Mjadala wa Katiba Mpya on Star TV this Sunday

Mjadala wa Katiba Mpya on Star TV this Sunday

Mbona habari roborobo? Taja wageni waalikwa tafadhali.

Naam, tuambie. Hatutaki wale wale wachovu wanaoshambulia personality ya msemaji badala ya hoja aliyotoa msemaji. Namaanisha hatutaki kafulila wala yule mwenzake wa cuf. Hii mada ni muhimu na watu wengi tunaitaka lakini hawa watatuboa
 
Mfumuko wa bei ulikuwepo tokea awamu ya kwanza

Wa sasa umezidi angalia bei ya mafuta angalia bei ya sembe, angalia bei ya saruji.

Umesikia kwa Gadafi hapo bei ya petroli ni Tsh.250/kwa lt bongo hapa dah uongozi umeoza huu
 
Kwanini huona kuwa hata kwa katiba yetu ya sasa watu wamekwamuliwa chini ya ccm??
mimi sijaona,na nina imani wewe pia hujaona ndo maana ukasema "WATANZANIA VIJIJINI WANAKUFA KWA NJAA"-kwa wachache walionufaika ni wale walio ndani ya chama
 
Ni kweli hatuna pesa? Kama Mama Kombani anavyodai?

Halafu hawa mawaziri waliopita shule za kuunga-unga (kama huyu Kombania). Hivi kusema serikali haina pesa maana yake nini? Kwa nini asitoe tarakimu. Tukajiridhisha kweli kwamba kwa hali ya nchi yetu, kweli pesa alizosema huyu mama hakuna pa kuzipata. Kwanini CCM hawataki kukubali kuwa Watanzania wa leo si wa mwaka 47?

Kama tuliweza kuwalipa Richmonduli Tsh. 152 000 000 kwa siku, tunashindwa vipi kupata pesa za kufanikisha suala nyeti kama Katiba mpya yenye kukidhi mahitaji ya Watanzania?

Upo wapi uhalali wa kujiita nchi huru inayojitawala? Kuna wakati tunakuwa wakali wenzetu wa nje wakitaka kuingilia mambo yetu na huwa tunawatamkia 'wasituingilie katika maswala yetu ya ndani', kwa hili la serikali haina pesa (kuendesha mambo yetu ya ndani kama katiba) limekaa sawa? Au hata pesa za kurekebisha katiba yetu tunategemea kutoka kwa wahisani?

Ni hayo tu.
 
QUOTE=JEYKEYWAUKWELI;Mfumuko wa bei ulikuwepo tokea awamu ya kwanza.

Pia katiba hii ipo toka awamu ya kwanza!
 
watanzania vijijini wanakufa kwa njaa toa mijadala ya kuwakwamua kiuchumi

Kasome uelewe katiba maana yake ni nini? na ina manufaa gani kwa mtanzania. Nina imani kama uelewa wako ni mzuri utapenda hiyo katiba ije sasa hivi na siyo kuijadili maana ni suala lililowazi. Lakini kuijadili ni sehemu ya elimu ili watu wapate kujua umuhimu wake nawe ukijumuishwa. Kama utakuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa hapo utakapo kuwa na ufahamu utakiri kuwa ni kutokana na mfumo mbovu wa utawala ulioletwa kwa kuwa na katiba mbovu ndiyo maana kuna njaa vijijini.
 
kama tulivyoahidi wiki iliyopita, elimu ya ulazima wa katiba mpya kwa watanzania itatolewa kupitia mjadala huu hapo kesho kuanzia saa 1 na dk 3o asubuhi katika kipindi cha tuongee asubuhi.
Wanajf micahngo na mawazo yenu yanakaribishwa na hatutasita kuyatumia kwa manufaa ya umma kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki makini na wa kipekee wiki iliyopita
yahya m

yahya napenda sana kuchangia mijadala sometimes hata live kama kuna uwezekano niambie utaratibu wa kuweza kushiriki kupitia studio za dar es salaam napenda sana yaani pia huwa nikipiga simu sipati line hata siku moja
 
Kama tulivyoahidi wiki iliyopita, elimu ya ulazima wa Katiba mpya kwa Watanzania itatolewa kupitia mjadala huu hapo kesho kuanzia saa 1 na dk 3O asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI.
WanaJF Micahngo na mawazo yenu yanakaribishwa na hatutasita kuyatumia kwa manufaa ya umma kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki makini na wa kipekee wiki iliyopita
Yahya M

YAHYA UNAWEZA KUNIPATIA UTARATIBU HUO THROUGH sabe_05@yahoo.com
 
Kama tulivyoahidi wiki iliyopita, elimu ya ulazima wa Katiba mpya kwa Watanzania itatolewa kupitia mjadala huu hapo kesho kuanzia saa 1 na dk 3O asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI.
WanaJF Micahngo na mawazo yenu yanakaribishwa na hatutasita kuyatumia kwa manufaa ya umma kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki makini na wa kipekee wiki iliyopita
Yahya M

Shukrani, muda umekaa vibaya kweli, wengine tutakuwa church!
 
Tazama post ya wiki iliyopita...Huu ni mwendelezo wa last week kama hukupata that means archieve hapa JF iondolewe

I think swali la wageni ni wakinanani ni zuri..... hata kama issue ipo kwenye archive its not bad kama ukitwambia pia hapa.... ofcourse ni mwendelezo lakini maybe lastweek someone was not interested lakini this week yupo so please wageni ni kina nani?
 
Kama tulivyoahidi wiki iliyopita, elimu ya ulazima wa Katiba mpya kwa Watanzania itatolewa kupitia mjadala huu hapo kesho kuanzia saa 1 na dk 3O asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI.
WanaJF Micahngo na mawazo yenu yanakaribishwa na hatutasita kuyatumia kwa manufaa ya umma kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki makini na wa kipekee wiki iliyopita
Yahya M

Ahsante,
Nchi yetu inaingia nusu karne punde huku tukiwa na katiba iliyotengenezwa mahsusi kwa watu mili.9 tu, hivi sasa nchi yetu ina takriban watu mil.42.
Katika muundo wa katiba tuitumiayo...kiujumla haikidhi hali ya wananchi kwa sasa ktika nnyanja zote za kiutawala, kiulinzi, kiuchumi, kijamii na hata kisiasa bali katiba hii iliyopo ni mahsisi kwa ajili ya wachache tu na wananchi ni kama wanaburuzwa na watawala.
Nchi yetu ni kisiwa cha amani, amani hii ni asili ya wananchi wa Tanzania, Wananchi wanapodai katiba mpya si kwa tamaa ya mambo fulani wategemeayo kimaslahi...bali ni katika mustakabali wa jamii iliyopo na maendeleo yake kiustawi wa ujumla. Haitoingilika akilini katika jamii ya wastaarabu watanzania ifikie hatua ya kudai katiba mpya kwa vurugu na kuvunja amani iliyopo ilhali ni jambo muhimu kwa ustawi wa taifa letu na raia wake, tuepushe yanayojiri nchi za wenzetu bali tuwe na angalizo jema kwa nchi yetu
Wananchi tumelalamika juu ya katiba, viongozi wastaafu serikalini wamelalama juu ya katiba, wanasiasa wanalalama juu ya katiba...JE TUSUBIRI NA HAWA WALIOPO MADARAKANI WAKISHASTAAFU NAO WAANZE KUDAI KATIBA KWA WARITHI WAO? KWA NINI ISIWE SASA?
Itapendeza watawala ifike muda sasa walione kwa macho mawili suala zima la katiba, wananchi wanataka nini ili kuweka misingi imara na madhubuti kwa muendelezo mwema wa taifa letu,,MABADILIKO YA KATIBA KWA SASA HAYAKWEPEKI...ILA KWA WENYE UCHU FULANI HAWAONI MANTIKI YA MABADILIKO YA KATIBA YA TANZANIA KWA SASA.
 
Kwanini huona kuwa hata kwa katiba yetu ya sasa watu wamekwamuliwa chini ya ccm??

sio kila mtu anaona kama unavo ona wewe!
akili yako imekamatwa na haiko huru kwa hiyo kila kitu kwako ndani ya katiba ya sasa ni "vema"
Atleast TUMIA AKILI SIKU MOJA MOJA BASI
 
Mfumuko wa bei ulikuwepo tokea awamu ya kwanza

hii ndio asili ya mtu juha....wewe ni juha unabwabwaja tu.......hata ukiwekwa kwenye chupa lazima unyooshe kidole.....

jitu hili bwana!!!!!!!!!!
 
sio kila mtu anaona kama unavo ona wewe!
akili yako imekamatwa na haiko huru kwa hiyo kila kitu kwako ndani ya katiba ya sasa ni "vema"
Atleast TUMIA AKILI SIKU MOJA MOJA BASI

huyu hata hajui kama ana akili.....ni mtu wa ajabu sana.....siku zote huwa anapinga mambo ya msingi ambayo hat wazee wake sasa hivi huko ccm wanatamani katiba mpya...... HE CANNOT THINK BEYOND THE NEXT MEAL!!
 
Ni mjadala mzuri Yahaya kipindi chenu cha Tuuongee Asubuhi endeleeni kukiboresha kimeanza kupata audience,kubwa kwa kweli mimi zamani Star TV haikuwa my favorite lakini mulivyo ripoti habari za uchaguzi na uchambuzi pamoja na makosa ya kibinadamu na kitaaluma kiujumla mimi niliwapa TK sasa nimekuwa teja wa kipindi hiki ,na mjadala kutokana yatakayoibuka kesho muyaendeleze munaweza mkawa na wageni mara moja kwa mwezi katika tuongee asubuhi mukakusanya yale yanayojitokeza kwenye hiyo mijadala mukaja mukatolea tathimini labada baada ya miezi sita au mwaka itaonyesha dira nzima
 
Ccm wanasikiliza hiyo mijadala................naomba na yule mama aliyesema utumbo ahudhurie ili asikie watz wanataka nini na sio ccm na yeye wanataka nin kwa sababu kwanza wanaongoza kiharamu na hatukuwa na imani na ilani yao japo wamechakachua.............wanaleta udini tunataka katiba ambayo itasisitiza uhuru wa kuabudu na sio serikali kubeba uislamu............
 
Kwani katiba ya sasa haitoshi?

Ingekuwa vizuri akaleta mjadala wa kuleta maendeleo Tanzania

baada ya kupata katiba mpya tutajadili maendeleo Tanzania. sasa hatuwezi kujadili maendeleo na madowans,maiptl,maf is Adi kibao...mpaka tuyanyonyoe manyoya maf is Adi ndo tunaweza kuendelea.
kama huna uwezo wa kujadili katiba tulia tuli mpaka tukiipata tutakuamsha tujadili pamoja maendeleo ya nchi hii.
 
Ccm wanasikiliza hiyo mijadala................naomba na yule mama aliyesema utumbo ahudhurie ili asikie watz wanataka nini na sio ccm na yeye wanataka nin kwa sababu kwanza wanaongoza kiharamu na hatukuwa na imani na ilani yao japo wamechakachua.............wanaleta udini tunataka katiba ambayo itasisitiza uhuru wa kuabudu na sio serikali kubeba uislamu............

mh,
how comes hapo imeingia kwa mada hii jamani...topic ya udini ni sumu kwa kila raia wa nchi hii na popote duniani, let's try to take some precautions kwayo ni hatari mno.
NAWASILISHA...
 
Back
Top Bottom