Mie nafikiri wasomi wetu wanasheria ndo wanatuangusha kusema uraia pacha hauruhusiwi Tanzania, kitu kinachopelekea hata police wetu kuanza kuandama watu ndivyo sivyo.
Uraia pacha Tanzania naamini unaruhusiwa ktk katiba hii hii ila tu haijapata mtu wakuitaka mahakama ielezee kwa undani zaidi. Nitachukua snap chache hapa kuonesha hilo.
Kinachotakiwa ni watanzania kurudishiwa haki yao, ambayo imebainishwa ktk katiba, ila watu ama ni ignorant ama kwasababu zao wanakomalia katiba hairuhusu. Wasomi wa sheria naomba mnitafsrie vifungu vya katiba hivi hasa ninapotilia mkazo.
Hii ya kwanza naelewa mimi kama mleyi kwamba mtu aliyeoa na akapata uraia wa huko anaruhusiwa kuendelea na uraia wa Tanzania-dual.
View attachment 1812824
Na hapa chini pia
View attachment 1812827