Mjadala; Nini cha kufanya gari yako ikigongwa au kugonga?

Mjadala; Nini cha kufanya gari yako ikigongwa au kugonga?

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
12,001
Reaction score
27,175
Wakuu
Habari zenu.

Najua kuna watu wameshawahi kupata ajali ya kugonga gari ya mtu mwingine au gari yake kugongwa na gari nyingine,(Private cars)

Je, ikitokea hali hio ni kipi cha kufanya au hatua gani za kuchukua zinazoendana na sheria za nchi yetu?

Pia hata kama kuna hatua za kufanya ambazo ni rafiki zaidi ukiachana na hizi za kisheria ambazo zinaweza kuwa na ukiritimba ndani yake unaweza kusema pia.

Naamini michango yetu itasaidia kwa sababu inapotokea hali ya dharura kama ajali wakati huo akili inaweza ikakufanya usifanye maamuzi sahihi,lakini mtu akijua cha kufanya itamsaidia kutuliza akili na kufanya maamuzi sahihi.

Karibuni kwa uzoefu.

Asante.


determining-fault-in-common-types-of-accidents.jpg
 
Ngoja nikae hapa nisubiri wajuvi zaidi

Kirafiki ni kukubaliana nani mwenye makosa kama mtafikia muafaka na kujua nani atafidia uharibifu kwa kulipa pesa au matengenezo ya gari.

Kisheria nafikiri unamuhusisha askari kabla ya yote aje kuchukua maelezo ya kila gari na dereva halafu baadae ndio taratibu zingine zifuatwe kutambua nani mwenye makosa.

Kumbuka gari zikishaenda kituo cha polisi kutoboka hela ni nje nje.
 
Kuna kukubaliana myamalize Wenyewe

au

Kumuita Askari wa Usalama barabarani aje achore ramani ya tukio, kwenda kituo cha polisi kufungua kesi mahakamani na kwenda Bima kulipia (Third party na Comprehensive) na vitu vingine.

Option ya kwanza ni rahisi ikiwa mmeelewana na Option ya pili ina process nyingi sana na inapoteza muda japo ni uhakika.
 
1. Angalia kama umeumia au abiria ulie nae ameumia au huyo uliemgonga ameumia. Kama kuna alieumia hangaika na first aid kwanza.

2. Kama hukuna alieumia, hakikisha kwanza vitu vyako ndani ya gari vinakuwa salama. Manake watu wanatumia huo mwanya kuiba vitu katika taharuki hiyo.

3. Weka alama kuonesha kama kuna ajali hapo. Ikiwemo triangles wengine wanaweka majani kama ni highway.

4. Kama umegongwa, shuka piga picha za kutosha kila angle. Iwe kama ushahidi.

5. Tafuteni traffic aliekaribu aje kupima. Kesi iende mahakamani. Kama umegongwa bima yake itakulipa. Kama umemgonga bima yako itamlipa.

Kumalizana kumekaa kienyeji sana.
 
Ngoja nikae hapa nisubiri wajuvi zaidi

Kirafiki ni kukubaliana nani mwenye makosa kama mtafikia muafaka na kujua nani atafidia uharibifu kwa kulipa pesa au matengenezo ya gari....
Ni kweli umeongea vizuri, kama mkiweza kukubaliana nahisi ni bora ila kama mkishindwana hakuna namna.
 
Ngoja nikae hapa nisubiri wajuvi zaidi..
Ni kweli umeongea vizuri, kama mkiweza kukubaliana nahisi ni bora ila kama mkishindwana hakuna namna, nahisi hapo kwenye 'nani mwenye makosa'ndio panaleta utata
 
Ngoja nikae hapa nisubiri wajuvi zaidi...
Ni kweli umeongea vizuri, kama mkiweza kukubaliana nahisi ni bora ila kama mkishindwana hakuna namna, nahisi hapo kwenye 'nani mwenye makosa' ndio panaleta utata
 
Kuna kukubaliana myamalize Wenyewe...
Asante, kama hutojali pia hebu tusaidie faida ya hio bima ya third party na Comprehensive, tuchukulie umegonga gari na hauna bima?
 
Ni kweli umeongea vizuri,kama mkiweza kukubaliana nahisi ni bora ila kama mkishindwana hakuna namna,nahisi hapo kwenye 'nani mwenye makosa'ndio panaleta utata
Ndio mkuu.
Maana askari akija anaweza kuanza kufosi uchukue break down ivute ila naye ale % flani hapo hata kama gari inaweza kutembea yenyewe.

Mkishafika kituoni ndio utazungushwa mpaka utoe chochote wakuandikie inspection na form nyingine zile la sivyo unaweza kuacha gari ilale hapo tatizo jingine linaibuka la kubadilishiwa spare za gari lako unaweza kukuta zimefunguliwa kesho yake.
 
1. Angalia kama umeumia au abiria ulie nae ameumia au huyo uliemgonga ameumia. Kama kuna alieumia hangaika na first aid kwanza...
Mkuu ni sahihi kabisa umeelezea vyema.

Ila kumalizana mara nyingi kuna save time na usumbufu wa kufuatilia.

Ili bimayake ilipe (wewe ni third party) inabidi kuwe na court judgement(maamuzi ya mahakama kusema who was at fault. Hii ni document ambayo ni lazima kuwa nayo ili ulipwe na bima.

Ili kuipata hii inabidi usubiri si chini ua mwezi mmoja kwa mahakama zetu hizi.
Sasa mwezi mzima hutumii gari yako plus kwenda mahakamani au kumuuliza askari mwenye hilo jalada ni usumbufu sana pia wanaomba sana hela ya maji mkuu.

Watu wanamalizana sio kwamba hawataki kufuata process ila time.
 
Ndio mkuu.
Maana askari akija anaweza kuanza kufosi uchukue break down ivute ila naye ale % flani hapo hata kama gari inaweza kutembea yenyewe.

Mkishafika kituoni ndio utazungushwa mpaka utoe chochote wakuandikie inspection na form nyingine zile la sivyo unaweza kuacha gari ilale hapo tatizo jingine linaibuka la kubadilishiwa spare za gari lako unaweza kukuta zimefunguliwa kesho yake.
Hivi wanaobadilisha spea za gari kituo cha polisi ni kina nani hasa,Polisi wenyewe au vibaka?au wanashirikiana.
 
Mkuu kwa akili tu ya kawaida hakuna kibaka anaeweza kwenda kufungua spare kituo cha polisi.
Jibu ni kwamba wanalindwa na kugawana mafao ya kazi baadae.
[emoji3][emoji3],aisee wananchi tunapata shida sana na Jeshi la Polisi
 
Kuna jamaa yangu aligongwa na daladala, mwanzo mhusika alikubali kutengeneza.

Ila baadaye akaanza kuzingua, mpaka kesi ikaenda mahakamani.

Kifupi jamaa alipoteza sana muda na ile kesi, mambo mengi yakasimama na isitoshe alikuwa mkoani mbali na ziliko shughuli zake.

Kwa muono wangu ni bora mmalizane tu, au kama umegingwa na uharibifu ni mdogo unaweza potezea tu.

Ila kuna wengine huwa wanafanya kama kukomoana, utakuta umekwaruza kidogo tu ila hela anayotaja unabaki unashangaa!
 
Asante,kama hutojali pia hebu tusaidie faida ya hio bima ya third party na Comprehensive,tuchukulie umegonga gari na hauna bima?
Policy ya third party inalipa mtu mmoja yule uliyemgonga wakati comprehensive inalipa watu wote wawili aliyegonga na aliyegongwa

Kuwa na gari bila bima ni kosa kisheria ambapo ukibananishwa polisi/mahakamani ni ishu ingine
 
Aisee mimi sikugonga wala kugongwa ila gari yetu iligonga nguzo barabarani.

Aisee mziki wa kule police sio wa mchezo ila shughuli iko zaidi TANROADS kama ukiwa umeharibu miundombinu yao na watu wengi hawajui hili,yaani pesa utakayotajiwa unaweza ukazimia.

Nilikuta magari pale Tanroads jamaa wameyatelekeza baada ya kushindwa kulipa uharibifu walioufanya kwny miundombinu kwny ajali mbalimbali.

Nina mfano hapa ila hauna uhusiano na ajali,Kuna jamaa wa Fuso yeye alipata Breakdown highway akamwaga oil barabarani aliambiwa alipe Tsh. 3mil kwa uharibifu wa lami.

So wkt ajali inatokea muwe mnaomba kusiwe na uharibifu umetokea kwny miundombinu ya Tanroads.,hakika utalichukia gari lako na kujuta nani alikutuma ulinunue.
 
Back
Top Bottom