Mjadala; Nini cha kufanya gari yako ikigongwa au kugonga?

Policy ya third party inalipa mtu mmoja yule uliyemgonga wakati comprehensive inalipa watu wote wawili aliyegonga na aliyegongwa

Kuwa na gari bila bima ni kosa kisheria ambapo ukibananishwa polisi/mahakamani ni ishu ingine
Ok, asante kwa maelezo
 
[emoji3][emoji3] inachekesha lakini inauma,yaani ukiwa na gari nchi hii ni kama wanakufanya mtaji hivi,yaani kumwaga oil tu mil 3,hapo lazima utaacha gari tu
 
[emoji3][emoji3] inachekesha lakini inauma,yaani ukiwa na gari nchi hii ni kama wanakufanya mtaji hivi,yaani kumwaga oil tu mil 3,hapo lazima utaacha gari tu
Hahah aiseee nilishangaa sana mkuu,yaani hata ukimwaga yale maji ya kwny rejeta barabarani jamaa hawakuachi una bonge la fine ambalo hukuwahi kulifikiria.
 
Kuna jamaa yangu aligongwa na daladala, mwanzo mhusika alikubali kutengeneza.
Mara nyingi wewe unaona umemkwaruza kidogo tu ila madhara yake ni kupiga rangi panel nzima(mlango,bumper,fender) ili kuepusha rangi kupishana. Rangi nyingine inabidi ipigwe upande mzima. Matokeo yake gharama inakuw kubwa wakati umemkwaruza sehemu ndogo tu
 
Nafahamu ila kuna wengine hufanya kukomoa tu!
 
Hivi Kama gari imekugonga ukiwa kwenye gari lingine na aliyekugonga kakimbia ila umepiga picha plate namba yake unawezaje kumkamata. Hii hutokea sana usiku ambapo mtu anakugonga Kisha anakimbia
 
Hivi Kama gari imekugonga ukiwa kwenye gari lingine na aliyekugonga kakimbia ila umepiga picha plate namba yake unawezaje kumkamata. Hii hutokea sana usiku ambapo mtu anakugonga Kisha anakimbia
Mkuu hii sijajua kama huo ushahidi wa picha likiwa linakimbia ni sufficient.
Labda uchukue video ya tukio zima.
 
Maelezo mazuri, tuchukulie kagonga gari yako yako mkiwa Highway,halafu akaamua kuondoka inakuaje hapo?
Nashika namba za hiyo gari ilionigonga.

Nasimama. Naangalia kama nimeumia.

Napiga picha za kutosha kama ushahidi.

Nikifika mbele nawataarifu polisi kilichotokea. Watafanya mawasiliano na wa mbele kusimamisha hilo gari.
 
Mtu amepasua taa zako kununua zote mbili unaambiwa 300k. Plus ufundi wa kurekebisha hapa na pale.

Yeye ataanza kulalamika akupe 50k au 100k au akakununulie mitumba ya ilala.

Wakati bima inakupa kitu brand new plus maintainance ya nzuri.

Hata nikikugonga, sikupi hata sh 100. Bima yangu itakulipa. Na ntakupa ushirikiano mwanzo mwisho.

Ndo maana sipendi mambo ya kumalizana kienyeji.
 
Kama una bima kubwa si italipwa?
 
Kama una bima kubwa si italipwa?
Yes italipwa(vigezo na masharti kuzingatiwa) ila inachukua muda mrefu sana,maana kuna magari mengi sana niliyakuta pale yakisubiri case zao za insurance kua settled.
 
Yes italipwa(vigezo na masharti kuzingatiwa) ila inachukua muda mrefu sana,maana kuna magari mengi sana niliyakuta pale yakisubiri case zao za insurance kua settled.
Muda mrefu ni upi?

Kwa watu ninaowafahamu, kesi zao za bima zilichukua 2 weeks na bima ikawafanyia matengenezo.

Kampuni ninayokata bima, mmiliki namfahamu personally. Nikipata shida, nampigia anaharakisha mchakato.

Nafahamu kesi nyingine canter iligonga gari tena mpya zile za kuchana makaratasi.

Mwenye kenta alikuwa na third party. Kesi ikaenda mahakamani na ndani ya week hukumu ikatoka.

Gari ikapelekwa kwa dealer, mzigo ukabadilishwa kila kitu kibovu.

Ni zoezi kama la week 2 tu.

Ndo maana nasema, hizi kampuni za bima zinaondoka na hela nyingi sana kwa wateja wao wanavyomalizana kienyeji barabarani.

Kuhusu suala la tanroads sijawahi kukutana nalo.
 
Naongelea suala la pesa ya bima kwny miundombinu ya serikali iliyoharibika kwa sababu ya ajali iliyosababishwa na gari husika.

Sijaongelea Pesa ya bima kwny ajali ya gari kwa gari.
 
Nashika namba za hiyo gari ilionigonga.

Nasimama. Naangalia kama nimeumia.

Napiga picha za kutosha kama ushahidi.

Nikifika mbele nawataarifu polisi kilichotokea. Watafanya mawasiliano na wa mbele kusimamisha hilo gari.
Asante
 
Naongelea suala la pesa ya bima kwny miundombinu ya serikali iliyoharibika kwa sababu ya ajali iliyosababishwa na gari husika.

Sijaongelea Pesa ya bima kwny ajali ya gari kwa gari.
Najua.

Kama kampuni ya bima inaweza kulipa claims za ajali na hiyo ni ajali.

Nayo inatakiwa kushughulikia kwa uzito uleule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…