kukupa antibiotics na uchauri zaidi.

Akumbuke kusafisha meno kila baada ya kula
Kabla hajalala na asubuhi akiamka.
 
Umenikumbsha mbali sana... ILA DAWA YA JINO NI KULITOA!! kabla ya Kulitoa apige x-ray wajue Kam Kuna tatizo lingine!!
 
Nawasalimu Wote kwa Pamoja.

Habari Zenu?

Bila kupoteza Musa Kuna mdau wangu wa karibu Sana meno yake yanamsumbua keshatoa Moja na juzi kaenda kutoa lingine kwa Bahati mbaya Doctor akakosea akatoa zima akaliacha Bovu linalostahili kutolewa.

Kwa Hiyo mpaka sasa anapata maumivu makali kutokana ubovu wake.

Meno yake haya ufa ila yanauma tu hivo naomba Msaada wa jina la Dawa na Mahali pa kupata Spea zake.

Ahsanteni Sana.

Makanya Mtoto
 

Kinondon sehem gani namie niende kesho alfajiri? Nateseka sana kaka. Gego la mwisho limetoboka halaf linauma kweli
 
Kuna lile jani ambalo inasemekana kutibu corona, kwa kichaga wanaita iyombo au ilaka, chukua jani lake lichomeke kwenye majivu ya moto, likishapata joto tafunia pale kwenye jino linalouma asubuhi na jioni siku 3 halafu ulete mrejesho. NB :mimi nilitumia nilipona kabisa. Usiku mwema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasumbuliwa na tatizo la jino/meno kuuma.
Huna haja ya kung'oa jino lako.

Dawa hii ina ufanisi wa [emoji817] katika kuondosha na kumaliza tatizo la maumivu ya jino/meno.

Mahitaji
1. Mafuta ya karafuu/clove oil.
2. mafuta ya Nazi/coconut oil.
3. Kitunguu maji.
4. Kitunguu swaum.
5. Pilipili manga.
6.Chumvi ya mawe/unga wake

MAANDALIZI
Ponda ponda Kitunguu maji,Kitunguu swaumu,chumvi ya mawe na pilipili manga kisha changanya na mafuta na Nazi na mafuta ya karafuu kwa kiasi kidogo (robo kijiko kidogo cha chai) kisha chukua mchanganyiko huu kisha uweke juani kwa muda wa dakika 15 kisha toa juani

MATUMIZI
1.ikiwa jino lina tundu
chukua uji uji wa mchanganyiko huu kisha weka katika tundu na mafuta yake yapakaae pembezoni mwa jino linalouma.

2.ikiwa jina halina tundu
pakaa mafuta ya mchanganyiko huu pembezoni kulizunguka jino linalouma

Tumia dawa hii kutwa mara tatu kwa muda wa siku tatu jino lako litakuwa limepona kabsaa kwa [emoji817].

MUHIMU:
[emoji871] Dawa hii inamatokeo ya haraka sana ambapo unaweza kutumia papo hapo jino likapoa,hivyo hakikisha unamaliza dozi kwa muda ulioelekezwa

[emoji871] Jiepushe na kunywa vinywaji vya moto sana au vya barid sana mpaka umalize dozi kwa muda uliopangwa.

Imeandaliwa na THABIT MAPANDE HERBAL CENTRE na kuchapishwa nami Nutritionist Kilindila.

Kwa mfululizo wa makala zitakazo kufundisha na kukupa elimu waweza kutufatilia kwenye page zetu;JipimeAfya
 
Ngoja nijaribu hii ya mgomba aisee. Nahisi dalili mbaya usiku wa leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…