Mjadala wa Katiba Mpya on Star TV this Sunday

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
270
Reaction score
317
Kama tulivyoahidi wiki iliyopita, elimu ya ulazima wa Katiba mpya kwa Watanzania itatolewa kupitia mjadala huu hapo kesho kuanzia saa 1 na dk 3O asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI.
WanaJF Micahngo na mawazo yenu yanakaribishwa na hatutasita kuyatumia kwa manufaa ya umma kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki makini na wa kipekee wiki iliyopita
Yahya M
 

Kwani katiba ya sasa haitoshi?

Ingekuwa vizuri akaleta mjadala wa kuleta maendeleo Tanzania
 
Mbona habari roborobo? Taja wageni waalikwa tafadhali.
 
Kwani katiba ya sasa haitoshi?

Ingekuwa vizuri akaleta mjadala wa kuleta maendeleo Tanzania

Hilo ni sehemu ya swali kwa wageni wangu, ahsante kwa mawazo. Mjadala upo pale pale mkubwa kama kwako hauna manufaa wengine inawanyima usingizi.
 
Tazama post ya wiki iliyopita...Huu ni mwendelezo wa last week kama hukupata that means archieve hapa JF iondolewe
 
Hilo ni sehemu ya swali kwa wageni wangu, ahsante kwa mawazo. Mjadala upo pale pale mkubwa kama kwako hauna manufaa wengine inawanyima usingizi.

watanzania vijijini wanakufa kwa njaa toa mijadala ya kuwakwamua kiuchumi
 
Hata wewe ni sehemu ya mshiriki muhimu ni mawazo yako na si nani yupo studio jamani, watanzania mbona kazi ipo.
 
Tushatoa sana wala wewe si wa kwanza kulisemea hilo, seems bro umekuja hapa leo katika mjadala huu. kama huna hoja usipochangia napo si dhambi.
 
Yahya,

Natumaini umesoma mapendekezo yetu hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ent-needed-mabadiliko-ya-katiba-uzalendo.html

Na pia umepitia mawazo yetu mengi sana juu ya katiba ya sasa jinsi ilivyo na tunavyopendekeza iwe hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ania-ilivyo-na-mapendekezo-ya-mabadiliko.html

Aidha, nawatakia kila la heri kipindi hicho cha kesho, ukisoma nondo hizo nilizokupa hutouliza maswali kama watangazaji wa TBC1 bali kama mwananchi pia, yani uwe sehemu ya wananchi usiwe sehemu ya watawala!
 
Waiting for your call brother, last week it was worth of salt despite some few technical problem with connection, but I appreciate.
Thank you in advance
 

Shukrani sana Mugumu
Ngoja nizitazame link hizo
 
QUOTE=Yahya M;Hata wewe ni sehemu ya mshiriki muhimu ni mawazo yako na si nani yupo studio jamani, watanzania mbona kazi ipo.

Ilo linaeleweka. Lakini nimeuliza ili nijue lead speakers ambao watanivutia kusikiliza mjadala,ambao watakua objective na si bias. Kwani kila mmoja akiwa lead speaker si tutakua tunapiga KELELE?!
 
 
Katiba ya sasa hivi ni ya kizazi kileeeeeee kilicho pita na imekuwa na viraka viraka mno mpaka inakosa mweleko. Tunahitaji Elimu kwanza kwa umma kuhusu katiba mpya nini kiwemo na nini kiondolewe na vile vile jamii inabidi iandaliwe kupokea hiyo katiba mpya. Hii ya sasa imepitwa na wakati maana sasa hivi dunia inapiga hatua katika sayansi ya teknolojia sisi tumeng'ang'ania katiba ile ile ya zamani.
Serikali inabidi ijipange jinsi gani itafanikisha zoezi zima la elimu kwa watanzania juu ya ujio wa katiba mpya ihusishe taasisi mbali mbali, mashirika na wanaharakati ili tupate katiba isiyo kuwa na manung'uniko pande zote katika jamii.
 
watanzania vijijini wanakufa kwa njaa toa mijadala ya kuwakwamua kiuchumi

Wanakufa kwa njaa kwa kukosa uongozi bora.

Uongozi wa kubebana ndo umetufanya tufike hapa tulipo angalia sasa mfumuko wa bei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…