Mjadala wa Katiba Mpya on Star TV this Sunday

mkenya aomba watz kuwe na tume ya taifa ya kubadilisha katiba kutenganisha mamlaka ya bunge/mahakama/mamlaka
 
YAHYA M.

Asante kwa kusoma maoni yangu kama nilivyoandika ninaomba mchakato huu uendelee moja kwa moja i can now trust you guys -big up.
 
Nawauliza wanasheria, je hamna jinsi yoyote ya kumlazimisha raisi kutolea tamko jambo linaongelewa na watu wengi, bila maandamano ?

Je waandishi wa habari hawana uhuru wa kumhoji raisi ili tujue msimamo wake ?
Je ni nani anayekwamisha mchakato wa kuandikwa katiba mpya ?maana viongozi wengi wamechangia na kukubaliana na umuhimu wa kuwa na
katiba mpya.
 
QUOTE=DENYO;

Asante kwa kusoma maoni yangu kama nilivyoandika.

Lakini amechakachua hoja yako kwa kutosoma hoja ya Celina Kombani na Mkwere.
 
Yahya M,
Tanesco wameshafanya vitu vyao. Hata hivyo mchango wangu ni huu:
Power separation haipo kwenye katiba ya sasa, natoa mifano miwili:
1. Kazi mojawapo ya Bunge ni kuisimamia serikali, mawaziri wote wanapokuwa wabunge, mathalani wakiwa bungeni wanakuwa ni sehemu ya bunge au serikali? Nani anamsimamia mwenzake??
2. Kazi mojawapo ya Bunge ni kutunga sheria, lakini sheria nyingi zinatungwa na serikali na kupelekwa bungeni kama muswada na bunge likipitisha bado muswada hauwi sheria mpaka rais ausaini. Hapa anayetunga sheria ni nani? Bunge si kama rubber stamp?? Na kama sheria hiyo ni ya uhalifu na mahakama ikamtia mtuhumiwa hatiani na anapaswa kunyongwa, hawezi kunyongwa mpaka rais asaini. Uhuru wa mahakama uko wapi??
 

Pole sana mdau, tumeyachukua mawazo yako na kwa kuwa tunajipanga kuwa na mjadala huo sehemu ya pili kwa kuwashirikisha Jaji Joseph Warioba na Profesa Issa Shivji tutayatumia mawazo hayo
Yahya
 
QUOTE=DENYO;

Asante kwa kusoma maoni yangu kama nilivyoandika.

Lakini amechakachua hoja yako kwa kutosoma hoja ya Celina Kombani na Mkwere.

Lakini bado hoja ilijotokeza kutoka Arusha kama taaluma inavyoelekeza na tukayaacha Mdau. Ila nashukuru sana kwa michango yenu. Tumeanza mcahakato kufanikisha kumpata Jaji Warioba na Prof Shivji wiki ijayo ili kuendeleza mjadala huo tena katika awamu nyingine.
Yahya
 
YAHYA M.

Asante kwa kusoma maoni yangu kama nilivyoandika ninaomba mchakato huu uendelee moja kwa moja i can now trust you guys -big up.

Shukrani Mkuu. I know you've accepted my apology kwa kucahakachua kidogo kijisehemu katika maoni yako pevu.
Nashukuru sana kwa ushiriki wenu Mzuri.
Pamoja we can bring changes
Yahya
 
mkenya aomba watz kuwe na tume ya taifa ya kubadilisha katiba kutenganisha mamlaka ya bunge/mahakama/mamlaka

Umeliona hilo mkuu, hii ni changamoto kubwa kwa serikali yetu kutambua kuwa THE WORLD IS WATCHING
Shukrani kwa Mchango wako
Yahya
 

Finally umetoa mchango. hitilafu za lugha zisikupe shaka Mkuu.
Yahya
 


Hii part nimeireserve kwa ajili ya next week Mkuu
Shukrani sana kwa kuchukua muda wako kwa manufaa ya Umma kujenga hoja ya msingi kwa kiasi hiki
Yahya
 
Umeliona hilo mkuu, hii ni changamoto kubwa kwa serikali yetu kutambua kuwa THE WORLD IS WATCHING
Shukrani kwa Mchango wako
Yahya

Sisi ambao tulikuwa safarini tunaomba kujua ni nini kilichojiri.

Kutokana na kile kinachojili tunaomba kujua sisi ni kizazi cha ngapi katika maisha ya Tanzania tuweze kujua kama tunaweza kuandika historia.
 
and this time is not perfect at all washauri wenzako na management muanzishe tuongee mchana au hata jioni this time especiall sundays watu wamepumzika au wengine wako church, na baadhi wamelala because of previous day hangovers

Maoni yamefika Mkuu, pia linatusumbua sana hili ni kwa kiwango gani tutaifikia audience yote kwa ujumla maana hapa pia tunaangalia NICHE, lakini bado tunaumiza vichwa kuwezesha mijadala kama hii kuwafikia walengwa hasa lakini sambamba na muda wa ratiba ambao pia unazingatia mambo mengi ya kiutendaji na commercial aspect
Shukrani kwa changamoto
Yahya
 
Yahya m shukrani mkuu tupo hewani we achana na huyu jeykey wa uongo kama angekuwa wa ukweli ange tumia jina lake halisi kama dr slaa,zitto,na wengine wengi, jey key wa ukweli wewe ndio unafaidika na hiyo katiba feki wananchi walisha sema kwenye tume ya jaji kisanga na jaji nyalali wanahitaji katiba. ebu mtizame samweli sitta star tv sasa hivi anahojiwa pole mchumia tumbo weeeeeee
 

Shukrani sana kwa mchango huu Mkuu
Yahya M
 
Nichukue fursa hii kuwashukuruni sana wanaJF wote walioshiriki katika mada hii, Mawazo na michango ilikuwa mingi na muda wetu studio ni mfinyu ila tumejitahidi kwa uwezo wetu kuyatumia mawazo yote kama yalivyo. Wiki ijayo tunakusudia tena kuwa mjadala juu ya Katiba sehemu ya pili. Na safari hii kwa kwenda hatua nyingine ya kuwashirikisha Jaji Joseph Warioba na Profesa Shivji na waandishi wa Habari wakomavu Jijini Mwanza. Litakapopata baraka za kiofisi na taratibu kukamilika kwa mialiko hiyo na uthibitisho tutawajulisha wanaJF.
Nashukuru sana kwa sauti zenu kwa Umma
Pamoja tutaleta Chachu ya Mabadiliko katika Taifa letu kwa masilahi ya Umma.
Jumapili Njema
Yahya M
 

Tuliposikia hotuba ya JK juu ya namna ya kufinance uchaguzi ndani ya vyama katika ushiriki wa chaguzi tulifikiri yalikuwa ni mawazo ya msingi kwa Taifa hili kutokana na kile kilichochukuliwa kama matumizi makubwa kwa vyama vya siasa pasipokujua ni wapi fedha hizo zinapatikana. Kuletwa kwa sheria ya gharama za uchaguzi ilionekana kama utekelezaji wa hoja hiyo lakini hapa ndipo tunagundua kuwa hata jambo jema laweza kutekelezwa kwa maslai ya kikundi cha watu. 'Impartiality' sheria inakidhi matakwa ya watu wachache. Pia sheria nzuri pasipo taasisi madhubuti kusimamia ni kazi bure na hapa tumeona PCCB ikituangusha, tumeona Police wakituangusha, tumeona NEC ikituangusha, tutaona mahakama zitakavyotuangusha. Je, hakuna vipengele muhimu katika katiba ambavyo vimeshindwa kupata meno kutokana na kushindwa kwa taasisi zilizopo? Je, katiba mpya katika mfumo huu wa watawala kung'ang'ania na kutokuheshimu sauti na kauli za watanzania itatufaa nini? Je, katiba mpya haiwezi kuwa kama sheria ya gharama ya uchaguzi? Swala la katiba mpya liwe la watanzania na si la serikali ya CCM na lazima watanzania hao wajitwalie mamlaka ya kitaifa kama wasimamizi wakubwa wa nchi hii. Ni lazima Bunge liwe la watanzania, wanasheria wawe watanzania, waandishi wa habari wawe watanzania na viongozi wastaafu wawe watanzania kwa maana ya uzalendo. Hatuwezi kupata katiba mpya wakati tumegawanyika. Baadhi ya waandishi wakifanya kazi za watawala, watatupa katiba ya wanao tutawala, wanasheria wanaoishi kwa migongo ya watawala watatupa katiba ya watawala, wasomi waliyowekwa karibu na watawala watatupa katiba ya watawala. Litakuwa ni pigo pale ambapo watawala wataweka nguzo zao katika katiba na hata katika taasisi za kusimamia katiba. Ni lazima watanzania waelimishwe ili kutambua wajibu wao umuhimu wa katiba mpya na taasisi zinazosimamia utekelezaji wake. Ni lazima watanzanie watambue kuwa wao ndio chimbuko la watawala na wanaotoa mamlaka ya watawala badala ya kujiona kama watawaliwa na kuwafanya watawala kuwa ndiyo chimbuko la mamlaka na utawala wao. Tukifika hapo hakika katiba mpya itakuwa ni fulsa ya maendeleo na democrasia ya kweli kwa watanzania. Tusichukulie katiba mpya kama mlango wa siasa za upinzani bali njia ya kumtoa mtanzania ktk hali duni kuelekea kwenye maendeleo sahihi na demokrasia yenye tija kwa taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…