Mjadala wa kitaifa: Tuziainishe faida na hasara za uraia-pacha (dual citizenship) kwa Tanzania yetu

Mjadala wa kitaifa: Tuziainishe faida na hasara za uraia-pacha (dual citizenship) kwa Tanzania yetu

A matter of international law.

Mimi kama raia wa Marekani, nikiwa Tanzania kama raia wa Marekani tu bila uraia pacha, serikali ya Marekani ina uwezo mkubwa sana wa kunitetea kama raia wake ambaye nina uraia wa Marekani tu.

Nikiwa na uraia pacha, wa Tanzania na Marekani, serikali yangu ya Marekani inapata vizingiti fulani vya kisheria kunitetea nikipata matatizo Tanzania.Kwa sababu ya uraia wangu pacha wa Tanzania na Marekani.
Nilivyokuelewa, uraia wa nchi moja ni bora zaidi ya uraia pacha. Ni sawa?
 
Tatizo la hii nchi ni ushamba na kutojiamini. Wengi wanaamini mtu akiwa na uraia pacha basi ataihujumu TZ na kuipa faida nchi nyingine, tunaacha kujiuliza kwanini mtu huyo huyo asihujumu nchi nyingine na kuleta maendelea bongo. Hatuamini uwezo wa watu wetu kushindana kwenye soko la kimataifa? Kama hatuwaamini ina maana tunatengeneza watu incompetent huku tukijua fika ni incompetent.

Tukienda ki-namba, mchango wa diaspora kwenye pato la taifa yani remittances za nchi kama Kenya na nchi zingine limeongezeka maradufu baada ya kuruhusu uraia pacha. Katika hizo nchi remittances zinachangia a substantial amount kwenye pato la taifa sababu watu wanawekeza heavily kwao huku wakiwa na imani na mali zao kwamba hawatazipoteza kwa sababu ya kigezo cha uraia.

Ukija bongo mtu unawaza kuwekeza nyumbani mara tu ukichukua uraia wa nchi nyingine. Aidha uanze kuandika majina ya ndugu kwenye mali zako au usitishe kabisa kuwekeza nyumbani kitu ambacho hakisaidii nchi kwa ujumla.

Kingine ni kasumba ambayo wabongo wamemezeshwa miaka nenda rudi kwamba nchi yao tu ndo ina mali na wengine wote wanawaonea wivu. Wanaamini wakiruhusu uraia pacha wageni watakuja kutumia mali asili zao kwa faida yao. Mali asili zipo kwa faida ya wote duniani so long as sheria na taratibu zinafuatwa. Leo hii nchi zenye less natural resources na dual citizenship zinaingiza pesa nyingi na zipo mbali kuliko sisi tunaozikumbatia maliasili kama viazi.

Nchi isiyo ruhusu uraia pacha, isiyo na viwanda vyenye kuzalisha ajira za kutosha, yenye mifumo kandamizi yakufanya malipo online is doomed to fail katika ulimwengu wa leo.
 
Nilivyokuelewa, uraia wa nchi moja ni bora zaidi ya uraia pacha. Ni sawa?
Kwa nchi, kiuchumi, uraia pacha karibu mara zote ni mzuri zaidi ya uraia wa nchi moja tu.

Kwa mtu, inategemea na kipaumbele cha mtu.

Kwa mfano, Mtanzania mwenye uraia wa Marekani pia, ambaye ana malengo ya kuwekeza Tanzania, anaweza kuona uraia pacha ni kitu cha muhimu kwa sababu ya malengo yake ya uwekezaji.

Kiujumla, uraia pacha una faida nyingi kiuchumi kwa sababu utawapa Watanzania wenye uraia wa nchi nyingine nafasi kubwa ya kuwekeza nchini.

Hili jambo lilijadiliwa sana. Serikali ya Mkapa ikalikataa. Kwa sababu ambazo zilielezwa kuwa za usalama, lakini zilikuwa za kisiasa zaidi. Watu wenye uraia wa nchi nyingine walionekana kuwa na upeo mkubwa wa mambo kutokana na kuishi nje, wakaonekana tishio kwa utawala wa CCM.

Mkapa alisema ameridhia kuona Watanzania waliochukua uraia wa nchi nyingine wanapewa "permanent residence" status Tanzania, waweze kuingia na kutoka bila visa, na wapewe upendeleo wa kuwekeza sawa na raia, lakini wadhibitiwe wasijiingize kwenye siasa.

Kuna Mzee mmoja niliongea naye akasema kuna Watanzania wengi wana hulka ya wivu tu, akasema hata enzi zao walivyokuwa wanafanya kazi Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, kuna Wakenya na Waganda wengi walikuwa wanatafutiana fursa za kwenda nje, lakini Watanzania walikuwa wanazibiana. Mtu akitaka kwenda nje kujiendeleza alikuwa anaonekana kama msaliti.

Ndiyo mpaka leo kuna huo ujinga, mtu akichukua uraia wa nchi nyingine, hata kwa kutafuta maisha tu, anaonekana si mzalendo, tishio, beberu na ujinga mwingine mwingi kama huo.

Wakati kiuhalisia mtu anayechukua uraia wa nchi nyingine ndiye anayeweza kuisaidia nchi zaidi.

Kuna wakati nilikuwa nafanya kazi Wall St. recruiters wakaiona resume (C.V) yangu, wakaipenda. Wakasema wana kazi Federal Reserve (Benki Kuu ya Marekani) wanataka kuniunganishia.

Nikawaambia sawa, lakini kwanza kabisa nikasema nataka kuwaambia kuwa mimi si raia wa Marekani (muda huo sijachukua uraia bado, nasubiria habari za uraia pacha Tanzania).

Recruiters wakaniambia, hilo si tatizo, tuachie sisi.

Nikawauliza, kweli? Mbona mimi ninavyojua position nyeti kama hii Benki Kuu ya Marekani itataka mtu aliye raia tu?

Wakasema tuachie sisi.

Nikasema sawa.

Wakaenda kuulizia vizuri zaidi, wakarudi.

Wakasema, ulivyosema ni kweli.

Ile kazi una kila sifa, ungefaa sana. Tatizo wanataka raia wa Marekani.

Nikasema mimi nilijua hilo. Nikawashukuru.

Nikaona kusubiri uraia pacha ni ujinga, after all, mimi niliamua kuhama kimoja kuja Marekani. Sijaja Marekani kwa lengo la kuishi na kurudi Tanzania.

Baada ya kusubiri uraia pacha kwa miaka 15, nikaamua kuchukua uraia wa Marekani.

Ukiangalia hapo, utaona kwamba, Tanzania imejinyima nafasi ya kuwa na raia wake anayefanya kazi Benki Kuu ya Marekani, anayeweza kuona mambo yanavyoenda huko Benki Kuu ya Marekani na kuisaidia Tanzania kwa ujuzi wake anaoupata huko.
 
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mijadala kuhusu Tanzania kuruhusu uraia pacha. Wapo wanaopendekeza Tanzania kama nchi ikubali uwepo wa uraia pacha ili kuzipata faida zitokanazo na uraia wa aina hiyo. Wapo wenye mtazamo kuwa muda wa Tanzania kuwa na uraia pacha bado haujafika. Hivyo basi, wanauunga mkono msimamo wa Serikali wa kutokubali na kuanzisha uraia pacha hapa nchini.

Uraia ni jambo la kisheria. Endapo Serikali itaridhia kuanzishwa kwa uraia pacha, lazima sheria inayosimamia masuala ya uraia ifanyiwe marekebisho kukidhi matakwa ya mabadiliko hayo. Ilivyo sasa, uraia unaokubalika hapa nchini ni uraia wa nchi moja: kama ni raia wa Tanzania au la. Raia wa Tanzania, ilivyo sasa, haruhusiwi kuwa raia wa nchi nyingine yeyote duniani. Ikitokea hivyo, raia husika itampasa kupoteza uraia mmojawapo: ima wa Tanzania au wa hiyo nchi nyingine.

Kwa kuwa mimi si mbobezi wa masuala ya kimataifa na kiuraia na naamini JF ni nyumba ya wabobezi wa mambo hayo na mengine, naomba kuwasilisha hoja na wito kwa waungwana kuziainisha faida na hasara za kuwa na uraia pacha hapa nchini kwetu Tanzania. Kujua faida na hasara kutachochea au kupooza wito wa wananchi wa kutaka uwepo wa uraia pacha kwa watanzania.

Karibuni waungwana wa JF...
Kijana wangu nashukuru kwa kuleta mada hii namimi napenda kuchangia ili kutoa elimu;

Faida za uraia Pacha; humuwezesha mtu kupata huduma za kijamii nchi yoyote ambayo ana uraia.Kama uraia wa Tanzania na Marekani,utanufaika na kupata elimu,huduma za afya bila kubaguliwa. Kwa Mtanzania mwenye uraia pacha hapa hunufaika na huduma bora toka nchi zilizoendelea na kuna fursa ya nchi kama Tanzania kunufaika na utaalamu na ujuzi wa raia hawa waliopata ujuzi nje ya nchi na pia kwa upande wa gharama za matibabu hili litaweza kupunguza gharama kwa Tanzania.

Pili,mtu mwenye uraia pacha anaweza kupiga kura au kuligiwa kura kupata uongozi nchi yoyote. Hapa kuna fursa kwa nchi kwamba kama mtu huyu ana utaalam na hana nia mbaya atakuwa msaada lakini kama mtu huyu atakuwa na nia mbaya au ni pandikizi kuna hatari kubwa ya sana kiusalama.Ni ngumu kutambua je huyu mtu ni mtiifu kwa taifa gani?

Tatu,mtu mwenye uraia pacha huweza kumiliki mali katika nchi yoyote atakayo.Ni fursa kwamba mali hususani nyumba kupata soko la uhakika ila kuna hatari ya kwamba watu hususani pale anapokuwa na maslahi ya kihasusi kununua mali na kisha kutozitumia,hii huathiri uchumi au kuitumia kwa maslahi ya ujasusi ya nchi nyingine.

Nne, mtu mwenye uraia pacha analipa kodi kwa zote ambazo ana uraia.Kwa nchi kama Tanzania hii ni fursa ya kukusanya kodi kutoka kwa madiaspora wote waliopo ulimwenguni.
 
Imethibika time and again katika nchi tofauti faida zina outweigh hasara na hayo mashaka ya mambo ya usalama na ujasusi.
 
Security reasons sio poa..Kama Nyarandu Ana green card TU wakati wa uchaguzi wa 2015 alijinadi Wamarekani wanataka awe raisi..nyie fanyeni kazi huko FBI etc huku mje kutembea tu ..Labda wanamichezo POA...
 
Wengine kwa sasa hata kutembea tunaishia JF.

Tutakuja harusi na misiba tu, tena ya watu wa karibu.

Isiwe tabu.
 
Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na mijadala kuhusu Tanzania kuruhusu uraia pacha. Wapo wanaopendekeza Tanzania kama nchi ikubali uwepo wa uraia pacha ili kuzipata faida zitokanazo na uraia wa aina hiyo. Wapo wenye mtazamo kuwa muda wa Tanzania kuwa na uraia pacha bado haujafika. Hivyo basi, wanauunga mkono msimamo wa Serikali wa kutokubali na kuanzisha uraia pacha hapa nchini.

Uraia ni jambo la kisheria. Endapo Serikali itaridhia kuanzishwa kwa uraia pacha, lazima sheria inayosimamia masuala ya uraia ifanyiwe marekebisho kukidhi matakwa ya mabadiliko hayo. Ilivyo sasa, uraia unaokubalika hapa nchini ni uraia wa nchi moja: kama ni raia wa Tanzania au la. Raia wa Tanzania, ilivyo sasa, haruhusiwi kuwa raia wa nchi nyingine yeyote duniani. Ikitokea hivyo, raia husika itampasa kupoteza uraia mmojawapo: ima wa Tanzania au wa hiyo nchi nyingine.

Kwa kuwa mimi si mbobezi wa masuala ya kimataifa na kiuraia na naamini JF ni nyumba ya wabobezi wa mambo hayo na mengine, naomba kuwasilisha hoja na wito kwa waungwana kuziainisha faida na hasara za kuwa na uraia pacha hapa nchini kwetu Tanzania. Kujua faida na hasara kutachochea au kupooza wito wa wananchi wa kutaka uwepo wa uraia pacha kwa watanzania.

Karibuni waungwana wa JF...
§337.1 Oath of allegiance.

Except as otherwise provided in the Act and after receiving notice from the district director that such applicant is eligible for naturalization pursuant to §335.3 of this chapter, an applicant for naturalization shall, before being admitted to citizenship, take in a public ceremony held within the United States the following oath of allegiance, to a copy of which the applicant shall affix his or her signature:

I hereby declare, on oath, that I absolutely and entirely renounce and abjure all allegiance and fidelity to any foreign prince, potentate, state, or sovereignty, of whom or which I have heretofore been a subject or citizen; that I will support and defend the Constitution and laws of the United States of America against all enemies, foreign and domestic; that I will bear true faith and allegiance to the same; that I will bear arms on behalf of the United States when required by the law; that I will perform noncombatant service in the Armed Forces of the United States when required by the law; that I will perform work of national importance under civilian direction when required by the law; and that I take this obligation freely, without any mental reservation or purpose of evasion; so help me God.

WEWE NDIWE PETRO, NA JUU YA MWAMBA HUU NITALIJENGA KANISA LANGU
 
ukiruhusu uraia pacha wakenya watakuja kutuchukulia ardhi yetu yote, Watanzania Tutakuwa wapangaji.
Siyo kweli. Kila nchi inaporuhusu uraia pacha huweka sheria kulingana na maslahi yake. Kwa mfano Tanzania ikiruhusu uraia pacha inaweza kuweka sheria kuwa mtu ambaye siyo mzaliwa wa Tanzania na hata kama atapata uraia wa kuomba anaweza kufanya mambo A,B,C, na hawezi kufanya mambo C,D,E,. Hata USA wanaruhusu uraia pacha lakini kuna mambo mengine kama swewe siyo raia wa kuzaliwa wa USA huwezi kuyafanya. Ni kiasi cha kuweka mipaka tu.
 
Kiukweli pro dual citizenship wa Tanzania hawana hoja za maana ndio maana hawaeleweki.

Na wengi wanaotoa hoja, wanagusia sana maslahi binafsi jambo ambalo ni gumu kushawishi watu wawaelewe. Ni sawa na mtu aende kutafuta kazi halafu sababu anasema anataka kusaidia familia yake.

Ifahamike nchi yetu bado changa na wabongo bado mbumbumbu na uwezo mdogo.

Silaha yetu kubwa kwasasa bado ni ARDHI kitu ambacho nchi nyingi zinazotuzunguka hazina.

Siku ukienda hapo Kenya ndio utajua thamani ya ardhi.

Tanzania ina takribani watu 60M hivi sasa na wanaongezeka kila siku. Unfortunately ardhi haiongezeki.

Na ukisema uruhusu uraia pacha with some limitations hasa kwenye ardhi au utawala hawa pro dual citizenship wanaweza wasikuelewe kwasababu wanachokitaka utakuwa umeziba.

Ni sawa na EAC kutaka eti mtu yeyote ndani ya jumuiya ya Africa Mashariki aruhusiwe kwenda kuishi popote ndani ya jumuiya. Wanaotunga sera hiyo wao ardhi hawana.

Muhimu ni kwanza sera zibadilike hasa za ardhi, either kila mtu apewe chake then ndio tuwe free kugawa uraia.

Au vile vile tunaweza pia kutoa Uraia pacha kwa watu wachache wenye uwezo wa kuwekeza kiwango fulani cha pesa kama $500,000+ na siyo kwa kila Tom and Jerry.
 
Sababu yako ya ardhi haina mashiko kabisa. Naona kilichojificha nyuma ya sababu ni inda kama walivyo wapinga uraia pacha wengi. Uraia pacha unaweza kuja na sheria na kanuni zake ambazo zitaondoa hofu ya wageni kujilimbikizia ardhi. Pia tunaweza kusema uraia pacha ni kwa raia wazawa wa Tanzania tu au wageni wanaotaka uraia pacha wakapewa vigezo vikali vya kuwachuja. Hakuna kinachoshindikana.
 
Toa hoja mkuu. Achana na sijui inda wala nini ?

Kwanza maelezo yote ni dhahili kwamba bila ardhi suala la Dual Citizenship kwako halina maana !!???
 
Toa hoja mkuu. Achana na sijui inda wala nini ?

Kwanza maelezo yote ni dhahili kwamba bila ardhi suala la Dual Citizenship kwako halina maana !!???
Hujasoma hoja niliyotoa? Haya nimeandika: Uraia pacha unaweza kuja na sheria na kanuni zake ambazo zitaondoa hofu ya wageni kujilimbikizia ardhi. Pia tunaweza kusema uraia pacha ni kwa raia wazawa wa Tanzania tu au wageni wanaotaka uraia pacha wakapewa vigezo vikali vya kuwachuja. Hakuna kinachoshindikana.
 
Anyway, Muhimu ni Taifa kwanza.

Tatizo la pro dual citizenship hawasemi ni kwa namna gani taifa litafaidika na huo uraia pacha.

Hoja zao nyingi ni mambo yao binafsi.
 
ukiruhusu uraia pacha wakenya watakuja kutuchukulia ardhi yetu yote, Watanzania Tutakuwa wapangaji.
Ndo uache uvivu mpaka ukashindwa kufikiri, sasa raia wa kenya anainchi yake akija hawezi kuwa tena kuwa pacha maana anauraia wa nchi yake huko na huku ni mgeni.
 
Tuanzie hapa,

Uraia pacha una faida gani kwa masikini wa hali ya chini (Kwa Tanzania Masikini Ni 95%)???
Kama ameona ni sifa kuwa masikini bila kuchukua juhudi basi acha akae pembeni wanaohitaji kutoka katika umasikini wajitoe, kila mtu amehimizwa afanye kazi sasa Kama mtu anaona fahari kuwa masikini maana yake ni mvivu na huyo hafai kwa ugoigoi wake zaidi sana atafundisha wengine wawe goigoi Kama yeye.
 
Anyway, Muhimu ni Taifa kwanza.

Tatizo la pro dual citizenship hawasemi ni kwa namna gani taifa litafaidika na huo uraia pacha.

Hoja zao nyingi ni mambo yao binafsi.
Ndiyo maana nikakuambia wewe unaongozwa na inda. Wewe bila shaka ni raia wa Tanzania. Taifa linafaidikaje na wewe? Taifa linafaidikaje na raia wengine wote wa Tanzania? Jinsi linavyofaidika na hao raia ndivyo hivyo hivyo litakavyofaidika na diaspora.
 
Endelea kupambania kombe Mkuu
 
Back
Top Bottom