OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Kumekucha!
Lengo la mjadala huu ni kuwafahamisha wanajamii kuwa wakati mwingine wasiwe na mategemeo makubwa saana juu ya utendaji wa viongozi wao. Wachukulie kawaida tu kwamba tunaenda kimungu-mungu. Lakini wajue moja ya sababu zinazotufanya tukwame kwa miaka mingi ni kuwa na watu wa namna hii.
Wakati nikiwa mdogo niliamini kuwa boss au kiongozi mkubwa kama Mbunge, Waziri, Mkurugenzi nk unakuwa dude lenye akili kubwa sana. Somi moja matata lenye uwezo wa kufikiria mambo kwa kasi ya kompyuta. Aisee kumbe nilikuwa najidanganya sana. Hali ni tofauti kabisa.
Fikra hizi wengi wetu bado wanazo sana, wana imani kubwa sana na mabosi na viongozi wao. Lakini ukweli ni huo mabosi wengi wana vyeo vyeti, wamevaa masuti mazuri, gari nzuri lakini ni weupe katika kiwango cha juu sana. Yaaani hamna kitu-ni mradi tu.
Prof. Assad aliwahi kusema hili akashtumiwa sana. Lakini alisema anachokijua.
Achana na siasa halafu fikiria jinsi kina Halima Mdee walivyobakia kuwa wabunge. Au fikiria jinsi Dkt. Gwajima alivyoanza kuzungumzia mkono wa baunsa wakati anajibu hoja za Askofu kuhusu Corona. Au fikiria DED wa Gairo anatuhumiwa kuiba mabati ya Halmashauri. Unaweza kufikiria pia wabunge walivyoweza kupitisha tozo za miamala ya simu bila kujua kiwango, halafu wanataka tena wapelekewe wajadili upya huku wakilipwa posho. Hawa ni watu takribani 300.
Sitaki kuingiza siasa lakini nakupa mifano hai uelewe kwamba bosi wa kitanzania ukimtoa suti anabaki mtupu.
Tanatokaje hapo, hata mimi sijui kwa sababu idadi yao ni kubwa sana.