Uchaguzi 2020 Mjadala ungelitakiwa uwe kumuongezea muda Dkt. Magufuli na sio kuombana kura

Uchaguzi 2020 Mjadala ungelitakiwa uwe kumuongezea muda Dkt. Magufuli na sio kuombana kura

Akili zikiwa zimejifungia ndani ya kasha, kwa hakika hazitakuwa na uwezo wa kuona vyema fursa zilizopo nje yake. Akili za namna hizi ndizo kikwazo kikubwa cha kujaribu hata kuthubutu kufanya uvumbuzi na ugunduzi wa mambo yaendayo na fikra mpya.

Akili zilizofungiwa ndani ya kasha, haziwezi kufanya tathimini sahihi juu ya ulinganisho unaoendana na thamani na ubora halisi wa bidhaa ama huduma zitolewazo kwa umma kupitia ktk mzigo wa kodi, maduhuli na hata deni halisi la taifa libebwalo na Watanzania.

Ni mtu pengine mwenye matarajio ya kufikiriwa kupewa cheo cha upendeleo hapo baadaye ndiye ambaye ataungangana na porojo za watawala. Naye atajiunga nao ili awaminishe watu kupitia takwimu zenye mashaka juu ya kile ambacho kimefanyika ndani ya awamu hii. Takwimu zisizo hakisi uhalisia wa ubora wa bidhaa wala huduma zitolewazo na serikali kwa wananchi waliokuwa wengi hapa nchini.

Ni lazima tujifunze kupitia mataifa mengine. Wao huwapima viongozi wao kupitia kuitii, kuilinda na kuizingatia katiba. Wao huwapima viongozi wao kupitia maono sahihi ambayo wanayabeba kwa ridhaa zao na siyo kupitia kuwabana watu wao pale wanapowakosoa ikitokea wanakwenda kinyume na matarajio yao.
 
Back
Top Bottom