Mjadala wa Katiba Mpya on Star TV this Sunday

Mjadala wa Katiba Mpya on Star TV this Sunday

Kama tulivyoahidi wiki iliyopita, elimu ya ulazima wa Katiba mpya kwa Watanzania itatolewa kupitia mjadala huu hapo kesho kuanzia saa 1 na dk 3O asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI.
WanaJF Micahngo na mawazo yenu yanakaribishwa na hatutasita kuyatumia kwa manufaa ya umma kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki makini na wa kipekee wiki iliyopita
Yahya M

Ukisema elimu ya ulazima una maana gani.Labda ungefafanua.Hata hivyo mjadala wa muda mfupi kiasi hicho hauzi kusaidia kutoa elimu,kwanza wangapi wana TV?Elimu ya uraia kwa ujumla inahitajika.Swali ni kwamba nani atatoa elimu hiyo?Lakini jambo la msingi hapa ni kwamba swala la katiba kwa serikali makini sio la kusukumwa sukumwa,kupangiwa mijadala nk.Ni issue ya kutekelezwa kwa wakati.Huu sio wakati wake,swala hili limepitwa na wakati sana.Lilipashwa kutekelezwa siku nyingi sana.Serikali ya kikwete ikae na wadau wote ili tupate katiba mpya haraka.Mambo mengi yanakwenda hovyo kwa sababu ya katiba tuliyo nayo.It's so irrelevant to our situation.
 
and this time is not perfect at all washauri wenzako na management muanzishe tuongee mchana au hata jioni this time especiall sundays watu wamepumzika au wengine wako church, na baadhi wamelala because of previous day hangovers
 
Viongozi walioko madarakani hawataki kuona kama kuna tatizo la msingi la kuwa na katiba mpya kwa wakati tulio kuwa nao! Na wanafanya hivyo si kwa sababu hawatambui umuhimu wa katiba mpya! Wanafanya hivyo kwa kuwa iliyoopo inaendana na matakwa yao na uroho wako wa kutaka kuendelea kuwa madarakani kwa njia zozote iwe hila, ghiriba au uchakachuaji.

Inasikitisha viongozi weledi wa mambo ya sheria ikiwemo majaji na mh Mkapa achilia mbali wanaharakati wamepaza sauti kuwa katiba mpya ina umuhimu wa kipekee na inahitajika kukidhi mazingira ya sasa lakini waziri wa katiba na sheria anajitokeza bila aibu akisema hakuna haja ya katiba mpya na iliyoopo inajitosheleza! Ana tuona watanzania ni majuha?! Anaona kuwa katiba iliyoopo inatosha kwa kuwa inakidhi mahitaji ya viongozi na chama tawala na si sisi wananchi tunao umia kwa kuwa na katiba ambayo haija shirikisha wananchi walio wengi katika mchakato wake.

Amani ya tanzania ya sasa ijayo iko mikononi mwa katiba mpya! Hii ya sasa ikiendelea kushikiliwa na viongozi wakiendeleza ukiziwi itakuja kutupelekea kwenye machafuko kama Kenya.
Katiba mpya si hitaji la viongozi wa kisiasa na lisichukuliwe kisiasa! Ni hitaji la watanzania tunao taka kuona maendeleo chanya ya kidemokrasia, kijamii, kiuchumi na kitamaduni.

Nawasilisha.
 
Yahya,
Mara nyingi tunashuhudia viongozi wetu wakiiweka ajenda ya katiba kisiasa zaidi, na tena hujiri pale tu kuwapo na mpenyo fulani wa kuibukia kisiasa au kujilinda kisiasa kwa nafasi zao (nje ya chama tawala)hususan katika chaguzi ndogo, chaguzi kuu, mipasuko ya kisiasa itokeapo ama katika chaguzi za ndani ya vyama vya siasa ndipo mambo haya muhimu huwa na nafasi. Ni vema tukajijengea utamaduni mahsusi sasa wa kuyazungumzia masuala muhimu na nyeti ya kitaifa kwa kupata maoni ya wananchi na kuyaheshimu ikiwemo katiba ya nchi yetu.
Lakini je! Ni kweli watanzania tunasubiri mpaka kuwepo na jambo fulani ndipo tudai katiba yetu ibadilishwe? Ama je! Tunahitaji katiba ibadilishwe pale tu wanasisa tunaowahusudu wanaposhindwa katika jambo fulani ndipo dai la katiba mpya lichomoze?
Binafsi nadhani jibu ni HAPANA, tusigeuze suala la katiba liwe kama UA (flower)…'huchomoza na kusinyaa'. Bali suala la katiba ya nchi yapaswa kuwa ni jambo kuu la kitaifa kwa mustakabali mzuri wa ustawi wetu na vizazi vyetu, iwapo hatutakuwa na njia bora za kusikiliza wananchi tunataka nini (kupitia maoni)…basi yaweza kuwa ni hasara kubwa tena yenye matokeo yenye mlengo wa uvunjifu wa amani siku za usoni.
Tumeshuhudia tume HALALI zikiundwa na serikali katika kutoa maoni ya wananchi juu ya mambo muhimu ikiwamo katiba, mfano wa tume hizo ni ile ya hayati Nyalali na ile ya jaji Kissanga. Matokeo ya wananchi kupitia tume hizi mbili tena kwa nyakati tofauti ilikuwa ni dhihirisho tosha sana kutambua nini chapaswa kufanywa na watawala katika kuheshimu nguvu ya wananchi juu ya marekebisho ya katiba mpya. Siku ya uhuru mwaka huu…mzee wetu balozi H.Mbitta akiwa katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo fulani hapa nchini alitoa angalizo la mahitaji ya katiba mpya, akifafanua kwa kusema katiba iliyokuwepo haikidhi hali ya sasa ya wananchi na ujumla wake. Rais mstaafu nae amepata kutoa tamko lenye mlengo wa hitajio la katiba mpya, alitoa angalizo hilo hivi karibuni katika moja ya khotuba yake iliyosomwa na balozi Mulamula(kama sijakosea jina hili). Hizi zatosha kuwa ni ishara za viongozi wastaafu wa nchi hii wakihitaji mabadiliko ya katiba ambapo wanaona umuhimu huo baada ya kung'atuka madarakani.
Hapa nchini hakuna jitihada za makusudi za kudai katiba mpya, imekuwa ikisomeka kwa wanasiasa mbalimbali wakitoa hoja za kudai katiba mpya kwa kila mmoja kivyake,,hakuna muunganiko wa nguvu ya pamoja na kutoa tamko hata ikibidi maandamano rasmi ya kudai katiba mpya,,na ikibidiiiii…..kuwepo na hamasa miongoni mwa viongozi kushinikiza nchi nzima kufanya maandamano ya amani katika kufikisha ujumbe murua kwa walengwa ili hatua mbadala kuchukuliwa na hatimae kuzaa tena matunda kwa njia ya MAONI YA WANANCHI kwa kudai katiba mpya
Tunahitaji katiba mpya kwa ustawi wa taifa letu na rasilimali zake kiujumla.
NAWAKILISHA !!!
 
wewe unaonekana ni mgeni au ni mbishi tu au ni pretender blind, watu kama ninyi hamtakiwi katika jamii hii ya sasa, je kuna kuna nani asiyejua kuwa watanzania wanahitaji katiba?? ninyi ndio wasomi then mnaakiti kiasi hicho je walio vijijini wafanye nini? unataka hadi mleta ,maada umvunje moyo? ndio maana tunasema waafrika tuna mioyo migumu na mibaya sana maana tunaona hali halisi lakini tumejaa unafiki zaidi ya vitendo. kila siku watu wanaongelea swala la katiba hata humu kuna mada kibao sana na watu wakitafuta intermediate kwa ppetition ,then watu wanajitolea na kuanzisha mada very sensitive to our nation badala ya kuwa-encourage na kuwa-support mnaanza kuwa jibu majibu ya kitoto.Be a great thinker before u crap
watanzania vijijini wanakufa kwa njaa toa mijadala ya kuwakwamua kiuchumi
 
Waiting for your call brother, last week it was worth of salt despite some few technical problem with connection, but I appreciate.
Thank you in advance
Yahya mimi ningefurahi sana kama mngekuwa mna-link hiyo mijadala hata kwenye RFA maana watu wengi watz wanasikiliza RFA maana hawana TV, kuna mjadala fulani mliuweka kwenye tv na redio. Ulikuwa ule mjadala wa fedha za majimboni kwa wabunge. Mimi nilikuwa kijijiniambako hakuna tv, infact hata mother ambaye yuko kule kasulu kijijini alisikiliza na alifurahi sana. Hivyo ninapendekeza mjadala huu muhimu uwe pia kwenye redio ili hata huko ambako hawana tv wasikilize. Nitafurahi sana kama mchango huu utasikilizwa.
 
and this time is not perfect at all washauri wenzako na management muanzishe tuongee mchana au hata jioni this time especiall sundays watu wamepumzika au wengine wako church, na baadhi wamelala because of previous day hangovers
Na mimi napata shida sana asubuhi kuwahi kipindi hiki
 
Star TV ni channel ambayo naiappriciate, ningeshauri hata channel zingine zingine ziungane na Star TV kwenye kuwaelimisha watz maana ndio kazi ya vyombo vya habari. Star tv dua za watz ziko pa1 nanyi.
 
Kwani katiba ya sasa haitoshi?

Ingekuwa vizuri akaleta mjadala wa kuleta maendeleo Tanzania

kwani Hujui Yahya ni mwandishi tuu wa habari??? Yeye anaalika watu waongee.. kazi yake kutayarisha maswali tuuu sasa unapayuka yasikuhusu... Big Up Yahya yaani hata siamini kama hii TV ya mzee Diallo inatumika kwa manufaa ya wananchi wa TZ kiasi hiki...
 
watanzania vijijini wanakufa kwa njaa toa mijadala ya kuwakwamua kiuchumi

sababu kuu ya wao kufa kwa njaa ni katiba mbovu inayotumika kusimamia misingi ya utawala wa nchi. Katiba ya sasa haiwapi wananchi fursa ya kuhoji kwani nini wanakufa njaa ili hali tanzania ni nchi yenye mali nyingi. Tunataka katiba itakayowapi fursa ya kuhoji mambo mbalimbali ya msingi na kuweka utawala wenye masilahi kwa wananchi.
 
Wa sasa umezidi angalia bei ya mafuta angalia bei ya sembe, angalia bei ya saruji.

Umesikia kwa Gadafi hapo bei ya petroli ni Tsh.250/kwa lt bongo hapa dah uongozi umeoza huu


Kitiba imetuongoza tokea kipindi wew umeaaliwa umekulea mpaka umwfika ulipo

QUOTE=JEYKEYWAUKWELI;Mfumuko wa bei ulikuwepo tokea awamu ya kwanza.

Pia katiba hii ipo toka awamu ya kwanza!


hii katiba toka awamu ya kwa nza ipo mabadiliko yamefanyika na imeboleshwa kwanini unataka serikali ibadilishe??

Kasome uelewe katiba maana yake ni nini? na ina manufaa gani kwa mtanzania. Nina imani kama uelewa wako ni mzuri utapenda hiyo katiba ije sasa hivi na siyo kuijadili maana ni suala lililowazi. Lakini kuijadili ni sehemu ya elimu ili watu wapate kujua umuhimu wake nawe ukijumuishwa. Kama utakuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa hapo utakapo kuwa na ufahamu utakiri kuwa ni kutokana na mfumo mbovu wa utawala ulioletwa kwa kuwa na katiba mbovu ndiyo maana kuna njaa vijijini.


katiba inaeleweka hakuna haja ya kuisoma tena

sio kila mtu anaona kama unavo ona wewe!
akili yako imekamatwa na haiko huru kwa hiyo kila kitu kwako ndani ya katiba ya sasa ni "vema"
Atleast TUMIA AKILI SIKU MOJA MOJA BASI


ya kwako itakuwa mgando mana utakuwa hujui hata katiba tuliyonayo inakusadiaje\//

baada ya kupata katiba mpya tutajadili maendeleo Tanzania. sasa hatuwezi kujadili maendeleo na madowans,maiptl,maf is Adi kibao...mpaka tuyanyonyoe manyoya maf is Adi ndo tunaweza kuendelea.
kama huna uwezo wa kujadili katiba tulia tuli mpaka tukiipata tutakuamsha tujadili pamoja maendeleo ya nchi hii.


tujadili maendeleo kabla ya katiba

Wewe Kananihii ulale acha mjadala wa wakubwa.....

wewe ndo ulale mana huju katiba ni nini

wewe unaonekana ni mgeni au ni mbishi tu au ni pretender blind, watu kama ninyi hamtakiwi katika jamii hii ya sasa, je kuna kuna nani asiyejua kuwa watanzania wanahitaji katiba?? ninyi ndio wasomi then mnaakiti kiasi hicho je walio vijijini wafanye nini? unataka hadi mleta ,maada umvunje moyo? ndio maana tunasema waafrika tuna mioyo migumu na mibaya sana maana tunaona hali halisi lakini tumejaa unafiki zaidi ya vitendo. kila siku watu wanaongelea swala la katiba hata humu kuna mada kibao sana na watu wakitafuta intermediate kwa ppetition ,then watu wanajitolea na kuanzisha mada very sensitive to our nation badala ya kuwa-encourage na kuwa-support mnaanza kuwa jibu majibu ya kitoto.Be a great thinker before u crap

crap

kwani Hujui Yahya ni mwandishi tuu wa habari??? Yeye anaalika watu waongee.. kazi yake kutayarisha maswali tuuu sasa unapayuka yasikuhusu... Big Up Yahya yaani hata siamini kama hii TV ya mzee Diallo inatumika kwa manufaa ya wananchi wa TZ kiasi hiki...

Yahya atakuwa katumwa

sababu kuu ya wao kufa kwa njaa ni katiba mbovu inayotumika kusimamia misingi ya utawala wa nchi. Katiba ya sasa haiwapi wananchi fursa ya kuhoji kwani nini wanakufa njaa ili hali tanzania ni nchi yenye mali nyingi. Tunataka katiba itakayowapi fursa ya kuhoji mambo mbalimbali ya msingi na kuweka utawala wenye masilahi kwa wananchi.


Katiba hii imetusadia sana maendeleo tumepata chini ya CCM
 
YAHYA M,

Kwanza nikupeni shime wewe na waandaji wengine kuliona hili la katiba mpya kama high priority, lakini pia niwape shime kwa kusimama mstari sahihi manake wana habari wengine ama hawajui ama ni wanafiki -wameshindwa kujua kwamba media ni mhimili wa nne baada ya bunge, mahakama na executives(serikali). Mawazo
1. Serikali lazima itambua kuwa KATIBA MPYA ni lazima kwa sasa kuepusha uvungifu wa AMANI
2. Katiba ya sasa ni kandamizi kwa mfano inatoa fursa TUME YA UCHAGUZI kuteua rais wa nchi ama kwa kupenda au kushinikizwa manake ikitangaza hakuna chombo chochote kinaweza kuhoji
3. Katiba ya sasa ipo kimfumo wa chama kimoja kwamba Rais anweza kuamua mambo mengi bila kuhojiwa mfano idadi ya mawaziri na wizara
4. Katiba ya sasa inaruhusu mbunge kuwa waziri hivi mbuinge kama waziri alawahudumaia vipi wananchi wake au ndio kusema atatumia uwaziri wake kufuja mali ya umma kwa ajili ya jimbo?
5. Katiba ya sasa imeweka nyasifa ambazo tunaona hazina tija kwa manufaa ya nchi -mfano mkuu wa wilaya na mkurugenzi, naibu waziri na kaitibu wa wizara, huu ni ufujaji wa mali na rasilimali za umma.
6. Katiba ya sasa inakandamiza haki ya kuwa na mgombea binafsi huu ni ukandamizaji why???
7. Katiba ya sasa inamruhusu RAIS kuteua wakuu wa tume ya uchaguzi -huu ni uzandiki na usultani -ibadilike
8. Katiba ya sasa inavitaka mamulaka kama PCCB kumutumia rais kama atakavyo-inaripot kwa rais -kwanini PCCB isiwajibike kwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, hii ni pamoja na CAG
9. KATIBA ya sasa inaruhusu viti maalumu huu ni uzandiki na ufujaji wa mali ya umma, wanamwakilisha nani??????
10. Katiba ya haitoi uhuru wa principles of separation of powers, waziri mkuu na mawaziri wanatokana na bunge na ni wabunge? watawala wengi wako juu ya sheria mahakama haipo huru -huu ni uzandiki katiba hii haitufai.

ninayo mengi lakini la mwisho tunamwomba RAIS ampangie kazi nyingine Celina Kombani ameonesha toka mwanzo hawezi kuongoza wizara hii, ni mchapa kazi lakini hapa amechemesha hawezi kuanza kazi kwa matusi kwa kauli yake ya kibabe na kinafiki. Ninaomba usome mawzo yangu tafadhari usichakachue manake itakuwa hakuna maana ya kuanzisha maada hii halafu uchakachue michango yetu -please tunaimani una dhamira ya kweli kwa Tanzania. Yangu maskio hiyo Kesho.-STAR TV
 
yahya vp kuhusu kauli ya mheshimiwa waziri kombani kwamba serikali haina pesa? niulizie hapo.
 
watu wa mwanza moto, jamaa huyi ana pointi sana tunahitaji watu kama hawa vichwa sio akina kafulila wanaingia kwa kukariri
 
Yahya mimi naona kama kungekuwa na mgeni anaewakilisha mawazo ya serikali ingependeza. Ili tusikie serikali inasemaje. Mjadala ni mzuri hususani hao wageni wa hapo Mwanza,wapo very objective.
 
Back
Top Bottom