Kama tulivyoahidi wiki iliyopita, elimu ya ulazima wa Katiba mpya kwa Watanzania itatolewa kupitia mjadala huu hapo kesho kuanzia saa 1 na dk 3O asubuhi katika kipindi cha TUONGEE ASUBUHI.
WanaJF Micahngo na mawazo yenu yanakaribishwa na hatutasita kuyatumia kwa manufaa ya umma kama ambavyo tumekuwa tukifanya.
Natanguliza shukrani zangu kwa ushiriki makini na wa kipekee wiki iliyopita
Yahya M
Ahsante,
Nchi yetu inaingia nusu karne punde huku tukiwa na katiba iliyotengenezwa mahsusi kwa watu mili.9 tu, hivi sasa nchi yetu ina takriban watu mil.42.
Katika muundo wa katiba tuitumiayo...kiujumla haikidhi hali ya wananchi kwa sasa ktika nnyanja zote za kiutawala, kiulinzi, kiuchumi, kijamii na hata kisiasa bali katiba hii iliyopo ni mahsisi kwa ajili ya wachache tu na wananchi ni kama wanaburuzwa na watawala.
Nchi yetu ni kisiwa cha amani, amani hii ni asili ya wananchi wa Tanzania, Wananchi wanapodai katiba mpya si kwa tamaa ya mambo fulani wategemeayo kimaslahi...bali ni katika mustakabali wa jamii iliyopo na maendeleo yake kiustawi wa ujumla. Haitoingilika akilini katika jamii ya wastaarabu watanzania ifikie hatua ya kudai katiba mpya kwa vurugu na kuvunja amani iliyopo ilhali ni jambo muhimu kwa ustawi wa taifa letu na raia wake, tuepushe yanayojiri nchi za wenzetu bali tuwe na angalizo jema kwa nchi yetu
Wananchi tumelalamika juu ya katiba, viongozi wastaafu serikalini wamelalama juu ya katiba, wanasiasa wanalalama juu ya katiba...JE TUSUBIRI NA HAWA WALIOPO MADARAKANI WAKISHASTAAFU NAO WAANZE KUDAI KATIBA KWA WARITHI WAO? KWA NINI ISIWE SASA?
Itapendeza watawala ifike muda sasa walione kwa macho mawili suala zima la katiba, wananchi wanataka nini ili kuweka misingi imara na madhubuti kwa muendelezo mwema wa taifa letu,,MABADILIKO YA KATIBA KWA SASA HAYAKWEPEKI...ILA KWA WENYE UCHU FULANI HAWAONI MANTIKI YA MABADILIKO YA KATIBA YA TANZANIA KWA SASA.