Mjadala wa kitaifa: Tuziainishe faida na hasara za uraia-pacha (dual citizenship) kwa Tanzania yetu

Mnadiss ujamaa as if ni mfumo mbovu kwa 100%.

Mna akili za kipumbavu sana. Na hii ni kwasababu hamjawahi kuuishi ubepari 100%.

Msichokijua hata huko kwa mabepari bado kuna practice kadhaa za kijamaa.
Mkuu, filosofia ya ujamaa ni filosofia nzuri sana ila isiyo na uhalisia katika dunia hii. China (ya Mao) iliyokuwa kinara wa ujamaa waliona kabisa kuwa haitekelezeki. Alichokifanya ni kuufanyia mageuzi ubepari, na sasa mwanafunzi kawa mwalimu mkuu. Kwa bahati mbaya sana, Ujamaa wa enzi Mwalimu ni "Utopian"..hauwezi kutekelezeka kwa dunia ya hii, hasa kiuchumi na kisiasa.
 
Mzee imeandikwa kifasihi...nimekupata sana...hongera
 
Nyerere alikimbilia sera za kijamaa kama njia ya kupata pesa za kuendeshea nchi baadae akagundua kuwa hao wajamaa wenyewe ni choka mbaya.

Wakati anaondoka 1985 aligundua tayari kuwa ujamaa ni mgumu na Mwinyi akawa hana ujanja zaidi ya kuingia mzima mzima kwenye utekelezaji wa matakwa ya kina world bank na IMF.
 
Na as long as kwa jinsi Tz wanavyoendelea bado kuwa na fikra hizo na 'Hang'over' za Ujamaa,mie naona itachukua muda na kazi kubwa kuja kutoboa na kupata maendeleo ya uhakika na yenye tija......
 
..ukichukua uraia pacha maana yake unajisalimisha na kujikabidhi kuwa chini ya mamlaka na dhuluma za watawala wa Tz.

..ni afadhali kuwa raia wa nchi nyingine, haswa nchi za magharibi, kwani nchi hizo zinajali raia wake na kuwatetea wanapopata matatizo ktk nchi nyingine.

..fikiria tukio la Aquilina kupigwa risasi halafu hakuna yeyote aliyewajibika. Binti yule angekuwa ni raia wa kigeni nchi yake ingelazimisha waliomuua wachukuliwe hatua, na huenda familia yake ingeshitaki na kulipwa fidia.

..sisemi kwamba ktk mataifa mengine hakuna uonevu au vyombo vya dola haviui raia wa nchi hizo. kilichowatofautisha wao na sisi ni kwamba vyombo vya dola na watawala ktk nchi za magharibi huwajibishwa pale wanapoumiza raia kwa makosa au kukusudia.

..binafsi ningeunyaka uraia wa nchi za magharibi msingenisikia nahangaika kutafuta uraia wa Tz.
 
Mkuu, vifungu vyote ulivyoviweka vinahusu kusita kwa uraia wa mtanzania pale ambapo amepata uraia wa nchi nyingine au ameondolewa uraia huo na Waziri wa Mambo ya Ndani
 

Binafsi sijaona emperical evidence kuonesha ni diaspora wangapi ambao walikwama ama hawakufika mbali kama unavyosema kwa sababu tu hakuna uraia pacha. Mengine mengi mnayoongea yanazunguka kwenye hisia za woga.

Kuhusu kulinganisha na kenya, wenyewe wana culture tofauti na ya Tanzania, nchini mwao hawaaminiani. wanapigana vita. wana mitazamo ya kikabila zaidi. wanaishi kwenye cast. wana class struggle. ndiyo maana ikitokea uchaguzi lazima waaze kudhuriana. hata sasa kuna wanasiasa wanaunda makundi ya kuzusha ghasia kipindi cha uchaguzi. Huwezi linganisha na nchi ambayo ukiwekeza kwa kufuata sheria hakuna mtu wa kuja kukubugudhi.
 
Mkuu hoja yako haijasimama wima, kwani raia na hata kiongozi au viongozi wa nchi hufanya huo usaliti. Huko ni kuvunja sheria, kinachotakiwa ni sheria zifanye kazi.
 
Kwanza tujipe utafiti kidogo!

1. Je, ni nchi zipi hapa Duniani zinaruhusu uraia pacha?

2. Je, hizo nchi zilizoruhusu uraia pacha zimepata hasara gani?

3. Kama nchi zipo zilizopata hasara, je, zilisimamisha uraia pacha au ziliendelea kuruhusu?
 

Sawa mkuu.
 
Kuna ukweli mkubwa katika hili.
Na baadhi ya nchi zinaamini kwamba ukiwa raia, unaweza hitajika muda wowote jeshini kuitetea nchi
.
Imagine ni dual citizen wa Russia na Ukraine. Mzawa wa Russia uliyekulia na kusomea huko na pengine ulipata kufanya kazi wizara ya ulinzi huko Russia.
.
Sasa umechukua uraia wa/ na unaishi Ukraine. Unadhani nani atakuwa na wasiwasi zaidi na uwepo wako nchi ya pili?
 
Uraia pacha usichanganywe na Uraisi pacha hauna tatizo lolote...Mulamula.
 
Kama kutakuwa na uraia pacha basi uwe ni kwa watanzania tu walio na uraia kwenye nchi nyingne ila kiasili ni watanzania (blood) hawa tu ndo wapewe dual citizenship hizo habari za wakenya, sijui warundi, wanyarwanda wahindi na wengineo kutoka makwao kuja kuomba dual citizenship ya Tanzania hiyo hapana kabisa ni very soon nchi itajaa raia wahamiaji na kutusababishia mambo ya ajabu yasiyo eleweka kwenye taifa letu.
Nchi zilizotuzunguka zina changamoto kubwa ya ardhi wote kitakacho waleta huku ni ardhi tu hakuna lolote lile la ziada au zaid ya hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…