Uchaguzi 2020 Mjadala ungelitakiwa uwe kumuongezea muda Dkt. Magufuli na sio kuombana kura

Uchaguzi 2020 Mjadala ungelitakiwa uwe kumuongezea muda Dkt. Magufuli na sio kuombana kura

mkanta majura

Member
Joined
Sep 22, 2020
Posts
97
Reaction score
71
Na Thadei Ole Mushi

Kuna siku niliwaambia wenzetu huko nje wakiona wamepata kiongozi mwenye maono huwa hawamwachii kwa haraka.

Niliwahi kuwaambia kuwa Urusi wao kwa kutambua Mchango wa Putin waliamua kubadilisha katiba yao badala ya Putin kustaafu 2024 walimuongezea muda mpaka 2036. Bunge la Urusi lilipitisha kipengele hicho cha kumuongezea muda Putin kwa kishindo. Warusi wanaona kuwa ili maono ya Taifa lao yakamilike lazima pale juu awepo mtu mbishi Kama Putin na asiyeyumbishwa na mataifa Mengine.

China wao mwaka 1990 kwenye katiba yao walipitisha kuwa kila Rais atastaafu baada ya miaka 10 akiwa madarakani. Lakini mwaka juzi waliamua kubadilisha kipengele hicho kwa kuhofia kumpoteza Xi Jinping wameamua kugusa Katiba yao na Sasa atakaa madarakani Hadi Kifo kitakapomchukua. Jinping alikuwa astaafu 2023 kwa mujibu wa katiba kabla hawajaigusa.

Nimekuwa nikiwaleta maajabu ya Serikali ya awamu ya Tano kila Mara leo tuguse kipengele cha Elimu kwa miaka mitano Nini kimefanyika.

1. Serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani iliamua kufuta kabisa ada kwa wanafunzi wote wa kuanzia awali Hadi kidato Cha nne. Mpaka kufikia February 2020 Serikali ilikuwa imeshatoa shilingi trilioni 1.01 kugharamia Elimu bure. Ni nchi pekee kwenye ukanda wetu huu iliyoweza kutoa Elimu bure.

2. Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuongeza shule za primary toka 16,899 zilizokutwa 2015 Hadi kufikia 17,804.

3. Kwa upande wa Shule za Sekondari zimeongezwa Kutoka 4,708 Hadi 5,330.

4. Serikali imefanya Ukarabati wa shule kongwe 73 Kati ya 89. Ukarabati huu kila pembe ya nchi mnauona unavyitafuna mabilioni ya shilingi.

5. Serikali ya awamu ya tano imefanya Ujenzi wa mabweni 253 ya shule za Serikali.

6. Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kufanya Ujenzi wa Maabara 227 katika shule mbalimbali nchini

7. Serikali ya awamu ya tano imetoa vifaa vya Maabara zipatazo 2,956.

7. Madawati JPM aliyokuta yalikuwa 3,024,311. Ameyaongeza Hadi kufikia 8,095,207 sawa na asilimia 200 ya ongezeko.

8. Vyuo vya ualimu 18 vimejarabaitiwa. Vyuo hivi vilielekea kuwa magofu. Hii Ni kazi ya Serikali ya awamu ya tano.

9. Vyuo viwili vimejengwa upya Murutunguru na Kabanga. Kazi hii imefanyika ndani ya miaka mitano.

10.Zimegawanywa computer 1,550 kwenye vyuo 35 vya ualimu nchini.

11. Vyuo vya ufundi VETA vimeongezwa toka 672 mwaka 2015 Hadi 712 mwaka 2020

12.Bajeti ya mikopo ya Elimu ya juu imeongeza toka Bilioni 348 kwa mwaka Hadi Bilioni 450.

Sisi tunaoelewa Nini kimefanyika usituulize kwa nn tunataka JPM aongezewe Muda.

Usituulize kwa nn tunataka JPM achaguliwe Tena.

Narudia, yale mazuri ya Upinzani yatachujuliwa na ikiwezekana wale wenye uwezo mkubwa kichwani wanaweza kuchukuliwa wakalijenge Taifa lao.

Duniani hakuna nchi ambayo imewahi kumaliza Changamoto zake zote. Lakini mnapopata mtu wa kupambana nazo Kama JPM sio wa kumwachia haraka.

Ole Mushi
0712702602.
 
Tundu Lissu anatembea na risasi katika nyonga yake, madaktari hakuweza kuitoa. Waliompiga risasi hamna anayetuhumiwa, hakuna aliyehojiwa, ila alinyimwa fedha za matibabu kwa Magufuli kumwagiza Ndugai, alivuliwa ubunge kwa mizengwe, na kuna kila ushahidi wa kimazingira kuwa dola inahusika.

Sio Lissu tu, Ben Saanane, Azory Gwanda, Simon Kanguye na wengine wengi kule Kibiti na Rufiji hawajulikani walipo. Hata kama amejenga vya kujenga lakini uhuru na haki ni muhimu kuliko hivyo. Jiwe kwa msingi huo apumzishwe tu. Kwani hakuna mwingine hata huko Ccm?
 
Tundu Lissu anatembea na risasi katika nyonga yake, madaktari hakuweza kuitoa. Waliompiga risasi hamna anayetuhumiwa, hakuna aliyehojiwa, ila alinyimwa fedha za matibabu kwa Magufuli kumwagiza Ndugai, alivuliwa ubunge kwa mizengwe, na kuna kila ushahidi wa kimazingira kuwa dola inahusika. Sio Lissu tu. Ben Saanane, Azory Gwanda, Simon Kanguye na wengine wengi kule Kibiti na Rufiji hawajulikani walipo. Hata kama amejenga vya kujenga lakini uhuru na haki ni muhimu kuliko hivyo. Jiwe kwa msingi huo apumzishwe tu. Kwani hakuna mwingine hata huko Ccm????
Wahusika wanacheck tu mkuu
 
Ni heri kubakia Maskini lakini kuwepo na Uhuru na Haki. Nchi hii tumefika mahali pabaya ikitokea umemkosoa kiongozi uwezekano wa kupotea ni mkubwa mno.

Tumchague Tundu Lissu atarejesha Haki, Uhuru wa kutoa maoni na kuleta maendeleo yatakayoakisi maisha wa watu na si maendeleo ya vitu tu.
 
Itabidi tuanze kuhoji uwezo wenu wa kufikiri, kwani 2015 aliomba kura kuja kuteka, kuua kutoshaurika, kutopangiwa, kudhalilisha utu wa watu kwenye hadhara pekee?

Alipiga push up ili akatende na hayo uliyoyataja, ni wajibu wake na sio hisani. Ndo maana tumekuwa Nchi ya watu omba omba kila kitu rais, maana hamfikilii kuwa kazi ya rais ni pamoja na kuleta maendeleo kwa watu wake bila kujari vyama, ni kodi zetu sote hivyo katiba ilindwe na sheria zifuatwe.

Hii nchi imeshaangamia tayari, kwa viongozi na baadhi ya wananchi kama wewe kukosa maarifa.

Sina haja ya kuuliza elimu yako baada ya kusoma huu uzi wako. Maana naweza nikahoji kisha nikapotezwa. Matabiriki nyie. ...
 
Baba wa taifa aliwahi kusema katiba iheshimiwe, muda wa kutawala uwe vipindi viwili tu awe amefanya mazuri au mabaya, la sivyo nchi inaweza kuishia kuwa na mfalme wa kuchaguliwa.
 
We Ole Mushi unajua nini aliyafanya Gaddafi kule Libya? Kwa nini walimtoa kishenzi hadi kumchomeka vijiti makalioni? Na jee unajua uharibifu wa nchi kwa sasa chanzo ni Gadaffi huyo huyo aliyejenga matabaka yanayoleta uhasama hadi Leo?

Kuwajibika kwa kiongozi wa nchi kwa taifa lake wala sio jambo LA ajabu bali wajibu ndio maana anatunzwa vizuri sana kuliko binadamu mwingine yeyote ndani ya nchi. Na akishindwa kutimiza ndio maana kuna uchaguzi kila baada ya kipindi fulani ili kama amezingua atolewe.

Huyu haheshimu katiba, hayo yote unayosifia hayapo kimpangilio na ethics za uongozi hazifuati kabisa.

Aende zake tuu
 
Narudia, yale mazuri ya Upinzani yatachujuliwa na ikiwezekana wale wenye uwezo mkubwa kichwani wanaweza kuchukuliwa wakalijenge Taifa lao.

Duniani hakuna nchi ambayo imewahi kumaliza Changamoto zake zote. Lakini mnapopata mtu wa kupambana nazo Kama JPM sio wa kumwachia haraka.
Kwangu mimi mjadala ni demokrasia tunayoitaka. China na Urusi si mifano mizuri ya kuiga hata kidogo kwenye demokrasia. Ni kitu cha ajabu kuamini kuwa ni mtu mmoja tu anaweza kuongoza nchi yenye watu zaidi ya 50,000,000. Tukiwa na mifumo mizuri tunaweza kubadilisha viongozi na bado tukapata maendeleo.

Katiba mbovu, uchama dola na "ukondoo wa Nyerere" ndio vinavyo turudisha nyuma. Tuna mifumo ambayo hata hayo wengine wanayo ona ni mazuri ya JPM akiondoka yanaweza kupotea ndani ya mwezi mmoja.

Bahati mbaya simuoni wala kumsikia akiongelea ujenzi wa mifumo bora-tunacho ambiwa ni serikali yangu, serikali ya magufuli, magufuli katoa hela za kufanya hili au lile na hili ndio litatufanya tuendelee na kila kiongozi kuwa na lake. Miaka 5 inatosha, ikilazimu 10 mwisho na sivingenevyo.
 
Wewe poyoyo kweli akili za jongoo.

Nyie ndio aina ya watu ambao mnadhihirisha jinsi elimu yetu ilivyo ovyo (kama hata umeenda shule). Teuzi naona unaitafuta kwa nguvu.

Hayo yote uliyoyasema ni WAJIBU WA SERIKALI kuyafanya. Sio hisani. Kwani hela anatoa mfukoni mwake? Si ni hela za watanzania?

TUTAMGOA MAGUFULI KWA SABABU YA KUFANYA AMBAYO HATUKUMTUMA NA AMBAYO NI KINIYUME NA KIAPO CHAKE:

1) Kuua na kuteka watanzania wenzetu
2) Kubambikia kesi watanzania wenzetu kwa malengo ya kisiasa
3) Kunyima haki na uhuru vyama vya upinzani kinyume na katiba
4) kuendesha nchi kama mali yake binafsi
5) kupora uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwanyima haki maelfu ya wagombea wa upinzani na kupandikiza CCM tu
 
Hiiiiiiiiii.
EkC6MxgXsAEG-gl.jpg
 
Ni kweli Dr. Magufuri ana maono mazuri kwa nchi hii, shida raia wengi wa tanzania bado wana njaa sana,watz wengi wanategemea kupata chakula walichotafta siku husika, hatuna akiba yoyote.

Hata wafanyakazi wa serikali hela ya mwezi inaisha kabla ya mwezi kuisha. Kibaya zaidi kabana ajira kwa hiyo hamna mzunguko wa hela mtaani.

Kwa hiyo magu tunampenda pia uhai wetu tunaupenda atusamehe tutakao mnyima kura
 
Back
Top Bottom