Mjadala: Nini chanzo na tiba ya tatizo la upele kuota kwenye uume?

Mjadala: Nini chanzo na tiba ya tatizo la upele kuota kwenye uume?

Pia limenikuta tatizo kama lako ila mimi nimeambukizwa na mshikaji wangu dah, nimehangaika sana adi kifika hapa na kusoma comments za watu najua zitanissidia. Akhasanteni sana
 
Mkuu huna picha ya shemeji utume tuone?

Huwezijuwa pengine na yeye ana tatizo.
 
Habarini za muda huu wakuu

Aisee hili tatizo na mimi limenikuta ni mda umepita nilipitia huu uzi....sasa nimejikuta na mimi limenikuta hili tatizo nilianza kuwashwa mwili yani kuwashwa ile serious hadi nikawa naogopa haikuchukua muda vikaanza kuchipua kijiupele hapa kwenye eneo ya kibovu na baadae uume nao anatokea kama ngozi flani ngumu na ukawa unawasha nikawa napaka mafuta ya nazi pia nikarudi kwenye huu uzi kusoma vizuri na kufuata baadhi ya ushauri uliokua ukitolewa hapa kwenye huu uzi pia nikamuona doctor Mmoja kwenye pharmacy yake hapa kijijini nikamuelezea tatizo langu nakuonyesha hivi kijiupele kwenye eneo la kibovu akaniambia ni tatizo la virus wa HPV akaniambia watibabu yake ni Sindano pamoja na dawa atanipa akaniambia nikatafute elf20 afu niende nayo anichome hiyo Sindano na kunipa hizo dawa nilipoenda kesho yake asubuhi akanichoma Sindano ambayo kama sijakosea ilikua imeandikwa zitheza yani hiyo dawa ipo kwenye kijichupa kidogo ya unga anaichanganya na vimaji flani vipo kwenye kichupa kingine afu anaitingisha kama kwa mda wa dakika 15 20 hivi afu ni dawa nyingi unachomwa Sindano mbili yaani tako la kulia moja na jingine moja inauma kiasi mtu muoga uchomi na dawa akanipa acyclovir yakumeza wiki moja pamoja na B.B.E yakupaka pamoja na azuma kidonge kimoja nikawa nameza 2x3 kwa Siku na kidonge za azuma nilimeza ile Siku tu na kidonge kingine alinipa pia

Sasa ni wiki ya pili sasa tangu nianze kutumia dawa kuwashwa kumeisha kwa asilimia kubwa sana ila sasa vile vijiupele kwenye uume bado vinaendelea na kingine kilitokea kwenye shingo ya kichwa cha umeme hadi kikawa kinatoa maji maji saivi kimekauka ila bado kuna vingine kama naota vidogo vidogo vinaendelea kuoteana na kile kinyama kwenye kibovu kipo vile vile sasa nikaona nitafute dawa nyingine nikarudi pale kwa doctor akaniambia hiyo ndio full doze ila inafanya kazi taratibu niendelee kusubiria sasa mimi naona navyoendelea kusubiria ndio tatizo litaendelea kuwa kubwa nikasema nitafute dawa nyingine ambayo Jina nililitoa hapa kwenye huu uzi inaitwa imiquimod na nyingine podofilox sasa kimbembe ni kwenye kuipata hiyo dawa nikaitafuta hapa kwetu hamna maana me nipo mkoani sasa kuna jamaa yangu yupo dar nimemuomba anitafutie kwenye pharmacy kubwa kubwa kule kariakoo ameniambia ameikosa..sasa nimebaki na wasiwasi sijui pakuipata nawaza vikiendelea itakuaje sitopiga tena shoo kweli daah hizi ngono naacha kama sio kupunguza hadi nitakapo oa mke wangu.. nimeweka kapicha hapo lengo ni kurahisisha kupata msaada

NB: Nimepima damu afya yangu ipo vizuri maana ndio cha kwanza nilifanya.. nilichoshindwa nikwenda kufanya vipimo zaidi vya huu ugonjwa maana sina bima.

Naomba kuwasilisha kwa msaada waungwana View attachment 1734415View attachment 1734416
View attachment 1734421
View attachment 1734426
Kaka umepata solution ya tatizo lako?
 
Mkubwa pamoja na mambo mengine yote tumia folic acid 1 kisonge Kwa siku Kwa mwezi
 
Unapata vipele kwenye kiwiko(kipepsi)? Luna vipele vidogovidogo vidoleni? Unawashwa Sana usiku ukilala? Unasikia vitu kama vinakutembea mwilini? Kuna saa unawashwa kiunoni?

Kama unapata his dalili nijibu nikuelekeze dawa pharmacy.. Zinauzwaga 8,000 -10,000( elf nane hadi elf kumi)
Dawa gani mkuu
 
Habari zenu wana JF, samahani sana kwa usumbufu kama vile tujuavyo misemo ya wahenga kuwa mficha uchi hazai.

Since mwezi wa nne nasumbuliwa na hili tatizo nimetumia dawa nyingi sana ant fungus kama zote za tube mpaka za kopo ila bado tatizo linanisumbua.

Ninawashwa sana mwilini na vijipele vimetokea mkononi na sehemu za siri, nimepima hospital kama BURHAN, Regency wanasema siumwi kitu ila hali yangu mimi naona inazidi kua mbaya.

Majuzi nimepima hospitali ya mtaani wakasema na syphilis nimeanza matibabu ya sindano zile nne za mwezi mpaka sasa nishachoma sindano 2 ila bado hali iko vile vile tena ndio inazidi kabisa.

Mwenye msaada naomba anisaidie nawashwa sana mwili.

View attachment 1183912View attachment 1183913View attachment 1183915

UFAFANUZI WA JUMLA TATIZO HILI KUTOKA KWA MTAALAMU

MASUNDOSUNDO, MALENGELENGE, VINGWARU NA VIPELE LAINI NA VIDOGO SEHEMU ZA SIRI
Ukiwa mzima mshukuru Mungu mara mia mia, sisemi ukiwa sio mzima usimshukuru Mungu la hasha ila ninataka kuonyesha msisitizo ya kwamba kuna watu wanateseka na mardhi ya kila aina ile hali wewe mzima kabisa wala huoni sababu ya kumshukutu Mola wako.

Leo ningependa kuongelea habari ya #masundosundo, #vipele laini na #malengelenge sehemu za siri, ni vitu vidogo lakini mara nyingi vinaleta usumbufu hadi wengine kuanza kudhania wameathirika, kumbe sio. Kumbuka ili kujua umeathirika na #VVU lazima uwe umepima. Tabia ya kujipima wenyewe haifai na ni hatari sana. Kuna watu wanaota vinyama laini vidogovidogo kwenye sehemu za siri yaani nfano kichwa cha uume, mashavu ya uke, ndani kwenye mirija ya mkojo, maeneo yanayozunguka haja kubwa, kwenye makoo na mdomoni. Aidha wengine wanaota vipele vidogo vidogo sehemu mbalimbali za siri vinavyopasuka na kuacha maji mnato ivi na kisha kuunda kidonda cha wastani. Usikae na ugonjwa onana na madaktari au washauri wa afya ili uweze kuanza safari ya matibabu.

MAAMBUKIZI NA CHANZO CHA MAGONJWA HAYA ni ukosefu wa kinga imara ya mwili, kujamiiana hovyo kwa njia ambazo sio za asili na kuvaa nguo za ndani chafu. Magonjwa haya ni ya kuambukiza na pia ya kujitakia. Wadudu jamii ya virusi,bacteria na fangasi hupata nafasi kutokana na tabia hizoo na kuanza kushambulia maeneo haya niliyoyataja kirahisi sana.

DALILI ZAKE
  • Kuna vinavyoonekana kwa macho lakini vingine huwa havionekani kabisa utasikia muwasho mkali kama wa kuunguza na moto kwa mbali, iwapo utakuna unaweza tokea michubuko inayochelewa kupona. Iwapo vinaonekana basi ni kama unavyoona katika picha hapo chini.
  • Maeneo yaliyozungukwa na masundosundo saa ingine yanapata ganzi
  • Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri kama ugonjwa upo kwa ndani.
  • Kutokwa na damu ukeni hasa baada ya kufanya tendo la ndoa, ile hali hauko bleed.

UBAYA WA MAGONJWA HAYA
  • Usumbufu wa kujikuna kuna sehemu za siri kila wakati wakati mwingine utajisahau hata mbele ya wakwe
  • Maumivu
  • Ukosefu wa uhuru
  • Kuchochea magonjwa mengine
  • Kukosa uhuru wa tendo la ndoa

NAMNA GANI UTAJIKINGA
  • CHAKULA NI KINGA YA KWANZA, kama hujapata bado basi hakikisha unakula chakula bora chenye uwingi wa vyakula vyenye kukukinga dhidi ya mardhi na vyenye kujenga nguvu ya mwili na kuzalisha seli kwa wingi. Vyakula hivyo ni pamoja na vyakula vyenye protein kwa wingi, mbogamboga na matunda
  • EPUKA NGONO ZEMBE NA NGONO KIYUME NA MAUMBILE
  • Wanawake wasagaji achana na mchezo huo
  • Kuwa msafi kila wakati (hasa mliopo sehemu za joto kama DSM). Badili nguo za ndani mara kwa mara, wanaume mara nyingi utakuta mtu anavaa jeansi moja wiki nzima, hii siyo sawa.
  • Vaa chupi zilizotengenezwa kwa pamba na usivae nguo nyingi za ndani.
  • Siku za bleed tumia pedi za pamba, zenye uwezo wa kuingiza hewa safi na kutoa hewa chafu na kisha kuuwa wadudu wa aina yeyeto walio na uharibifu kwa mwili wako. Sisi tunapendekeza pedi za #Neplily kama hujawahi zitumia jaribu inaweza kuwa ndio mkombozi wako.
Kama tayari umeshapata na unamagonjwa haya kwa muda mrefu au huwa yanakuja na kutoweka basi wasiliana nasi kwa ushauri zaidi. Ili uweze kupata ushauri kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili, kupata food suppliment ili kuweza kudhibiti wadudu hawa waharibifu na wasumbufu.

USHAURI KWA WADADA – Mapenzi ya kusagana, kunyonyana sehemu za siri na mapenzi kinyume na maumbile hayafai. Tafuta namna ingine ya kumridhisha mwenza wako. Najua wadada wengi ni wasafi lakini wachache ni wachafu kabisa, pia wengi hamtumii pedi salama.

USHAURI KWA WAKAKA – Mara nyingi wakaka hukutwa na malengelenge kwenye uume na vile vipele laini vyenye kutoa maji, masundodundo wengi yanawatokea kwenye haja kubwa. Wengi hubakia kuwa cariers kwa kuendelea kuambukiza wanawake wengine ile hali wao hawana dalili, kama mpenzi wako ana dalili mojawapo kati ya hizo hapo juu basi na wewe lazima upate tiba ili kumaliza tatizo hili kikamilifu.

Achana na tabia mbaya za ngono kinyume na maumbile, kupiga punyeto, kula vyakula visivyokuwa na matunda na mboga, kuvaa nguo chafu muda mrefu bila kufua, kutumia madawa ya kulevya na pombe kali kupindukia. Kama tayari una tatizo hili tafadhali kwa sasa lina ufumbuzi na utatuzi ambapo utatumia


BAADHI YA MAONI NA USHAURI KUTOKA KWA WADAU WA JF

---

---

---

---
Ni kaswende hiyo au kitaalamu ni syphilis. Wewe na mke wako mkapime kipimo cha VDRL ili muanze shindano za Benzathine penicillin
 
Pole sana dokta wa Mchongo nliishapona na kusahu, ilo lilikua sio tatizo bali ni ugonjwa wa Ngozi na nlipewa dawa kwa wiki 3 tu nikawa nimepona nashauri ukasome tena issue za scabies
 
Pole sana dokta wa Mchongo nliishapona na kusahu, ilo lilikua sio tatizo bali ni ugonjwa wa Ngozi na nlipewa dawa kwa wiki 3 tu nikawa nimepona nashauri ukasome tena issue za scabies
Hongera so walisema ni scabies

Basi mimi ni mweupe aisee so ukapewa BBE
 
Mkuu ifike wakati tuache kushauri vitu ambavyo sio field yetu. Kwa ulichoandika hapa nina uhakika 100% hauko kwenye field ya medical.
Clotrimazole and whitefield zote ni antifungal
Hydrocortisone ni antihistamine and anti inflammatory
Ni kwa vipi hizo dawa ziko associated na dalili ya ugonjwa unaonekana kwenye pic hapo.
Please let us respect other's professional tuachane na taarifa za mtaani
This guy need serious treatment sasa wewe unakuja na hadithi za namna hii
Utamchelewesha kupata tiba sahihi
Upo sahihi 100%
 
Back
Top Bottom