Yahya,
Mara nyingi tunashuhudia viongozi wetu wakiiweka ajenda ya katiba kisiasa zaidi, na tena hujiri pale tu kuwapo na mpenyo fulani wa kuibukia kisiasa au kujilinda kisiasa kwa nafasi zao (nje ya chama tawala)hususan katika chaguzi ndogo, chaguzi kuu, mipasuko ya kisiasa itokeapo ama katika chaguzi za ndani ya vyama vya siasa ndipo mambo haya muhimu huwa na nafasi. Ni vema tukajijengea utamaduni mahsusi sasa wa kuyazungumzia masuala muhimu na nyeti ya kitaifa kwa kupata maoni ya wananchi na kuyaheshimu ikiwemo katiba ya nchi yetu.
Lakini je! Ni kweli watanzania tunasubiri mpaka kuwepo na jambo fulani ndipo tudai katiba yetu ibadilishwe? Ama je! Tunahitaji katiba ibadilishwe pale tu wanasisa tunaowahusudu wanaposhindwa katika jambo fulani ndipo dai la katiba mpya lichomoze?
Binafsi nadhani jibu ni HAPANA, tusigeuze suala la katiba liwe kama UA (flower)…'huchomoza na kusinyaa'. Bali suala la katiba ya nchi yapaswa kuwa ni jambo kuu la kitaifa kwa mustakabali mzuri wa ustawi wetu na vizazi vyetu, iwapo hatutakuwa na njia bora za kusikiliza wananchi tunataka nini (kupitia maoni)…basi yaweza kuwa ni hasara kubwa tena yenye matokeo yenye mlengo wa uvunjifu wa amani siku za usoni.
Tumeshuhudia tume HALALI zikiundwa na serikali katika kutoa maoni ya wananchi juu ya mambo muhimu ikiwamo katiba, mfano wa tume hizo ni ile ya hayati Nyalali na ile ya jaji Kissanga. Matokeo ya wananchi kupitia tume hizi mbili tena kwa nyakati tofauti ilikuwa ni dhihirisho tosha sana kutambua nini chapaswa kufanywa na watawala katika kuheshimu nguvu ya wananchi juu ya marekebisho ya katiba mpya. Siku ya uhuru mwaka huu…mzee wetu balozi H.Mbitta akiwa katika mahojiano ya moja kwa moja na kituo fulani hapa nchini alitoa angalizo la mahitaji ya katiba mpya, akifafanua kwa kusema katiba iliyokuwepo haikidhi hali ya sasa ya wananchi na ujumla wake. Rais mstaafu nae amepata kutoa tamko lenye mlengo wa hitajio la katiba mpya, alitoa angalizo hilo hivi karibuni katika moja ya khotuba yake iliyosomwa na balozi Mulamula(kama sijakosea jina hili). Hizi zatosha kuwa ni ishara za viongozi wastaafu wa nchi hii wakihitaji mabadiliko ya katiba ambapo wanaona umuhimu huo baada ya kung'atuka madarakani.
Hapa nchini hakuna jitihada za makusudi za kudai katiba mpya, imekuwa ikisomeka kwa wanasiasa mbalimbali wakitoa hoja za kudai katiba mpya kwa kila mmoja kivyake,,hakuna muunganiko wa nguvu ya pamoja na kutoa tamko hata ikibidi maandamano rasmi ya kudai katiba mpya,,na ikibidiiiii…..kuwepo na hamasa miongoni mwa viongozi kushinikiza nchi nzima kufanya maandamano ya amani katika kufikisha ujumbe murua kwa walengwa ili hatua mbadala kuchukuliwa na hatimae kuzaa tena matunda kwa njia ya MAONI YA WANANCHI kwa kudai katiba mpya
Tunahitaji katiba mpya kwa ustawi wa taifa letu na rasilimali zake kiujumla.
NAWAKILISHA !!!