Nilivyokuelewa, uraia wa nchi moja ni bora zaidi ya uraia pacha. Ni sawa?
Kwa nchi, kiuchumi, uraia pacha karibu mara zote ni mzuri zaidi ya uraia wa nchi moja tu.
Kwa mtu, inategemea na kipaumbele cha mtu.
Kwa mfano, Mtanzania mwenye uraia wa Marekani pia, ambaye ana malengo ya kuwekeza Tanzania, anaweza kuona uraia pacha ni kitu cha muhimu kwa sababu ya malengo yake ya uwekezaji.
Kiujumla, uraia pacha una faida nyingi kiuchumi kwa sababu utawapa Watanzania wenye uraia wa nchi nyingine nafasi kubwa ya kuwekeza nchini.
Hili jambo lilijadiliwa sana. Serikali ya Mkapa ikalikataa. Kwa sababu ambazo zilielezwa kuwa za usalama, lakini zilikuwa za kisiasa zaidi. Watu wenye uraia wa nchi nyingine walionekana kuwa na upeo mkubwa wa mambo kutokana na kuishi nje, wakaonekana tishio kwa utawala wa CCM.
Mkapa alisema ameridhia kuona Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine wanapewa "permanent residence" status Tanzania, waweze kuingia na kutoka bila visa, na wapewe upendeleo wa kuwekeza sawa na raia, lakini wadhibitiwe wasijiingize kwenye siasa.
Kuna Mzee mmoja niliongea naye akasema kuna Watanzania wengi wana hulka ya wivu tu, akasema hata enzi zao walivyokuwa wanafanya kazi Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuna Wakenya na Waganda wengi walikuwa wanatafutiana fursa za kwenda nje, lakini Watanzania walikuwa wanazibiana. Mtu akitaka kwenda nje kujiendeleza alikuwa anaonekana kama msaliti.
Ndiyo mpaka leo kuna huo ujinga, mtu akichukua uraia wa nchi nyingine, hata kwa kutafuta maisha tu, anaonekana si mzalendo, tishio, beberu na ujinga mwingine mwingi kama huo.
Wakati kiuhalisia mtu anayechukua uraia wa nchi nyingine ndiye anayeweza kuisaidia nchi zaidi.
Kuna wakati nilikuwa nafanya kazi Wall St. recruiters wakaiona resume (C.V) yangu, wakaipenda. Wakasema wana kazi Federal Reserve (Benki Kuu ya Marekani) wanataka kuniunganishia.
Nikawaambia sawa, lakini kwanza kabisa nikasema nataka kuwaambia kuwa mimi si raia wa Marekani (muda huo sijachukua uraia bado, nasubiria habari za uraia pacha Tanzania).
Recruiters wakaniambia, hilo si tatizo, tuachie sisi.
Nikawauliza, kweli? Mbona mimi ninavyojua position nyeti kama hii Benki Kuu ya Marekani itataka mtu aliye raia tu?
Wakasema tuachie sisi.
Nikasema sawa.
Wakaenda kuulizia vizuri zaidi, wakarudi.
Wakasema, ulivyosema ni kweli.
Ile kazi una kila sifa, ungefaa sana. Tatizo wanataka raia wa Marekani.
Nikasema mimi nilijua hilo. Nikawashukuru.
Nikaona kusubiri uraia pacha ni ujinga, after all, mimi niliamua kuhama kimoja kuja Marekani. Sijaja Marekani kwa lengo la kuishi na kurudi Tanzania.
Baada ya kusubiri uraia pacha kwa miaka 15, nikaamua kuchukua uraia wa Marekani.
Ukiangalia hapo, utaona kwamba, Tanzania imejinyima nafasi ya kuwa na raia wake anayefanya kazi Benki Kuu ya Marekani, anayeweza kuona mambo yanavyoenda huko Benki Kuu ya Marekani na kuisaidia Tanzania kwa ujuzi wake anaoupata huko.