Mjadala: Ni jambo gani kwenye Maisha yako lilichelewa sana? Ila sasa unaona kawaida sana

Mjadala: Ni jambo gani kwenye Maisha yako lilichelewa sana? Ila sasa unaona kawaida sana

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
18,585
Reaction score
16,780
Wakuu,

Kwenye haya maisha tuna mambo mengi sana ambayo ni matamanio, na kila mtu nafikiri wanayo. Sasa ni vitu gani ambavyo ulivitamani sana kuwa navyo, yaani ile tu unajiambia I wish, I wish...

Ila sasa unavyo au unavifanya na unaona ni kawaida kabisa yani!! Kuna watu walitamani kuwa na nyumba zao, sasa wanazo so wanaona ni kawaida tu, Wengine magari sasa wanayo so inaonekana kawaida tu...

Wengine kuwa na familia n.k Wengine hata elimu tu, kuna wale waliokuwa wanatamani kuwa na degree, masters au hata PHD sasa wanazo na ishakuwa kawaida tu!

Kila ambition mi naona kama inawezekana kwenye maisha ni kutia nia tu,

Kila unachokiona/kitamani kuwa nacho inawezekana kabisa.

Sasa kuna baadhi ya vitu vinachelewa, ila vinakuja tu!

Je, ni kitu gani mdau ulitamani kuwa nacho au kukifanya na sasa imewezekana na unaona kawaida?

Binafsi, nilichelewa sana kusafiri kwa kutumia ndege!!

Kwa sasa nasafiri na ndege maeneo mbalimbali Duniani kuliko hata ninavyosafiri na gari.

Sasa imekuwa kawaida sana 🤗.

Twende kazi.....
 
Kwa huu umri nilionao nilitamani sana niwe na kwangu pamoja na kazi labda pia na familia, ila ndo kwanza najitafuta mana sina hata kimoja hapo lakini huu mwaka kabla hujaisha nakwenda kufanya jambo moja kati ya niliyoyatamani.
 
Back
Top Bottom