Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
- Thread starter
-
- #21
Nilivyokuelewa, uraia wa nchi moja ni bora zaidi ya uraia pacha. Ni sawa?A matter of international law.
Mimi kama raia wa Marekani, nikiwa Tanzania kama raia wa Marekani tu bila uraia pacha, serikali ya Marekani ina uwezo mkubwa sana wa kunitetea kama raia wake ambaye nina uraia wa Marekani tu.
Nikiwa na uraia pacha, wa Tanzania na Marekani, serikali yangu ya Marekani inapata vizingiti fulani vya kisheria kunitetea nikipata matatizo Tanzania.Kwa sababu ya uraia wangu pacha wa Tanzania na Marekani.
Kwa nchi, kiuchumi, uraia pacha karibu mara zote ni mzuri zaidi ya uraia wa nchi moja tu.Nilivyokuelewa, uraia wa nchi moja ni bora zaidi ya uraia pacha. Ni sawa?
Kijana wangu nashukuru kwa kuleta mada hii namimi napenda kuchangia ili kutoa elimu;Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mijadala kuhusu Tanzania kuruhusu uraia pacha. Wapo wanaopendekeza Tanzania kama nchi ikubali uwepo wa uraia pacha ili kuzipata faida zitokanazo na uraia wa aina hiyo. Wapo wenye mtazamo kuwa muda wa Tanzania kuwa na uraia pacha bado haujafika. Hivyo basi, wanauunga mkono msimamo wa Serikali wa kutokubali na kuanzisha uraia pacha hapa nchini.
Uraia ni jambo la kisheria. Endapo Serikali itaridhia kuanzishwa kwa uraia pacha, lazima sheria inayosimamia masuala ya uraia ifanyiwe marekebisho kukidhi matakwa ya mabadiliko hayo. Ilivyo sasa, uraia unaokubalika hapa nchini ni uraia wa nchi moja: kama ni raia wa Tanzania au la. Raia wa Tanzania, ilivyo sasa, haruhusiwi kuwa raia wa nchi nyingine yeyote duniani. Ikitokea hivyo, raia husika itampasa kupoteza uraia mmojawapo: ima wa Tanzania au wa hiyo nchi nyingine.
Kwa kuwa mimi si mbobezi wa masuala ya kimataifa na kiuraia na naamini JF ni nyumba ya wabobezi wa mambo hayo na mengine, naomba kuwasilisha hoja na wito kwa waungwana kuziainisha faida na hasara za kuwa na uraia pacha hapa nchini kwetu Tanzania. Kujua faida na hasara kutachochea au kupooza wito wa wananchi wa kutaka uwepo wa uraia pacha kwa watanzania.
Karibuni waungwana wa JF...
Kijana wangu nashukuru kwa kuleta mada hii namimi napenda kuchangia ili kutoa elimu;
Faida za uraia Pacha; humuwezesha mtu kupata huduma za kijamii nchi yoyote ambayo ana uraia.Kama uraia wa Tanzania na Marekani,utanufaika na kupata elimu,huduma za afya bila kubaguliwa. Kwa Mtanzania mwenye uraia pacha hapa hunufaika na huduma bora toka nchi zilizoendelea na kuna fursa ya nchi kama Tanzania kunufaika na utaalamu na ujuzi wa raia hawa waliopata ujuzi nje ya nchi na pia kwa upande wa gharama za matibabu hili litaweza kupunguza gharama kwa Tanzania.
Pili,mtu mwenye uraia pacha anaweza kupiga kura au kuligiwa kura kupata uongozi nchi yoyote. Hapa kuna fursa kwa nchi kwamba kama mtu huyu ana utaalam na hana nia mbaya atakuwa msaada lakini kama mtu huyu atakuwa na nia mbaya au ni pandikizi kuna hatari kubwa ya sana kiusalama.Ni ngumu kutambua je huyu mtu ni mtiifu kwa taifa gani?
Tatu,mtu mwenye uraia pacha huweza kumiliki mali katika nchi yoyote atakayo.Ni fursa kwamba mali hususani nyumba kupata soko la uhakika ila kuna hatari ya kwamba watu hususani pale anapokuwa na maslahi ya kihasusi kununua mali na kisha kutozitumia,hii huathiri uchumi au kuitumia kwa maslahi ya ujasusi ya nchi nyingine.
Nne, mtu mwenye uraia pacha analipa kodi kwa zote ambazo ana uraia.Kwa nchi kama Tanzania hii ni fursa ya kukusanya kodi kutoka kwa madiaspora wote waliopo ulimwenguni.
Ufugwa na watawalaWafuge uone moto wake
Wengine kwa sasa hata kutembea tunaishia JF.Security reasons sio poa..Kama Nyarandu Ana green card TU wakati wa uchaguzi wa 2015 alijinadi Wamarekani wanataka awe raisi..nyie fanyeni kazi huko FBI etc huku mje kutembea tu ..Labda wanamichezo POA...
§337.1 Oath of allegiance.Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mijadala kuhusu Tanzania kuruhusu uraia pacha. Wapo wanaopendekeza Tanzania kama nchi ikubali uwepo wa uraia pacha ili kuzipata faida zitokanazo na uraia wa aina hiyo. Wapo wenye mtazamo kuwa muda wa Tanzania kuwa na uraia pacha bado haujafika. Hivyo basi, wanauunga mkono msimamo wa Serikali wa kutokubali na kuanzisha uraia pacha hapa nchini.
Uraia ni jambo la kisheria. Endapo Serikali itaridhia kuanzishwa kwa uraia pacha, lazima sheria inayosimamia masuala ya uraia ifanyiwe marekebisho kukidhi matakwa ya mabadiliko hayo. Ilivyo sasa, uraia unaokubalika hapa nchini ni uraia wa nchi moja: kama ni raia wa Tanzania au la. Raia wa Tanzania, ilivyo sasa, haruhusiwi kuwa raia wa nchi nyingine yeyote duniani. Ikitokea hivyo, raia husika itampasa kupoteza uraia mmojawapo: ima wa Tanzania au wa hiyo nchi nyingine.
Kwa kuwa mimi si mbobezi wa masuala ya kimataifa na kiuraia na naamini JF ni nyumba ya wabobezi wa mambo hayo na mengine, naomba kuwasilisha hoja na wito kwa waungwana kuziainisha faida na hasara za kuwa na uraia pacha hapa nchini kwetu Tanzania. Kujua faida na hasara kutachochea au kupooza wito wa wananchi wa kutaka uwepo wa uraia pacha kwa watanzania.
Karibuni waungwana wa JF...
Siyo kweli. Kila nchi inaporuhusu uraia pacha huweka sheria kulingana na maslahi yake. Kwa mfano Tanzania ikiruhusu uraia pacha inaweza kuweka sheria kuwa mtu ambaye siyo mzaliwa wa Tanzania na hata kama atapata uraia wa kuomba anaweza kufanya mambo A,B,C, na hawezi kufanya mambo C,D,E,. Hata USA wanaruhusu uraia pacha lakini kuna mambo mengine kama swewe siyo raia wa kuzaliwa wa USA huwezi kuyafanya. Ni kiasi cha kuweka mipaka tu.ukiruhusu uraia pacha wakenya watakuja kutuchukulia ardhi yetu yote, Watanzania Tutakuwa wapangaji.
Sababu yako ya ardhi haina mashiko kabisa. Naona kilichojificha nyuma ya sababu ni inda kama walivyo wapinga uraia pacha wengi. Uraia pacha unaweza kuja na sheria na kanuni zake ambazo zitaondoa hofu ya wageni kujilimbikizia ardhi. Pia tunaweza kusema uraia pacha ni kwa raia wazawa wa Tanzania tu au wageni wanaotaka uraia pacha wakapewa vigezo vikali vya kuwachuja. Hakuna kinachoshindikana.Kiukweli pro dual citizenship wa Tanzania hawana hoja za maana ndio maana hawaeleweki.
Na wengi wanaotoa hoja, wanagusia sana maslahi binafsi jambo ambalo ni gumu kushawishi watu wawaelewe. Ni sawa na mtu aende kutafuta kazi halafu sababu anasema anataka kusaidia familia yake.
Ifahamike nchi yetu bado changa na wabongo bado mbumbumbu na uwezo mdogo.
Silaha yetu kubwa kwasasa bado ni ARDHI kitu ambacho nchi nyingi zinazotuzunguka hazina.
Siku ukienda hapo Kenya ndio utajua thamani ya ardhi.
Tanzania ina takribani watu 60M hivi sasa na wanaongezeka kila siku. Unfortunately ardhi haiongezeki.
Na ukisema uruhusu uraia pacha with some limitations hasa kwenye ardhi au utawala hawa pro dual citizenship wanaweza wasikuelewe kwasababu wanachokitaka utakuwa umeziba.
Ni sawa na EAC kutaka eti mtu yeyote ndani ya jumuiya ya Africa Mashariki aruhusiwe kwenda kuishi popote ndani ya jumuiya. Wanaotunga sera hiyo wao ardhi hawana.
Muhimu ni kwanza sera zibadilike hasa za ardhi, either kila mtu apewe chake then ndio tuwe free kugawa uraia.
Au vile vile tunaweza pia kutoa Uraia pacha kwa watu wachache wenye uwezo wa kuwekeza kiwango fulani cha pesa kama $500,000+ na siyo kwa kila Tom and Jerry.
Toa hoja mkuu. Achana na sijui inda wala nini ?Sababu yako ya ardhi haina mashiko kabisa. Naona kilichojificha nyuma ya sababu ni inda kama walivyo wapinga uraia pacha wengi. Uraia pacha unaweza kuja na sheria na kanuni zake ambazo zitaondoa hofu ya wageni kujilimbikizia ardhi. Pia tunaweza kusema uraia pacha ni kwa raia wazawa wa Tanzania tu au wageni wanaotaka uraia pacha wakapewa vigezo vikali vya kuwachuja. Hakuna kinachoshindikana.
Hujasoma hoja niliyotoa? Haya nimeandika: Uraia pacha unaweza kuja na sheria na kanuni zake ambazo zitaondoa hofu ya wageni kujilimbikizia ardhi. Pia tunaweza kusema uraia pacha ni kwa raia wazawa wa Tanzania tu au wageni wanaotaka uraia pacha wakapewa vigezo vikali vya kuwachuja. Hakuna kinachoshindikana.Toa hoja mkuu. Achana na sijui inda wala nini ?
Kwanza maelezo yote ni dhahili kwamba bila ardhi suala la Dual Citizenship kwako halina maana !!???
Anyway, Muhimu ni Taifa kwanza.Hujasoma hoja niliyotoa? Haya nimeandika: Uraia pacha unaweza kuja na sheria na kanuni zake ambazo zitaondoa hofu ya wageni kujilimbikizia ardhi. Pia tunaweza kusema uraia pacha ni kwa raia wazawa wa Tanzania tu au wageni wanaotaka uraia pacha wakapewa vigezo vikali vya kuwachuja. Hakuna kinachoshindikana.
Ndo uache uvivu mpaka ukashindwa kufikiri, sasa raia wa kenya anainchi yake akija hawezi kuwa tena kuwa pacha maana anauraia wa nchi yake huko na huku ni mgeni.ukiruhusu uraia pacha wakenya watakuja kutuchukulia ardhi yetu yote, Watanzania Tutakuwa wapangaji.
Kama ameona ni sifa kuwa masikini bila kuchukua juhudi basi acha akae pembeni wanaohitaji kutoka katika umasikini wajitoe, kila mtu amehimizwa afanye kazi sasa Kama mtu anaona fahari kuwa masikini maana yake ni mvivu na huyo hafai kwa ugoigoi wake zaidi sana atafundisha wengine wawe goigoi Kama yeye.Tuanzie hapa,
Uraia pacha una faida gani kwa masikini wa hali ya chini (Kwa Tanzania Masikini Ni 95%)???
Ndiyo maana nikakuambia wewe unaongozwa na inda. Wewe bila shaka ni raia wa Tanzania. Taifa linafaidikaje na wewe? Taifa linafaidikaje na raia wengine wote wa Tanzania? Jinsi linavyofaidika na hao raia ndivyo hivyo hivyo litakavyofaidika na diaspora.Anyway, Muhimu ni Taifa kwanza.
Tatizo la pro dual citizenship hawasemi ni kwa namna gani taifa litafaidika na huo uraia pacha.
Hoja zao nyingi ni mambo yao binafsi.
Endelea kupambania kombe MkuuNdiyo maana nikakuambia wewe unaongozwa na inda. Wewe bila shaka ni raia wa Tanzania. Taifa linafaidikaje na wewe? Taifa linafaidikaje na raia wengine wote wa Tanzania? Jinsi linavyofaidika na hao raia ndivyo hivyo hivyo litakavyofaidika na diaspora.