Mjadala wa kitaifa: Tuziainishe faida na hasara za uraia-pacha (dual citizenship) kwa Tanzania yetu

Mjadala wa kitaifa: Tuziainishe faida na hasara za uraia-pacha (dual citizenship) kwa Tanzania yetu

Mnadiss ujamaa as if ni mfumo mbovu kwa 100%.

Mna akili za kipumbavu sana. Na hii ni kwasababu hamjawahi kuuishi ubepari 100%.

Msichokijua hata huko kwa mabepari bado kuna practice kadhaa za kijamaa.
Mkuu, filosofia ya ujamaa ni filosofia nzuri sana ila isiyo na uhalisia katika dunia hii. China (ya Mao) iliyokuwa kinara wa ujamaa waliona kabisa kuwa haitekelezeki. Alichokifanya ni kuufanyia mageuzi ubepari, na sasa mwanafunzi kawa mwalimu mkuu. Kwa bahati mbaya sana, Ujamaa wa enzi Mwalimu ni "Utopian"..hauwezi kutekelezeka kwa dunia ya hii, hasa kiuchumi na kisiasa.
 
Ipo imani kwamba ni rahisi kwa mtu mwenye uraia wa nchi mbili kuweza kuifanyia hujuma Tanzania. Cha ajabu ni kwamba wenye kuifanyia mambo ya ajabu wengi ni wale wenye kuvaa koti la uzalendo.

Mtu anatembea na tai yenye rangi za bendera ya taifa kumbe akiwa mbali na kamera ni mpigaji mkubwa. Waliokuwa wanakausha maji kule kwenye bwawa la mtera ili majenereta yauzwe Kariakoo na mjini katikati ni wazalendo wanaoweka mikono juu ya kifua wakati wimbo wa taifa unapoimbwa.

Uraia pacha utaisaidia zaidi Tanzania kuliko hizi dhana potofu zilizopo. Upeo wa mtu aliyezaliwa Denmark ambaye mama yake ni mwenyeji wa kule na baba mtanzania ni tofauti na yule aliyezaliwa Nzega na kukulia Mwanza mjini.

Utangamano wa Afrika ya Kusini ndio chanzo cha uchumi kuwa mkubwa na wenye kuheshimika, wasingekuwepo wazungu na wahindi kule nina uhakika wale weusi wangekuwa wachovu tu kama mataifa yanayoizunguka nchi ile.
Mzee imeandikwa kifasihi...nimekupata sana...hongera
 
Mkuu, filosofia ya ujamaa ni filosofia nzuri sana ila isiyo na uhalisia katika dunia hii. China (ya Mao) iliyokuwa kinara wa ujamaa waliona kabisa kuwa haitekelezeki. Alichokifanya ni kuufanyia mageuzi ubepari, na sasa mwanafunzi kawa mwalimu mkuu. Kwa bahati mbaya sana, Ujamaa wa enzi Mwalimu ni "Utopian"..hauwezi kutekelezeka kwa dunia ya hii, hasa kiuchumi na kisiasa.
Nyerere alikimbilia sera za kijamaa kama njia ya kupata pesa za kuendeshea nchi baadae akagundua kuwa hao wajamaa wenyewe ni choka mbaya.

Wakati anaondoka 1985 aligundua tayari kuwa ujamaa ni mgumu na Mwinyi akawa hana ujanja zaidi ya kuingia mzima mzima kwenye utekelezaji wa matakwa ya kina world bank na IMF.
 
Na as long as kwa jinsi Tz wanavyoendelea bado kuwa na fikra hizo na 'Hang'over' za Ujamaa,mie naona itachukua muda na kazi kubwa kuja kutoboa na kupata maendeleo ya uhakika na yenye tija......
Mkuu, filosofia ya ujamaa ni filosofia nzuri sana ila isiyo na uhalisia katika dunia hii. China (ya Mao) iliyokuwa kinara wa ujamaa waliona kabisa kuwa haitekelezeki. Alichokifanya ni kuufanyia mageuzi ubepari, na sasa mwanafunzi kawa mwalimu mkuu. Kwa bahati mbaya sana, Ujamaa wa enzi Mwalimu ni "Utopian"..hauwezi kutekelezeka kwa dunia ya hii, hasa kiuchumi na kisiasa.
 
..ukichukua uraia pacha maana yake unajisalimisha na kujikabidhi kuwa chini ya mamlaka na dhuluma za watawala wa Tz.

..ni afadhali kuwa raia wa nchi nyingine, haswa nchi za magharibi, kwani nchi hizo zinajali raia wake na kuwatetea wanapopata matatizo ktk nchi nyingine.

..fikiria tukio la Aquilina kupigwa risasi halafu hakuna yeyote aliyewajibika. Binti yule angekuwa ni raia wa kigeni nchi yake ingelazimisha waliomuua wachukuliwe hatua, na huenda familia yake ingeshitaki na kulipwa fidia.

..sisemi kwamba ktk mataifa mengine hakuna uonevu au vyombo vya dola haviui raia wa nchi hizo. kilichowatofautisha wao na sisi ni kwamba vyombo vya dola na watawala ktk nchi za magharibi huwajibishwa pale wanapoumiza raia kwa makosa au kukusudia.

..binafsi ningeunyaka uraia wa nchi za magharibi msingenisikia nahangaika kutafuta uraia wa Tz.
 
Mie nafikiri wasomi wetu wanasheria ndo wanatuangusha kusema uraia pacha hauruhusiwi Tanzania, kitu kinachopelekea hata police wetu kuanza kuandama watu ndivyo sivyo.

Uraia pacha Tanzania naamini unaruhusiwa ktk katiba hii hii ila tu haijapata mtu wakuitaka mahakama ielezee kwa undani zaidi. Nitachukua snap chache hapa kuonesha hilo.
Kinachotakiwa ni watanzania kurudishiwa haki yao, ambayo imebainishwa ktk katiba, ila watu ama ni ignorant ama kwasababu zao wanakomalia katiba hairuhusu. Wasomi wa sheria naomba mnitafsrie vifungu vya katiba hivi hasa ninapotilia mkazo.

Hii ya kwanza naelewa mimi kama mleyi kwamba mtu aliyeoa na akapata uraia wa huko anaruhusiwa kuendelea na uraia wa Tanzania-dual.
View attachment 1812824

Na hapa chini pia
View attachment 1812827
Mkuu, vifungu vyote ulivyoviweka vinahusu kusita kwa uraia wa mtanzania pale ambapo amepata uraia wa nchi nyingine au ameondolewa uraia huo na Waziri wa Mambo ya Ndani
 
Kumbe Unaongelea hisani na mazoea.

Mtu anayetaka kuwekeza kiasi cha kutosha hawezi kurisk kufanya biashara kwa kutegemea kudra na uzembe wa wabongo. Moreover, unajiumiza zaidi wewe mwenyewe kwa kufanya mambo kinyemela. Huwezi kufika mbali.

Fuatilia michango ya diaspora Kenya kabla na baada ya kuruhusu uraia pacha uone exponential increase of remittances. Leo hii banks za Kenya zinazunguka dunia nzima kuwaomba diaspora wawekeze KE na wao wanafanya hivyo sababu hakuna tena vikwazo.

Binafsi sijaona emperical evidence kuonesha ni diaspora wangapi ambao walikwama ama hawakufika mbali kama unavyosema kwa sababu tu hakuna uraia pacha. Mengine mengi mnayoongea yanazunguka kwenye hisia za woga.

Kuhusu kulinganisha na kenya, wenyewe wana culture tofauti na ya Tanzania, nchini mwao hawaaminiani. wanapigana vita. wana mitazamo ya kikabila zaidi. wanaishi kwenye cast. wana class struggle. ndiyo maana ikitokea uchaguzi lazima waaze kudhuriana. hata sasa kuna wanasiasa wanaunda makundi ya kuzusha ghasia kipindi cha uchaguzi. Huwezi linganisha na nchi ambayo ukiwekeza kwa kufuata sheria hakuna mtu wa kuja kukubugudhi.
 
Hatutaki uraia chotara. Kama ilivyo kwa mtu chotara anajipendekeza kwa mbari nyeupe na kujiweka mbali na watu weusi. Tabia yao wengine ni wabaguzi kuliko mtu mzungu au mwarabu. Vivyo hivyo uchotara wa uraia mtu utamkuta kujifanya mzalendo uzunguni au uarabuni. Wanaweza kutumia haki za uraia afrika kwa faida ya huo uraia wake wa kizungu au asia kwa kuzifaidisha nchi zingine na kuwafukarisha wenyeji wa nchi yake asili.
Mkuu hoja yako haijasimama wima, kwani raia na hata kiongozi au viongozi wa nchi hufanya huo usaliti. Huko ni kuvunja sheria, kinachotakiwa ni sheria zifanye kazi.
 
Kwanza tujipe utafiti kidogo!

1. Je, ni nchi zipi hapa Duniani zinaruhusu uraia pacha?

2. Je, hizo nchi zilizoruhusu uraia pacha zimepata hasara gani?

3. Kama nchi zipo zilizopata hasara, je, zilisimamisha uraia pacha au ziliendelea kuruhusu?
 
Binafsi sijaona emperical evidence kuonesha ni diaspora wangapi ambao walikwama ama hawakufika mbali kama unavyosema kwa sababu tu hakuna uraia pacha. Mengine mengi mnayoongea yanazunguka kwenye hisia za woga.

Kuhusu kulinganisha na kenya, wenyewe wana culture tofauti na ya Tanzania, nchini mwao hawaaminiani. wanapigana vita. wana mitazamo ya kikabila zaidi. wanaishi kwenye cast. wana class struggle. ndiyo maana ikitokea uchaguzi lazima waaze kudhuriana. hata sasa kuna wanasiasa wanaunda makundi ya kuzusha ghasia kipindi cha uchaguzi. Huwezi linganisha na nchi ambayo ukiwekeza kwa kufuata sheria hakuna mtu wa kuja kukubugudhi.

Sawa mkuu.
 
A matter of international law.

Mimi kama raia wa Marekani, nikiwa Tanzania kama raia wa Marekani tu bila uraia pacha, serikali ya Marekani ina uwezo mkubwa sana wa kunitetea kama raia wake ambaye nina uraia wa Marekani tu.

Nikiwa na uraia pacha, wa Tanzania na Marekani, serikali yangu ya Marekani inapata vizingiti fulani vya kisheria kunitetea nikipata matatizo Tanzania.Kwa sababu ya uraia wangu pacha wa Tanzania na Marekani.
Kuna ukweli mkubwa katika hili.
Na baadhi ya nchi zinaamini kwamba ukiwa raia, unaweza hitajika muda wowote jeshini kuitetea nchi
.
Imagine ni dual citizen wa Russia na Ukraine. Mzawa wa Russia uliyekulia na kusomea huko na pengine ulipata kufanya kazi wizara ya ulinzi huko Russia.
.
Sasa umechukua uraia wa/ na unaishi Ukraine. Unadhani nani atakuwa na wasiwasi zaidi na uwepo wako nchi ya pili?
 
Uraia pacha usichanganywe na Uraisi pacha hauna tatizo lolote...Mulamula.
 
Kama kutakuwa na uraia pacha basi uwe ni kwa watanzania tu walio na uraia kwenye nchi nyingne ila kiasili ni watanzania (blood) hawa tu ndo wapewe dual citizenship hizo habari za wakenya, sijui warundi, wanyarwanda wahindi na wengineo kutoka makwao kuja kuomba dual citizenship ya Tanzania hiyo hapana kabisa ni very soon nchi itajaa raia wahamiaji na kutusababishia mambo ya ajabu yasiyo eleweka kwenye taifa letu.
Nchi zilizotuzunguka zina changamoto kubwa ya ardhi wote kitakacho waleta huku ni ardhi tu hakuna lolote lile la ziada au zaid ya hilo.
 
Back
Top Bottom