Aisee kumbe ukikwaruza unaweza kuosha pakangaaa kabisa??Kuna Mama mmoja aligongwa na Mzee basi bana Mama anataka aende kwa Mchina kasehemu kenyewe kadogo sana.
Mzee akampa 50,000 akagoma, nikazichukua nikapanda gari la huyo Mama tukafika Mwenge nikachukua wale mafundi wakasema mbona hapa twaosha tu panakuwa safi....
Kweli bana wakaosha tu nikawapa 15,000
Yule mama alisonya sana
Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kuna kitu kinaitwa EXCESS kwenye bima. Hiki ni kiwango wewe unachangia kwenye matengenezo iwapo gari yako itapata ajali. Kwa Mimi ni around 300,000. Sasa ukipata ajali gharama zikawa 1m bima watatoa 700,000 na wewe 300,000. Sasa iwapo gharama za matengenezo ni chini ya 300,000 bima haitatoa chochote utalipa wewe mwenyewe. Hii ndio sababu viajali vidogovidogo mtu anakukomalia kwasababu bima haitamlipa. Hapa nazungumzia bima kubwaSafi sana huu ndo ubinadamu
Sasa kuna mtu atauliza unalipa bima ina kazi gani?
Kuna jamaa alikwarua gari ya mwenzake akavunja taa ya mbele wakati anapaki baa
Aliyepasuliwa taa akataka jamaa amlipe bei ya taa na ufundi wamalizane
Mshkaji akagoma akasema ita trafiki waje kupima atalipwa na bima na ndio maana amelipia bima gari yake
Mgongwaji akaondoka...... jamaa alipomaliza bia zake ile kutoka akakuta taa zote zimevunjwa halafu jamaa hamjui [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]